Jumamosi, 7 Novemba 2015


Mh Katule Kingamkono akitembelea miundombinu ya vyanzo vya maji katika kata ya Ikimba vilivyopo katika Kitongoji cha london huko mpakani mwa Kyela na ILEJE

Wakiendelea na zoezi la kuangalia hali ya miundombinu ya vyanzo vya maji


Hii ni sehemu ya bomba linalotakiwa kutiririsha maji kutoka kwenye chanzo hicho cha maji kama anavolionesha Mheshimiwa Kingamkono  


*******************************************************************************
Mheshimiwa Katule Kingamkono jana tarehe 06 Novemba 2015 ameanza rasmi utekelezaji wa Ilani ya CCM chama kilichomuweka madarakani kwa  ridhaa  ya wananchi wa kata ya Ikimba kupitia sanduku la kura katika uchaguzi mkuu  uliofanyika Octoba 25 mwaka huu Tanzania nzima.. 
Diwani huyo  ametembelea chanzo cha maji katika mto mwega kilichopo  katika kijiji cha Kapeta kitongoji cha London wilayani Ileje ambayo muda mrefu hayatoki kwenye mabomba hasa ya wananchi wa kata ya Ikimba.
Akiongea na Mwandishi mkuu wa mtandao wako wa nyumbani mheshimiwa Kingamkono amesema"Lengo la kutembelea vyanzo hivyo amesema kuwa anataka kujua changamoto na kujua sababu kwanini wananchi hawapati maji ili akiapishwa akajenge hoja kwenye vikao vya baraza la madiwani vitakapoanza". 
Mheshimiwa Katule aliongeza kwa kusema katika ziara hiyo ya uchunguzi amegundua   kuna baadhi ya maeneo kuna mabomba ambayo yametoboka yaliokuwa yakipeleka maji Ikimba yanahitaji kuyarejesha kwenye hali ya kawaida. 
Wakati huo huo mheshimiwa Katule Kingamkono ni miongoni mwa Madiwani waliochukua fomu ya kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kyela ambayo ilikuwa ikishikiliwa na Gabriel Martin Kipija aliemaliza muda wake

Imeandikwa na; Puyol B Mwasampeta  (0757337870)
Imehaririwa na ; Martin Emanuel  (0716879949)

Jumatatu, 19 Oktoba 2015

Timu ya MPUNGA CITY wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi Bwana Bedoni Gwatengile kabla ya fainali

Timu ya ISAMBULA FC wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi Bwana Bedoni Gwatengile kabla ya fainali

Bedoni Gwatengile akisoma risala kwa niaba ya Ezekiel Gwatengile wakati wa fainali za GWATENGILE CUP huko BUSOKELO
Bwana Bedoni Gwatengile akifuatilia kwa makini mchezo wa fainali ya GWATNGILE CUP

Mabingwa wa GWATENGILE CUP 2015 wakishangilia kikombe baada ya kukabidhiwa na Mgeni rasmi Bwana Bedoni Gwatengile jana huko BUSOKELO 
Bwana Bedoni  Gwatengile kwa niaba ya Ezekiel Gwatengile amekabidhi zawadi kwa mabingwa wa ligi ya GWATENGILE CUP  ambao ni timu ya Isambula Fc ambao ndio mabingwa wa ligi hiyo kwa kuwanyuka wapinzani wao mabingwa wa kihistoria Mpunga city goli moja lilofungwa na Lughano Mwantingo kwa njia ya penalti baada ya mabeki wa Mpunga city kuunawa mpira katika eneo la hatari wakati wa mechi ya fainali hiyo iliyokuwa na upinzani wa hali ya juu 
Zawadi kwa washindi wa ligi hiyo zilizokabidhiwa na Bwana Bedoni Gwatengile ambaye alikuwa mgeni rasmi ni kama ifuatavyo
1.Isambula kikombe cha dhahabu na seti moja ya jezi 
2.Mpunga City seti moja ya jezi 
3.mpira mmoja. 
Akikabidhi zawadi hizo Bedon Gwatengile kwa niaba ya Ezekiel Gwatengile amesema kuwa zawadi alizotoa haziwezi kulingana na thamani ya kazi walioifanya uwanjani ila zawadi hizo ni ishara tu ya kuwatambua washindi.
Amesema kuwa kama Mungu atampa uhai ataweka ligi ya jimbo mwakani itakayozishirikisha mshindi wa kwanza na wa pili wa kila kata ambapo jumla ya timu ishirini na nne(24), amewataka vijana kujituma ili waweze kupata ajira kupitia michezo na amesema ataviomba vyombo vya habari kuitangaza ligi hiyo ili wachezaji wapate soko.

Mwandishi ;Aidan Mwasampeta 0757337870
Mhariri; Martin Emanuel 0769858521
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la  MIICO Bwana ADAM SIWINGWA akiwaelekeza jambo baadhi ya wakulima waliohudhuria semina hiyo wilayanio Kyela juzi 
 Mkurugenzi wa Shirika la MIICO akiwapatia mafunzo wanakulima waliohudhuria semina hiyo 


Bi Catherine Mlaga akiwezesha semina kwa wanakijiji waliohudhuria semina iliyoandaliwa na shirika la MIICO
Majadiliano ya vikundi yakiendelea katika semina hiyo yakisimamiwa na Bi Catherine Mlaga
Mkuu wa wilaya ya Kyela Bi Thea Ntara akizungumza wakati wa uzinduzi wa semina hiyo ya uwezeshwaji kwa wakulima wa mpungawilayani Kyela




Mkuu wa wilaya akiwa na Kaimu afisa kilimo wa wilaya ya Kyela Bwana Paulo Sheyo wakati wa Semina hiyo


Mkuu wa wilaya Kyela akiwakabidhi baiskeli zilizotolewa na shirika la MIICO kwa wakulima waliohudhuria semina hiyo ya uwezeshaji wakulima wa kilimo cha mpunga wilayani Kyela
Shirika lisilo la kiserikali la MIICO kutoka jijini Mbeya juzi tarehe 16.10.2015 liliendesha semina ya kuwajengea uwezo baadhi ya wakulima wa kilimo cha mpunga wilayani Kyela
Semina hiypo iliyojumuisha washiriki ambao ni Wakulima kutoka vijiji kumi na sita ambavyo ni Katumba,Mpunguti, Isanga,Tenende, Bwato, Isuba,Makwale, Mahenge, Ngeleka, Katela, Kanga,Kafundo, Mubunga, Kingili,Ngana na Mpunguti ya Makwale. 
Mfanyakazi na mwezeshaji  wa shirika la Miico lenye makao makuu jijini Mbeya nane nane  Bi Catherine Mlaga amesema kuwa shirika hilo linafanya kazi na wakulima wa mikoa minne ambayo ni Morogoro,Iringa, Rukwa na Mbeya na wilaya sita zinanufaika na miradi yao. 
Pamoja na kuwapatia wakulima mafunzo jinsi ya uzalishaji wa mpunga pia shirika la MIICO limetoa baiskeli kumi na sita (16) kwa vijiji vinavyonufaika na mradi huo. 
Akikabidhi baiskeli hizo mkuu wa wilaya ya Kyela bi Thea Ntara amelishukuru shirika la MIICO kwa kuja wilayani Kyela na kuwafundisha wakulima wa zao la mpunga na kuwaomba MIICO kuendelea kufanya hivyo mara kwa mara wilayani Kyela. 
Ameliomba shirika hilo kuwapeleka baadhi ya wakulima nje ya nchi ili wakajifunze na kubadilishana mawazo na wakulima wa mpunga wa nje ya Tanzania. 
Mkuu wa wilaya pia  amewaomba wakulima hasa wanaume kutowanyanyasa wake zao hasa kipindi cha mavuno ambapo amesema kuwa wanaume wengi wakivuna mpunga wanakuwa wakali kitu ambacho kinasababisha mpunga kuisha bila mwanamke kujua na kuleta mfalakano ndani ya nyumba.
Mkuuwa wilaya hakusita kuwaomba wananchi wa wilayani Kyela na Nchini kwa ujumla kushiriki kwa amani katika zoezi lijalo la Uchaguzio mkuu Tanzania kwa kutimiza wajibu wao na kufuata na kutii sheria za uchaguzi...Amesisitiza sana wajibu wa wananchi katika kuilinda amani yao.... 

Mwandishi ;Aidan Mwasampeta 0757337870
Mhariri; Martin Emanuel 0769858521