Jumapili, 7 Septemba 2014


Mwenyekiti wa kamati ya afya Aga Khan Mbeya (kushoto)Sultan Thawer, akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro kabla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya tiba kwa Halmashauriya Wilaya ya Kyela na nyingine tatu za Mkoa wa Mbeya.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro,akisaidiwa na Mganga mkuu wa Mkoa,Dk. Seif Mhina,Katibu tawala Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja na Mwenyekiti wa Kamati ya afya Aga Khan Sultan Thawer wakikata utepe kuashiria kukabidhi msaada wa vifaa hivyo.

Picha ya pamoja
HOSPITALI ya Aga khan ya Mbeya imetoa msaada wa vifaa tiba kwa Hospitali na vituo vya afya katika Halmashauri nne za Mkoa wa Mbeya vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 300. Msaada huo ulikabidhiwa na uongozi wa Hospitali hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro kwa niaba ya Halmashauri husika katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkapa uliopo Sokomatola jijini hapa. Mratibu wa Mradi wa tuunganishe mkono pamoja(JHI) Mkoa wa Mbeya, Abel Kide, ambaye pia ni Meneja wa Hospitali ya Aga Khan alisema Halmashauri zilizonufaika na mradi huo ni pamoja na Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Kyela, Mbozi na Momba. Kide alizitaja Hospitali na zahanati zinazopatiwa vifaa hivyo kuwa ni Zahanati ya Ngana na Hospitali ya Wilaya ya Kyela(Kyela), Zahanati ya Iyunga na kituo cha Afya Kiwanja Mpaka(Mbeya jiji), Hospitali ya Wilaya ya Mbozi(Vwawa)na Zahanati ya Ivuna iliyopo wilayani Momba. Alivitaja vifaa hivyo kuwa ni Vitanda vya kujifungulia wajawazito, vitanda vya wagonjwa wa kawaida, Mashine za kuchemshia vifaa vya hospitalini, Mashine ya kumpa joto mtoto aliyetoka kuzaliwa, Mashine ya Ultra Sound,Mashine ya kumtolea uchafu mtoto mchanga,mashine za kupima uzito, joto, urefu na Presha na kwamba vyote jumla vinagharimu zaidi ya shilingi Milioni 300. Kide alisema lengo la kutoa msaada huo ni kuboresha afya ya mama mjamzito, mtoto mchanga na mtoto aliyechini ya miaka mitano ikiwa ni pamoja na kusogeza huduma za afya karibu na wananchi hususani kuokoa vifo vinavyotokea wakati wa kujifungua. Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbasi Kandoro alipongeza Hospitali ya Aga Khani kwa Msaada waliotoa katika Halmashauri hizo na kuziomba taasisi zingine kuungana na Serikali katika mpango wa kuhakikisha vifo vya Wanawake wajawazito, watoto wachanga na waliochini ya umri wa miaka mitano vinapungua. Kandoro alisema mkakati wa kupunguza vifo hivyo hautafanikiwa ikiwa utakuwa ukifanywa na sekta moja ya afya pekee bali kwa kushirikisha sekta zingine binafsi za serikali, viongozi wa dini na vyombo vya habari. Aliongeza kuwa ili kukomesha kabisa vifo hivyo, Halmashauri zitenge bajeti za kununua mfumo wa huduma tembezi(Mobile clinic) ili ziweze kufika hata maeneo ambayo hakuna huduma ya afya kwa kuwasogezea wananchi huduma ili waweze kupata msaada wa matibabu wakati wowote. Sambamba na kupokea msaada huo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya alizindua Mpango wa utekelezaji wa kupunguza kasi ya vifo vitokanavyo na matatizo ya uzazi, watoto na watoto waliochini ya umri wa miaka mitano. Kandoro aliongeza kuwa mkakati huo ni maagizo ya Raisi wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Mkakati wa kitaifa uliofanyika Mei 15 Mwaka huu ambapo aliagiza Kila Mkuu wa Mkoa kuutafakari mkakati huo kulingana na mazingira wanakotoka.
CREDIT;MBEYA YETU

Jumatatu, 1 Septemba 2014


Wanafunzi wakipakizwa kwenye lori kupelekwa Kittuo cha Polisi

Akari kituo cha polisi Kyelai wakijadili jambo

Wanafunzi wakiwa kwenye lori tayari kupelekwa kituoni

Wanafunzi wakiwa wamefikishwa nje ya Kituo cha polisi Kyela

Viongozi wa Serikali Kyela wakiongea na wanafunzi kituoni Polisi Kyela.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya aya Kyela ndugu Gabriel Mwakalinga(KIPIJA)akiongea na Mwandishi wetu

Mwanafunzi wa KEIFO Livingstone Msusi akiishukuru Serikali kwa kumrekebisha

Mwanafunzi Salome Mwaiposa akizungumzia tukio hilo kwa kuwaasa wazazi washirikiane na Serikali
KATIKA kuhakikisha elimu inapewa kipaumbele na kuongeza ufaulu kwa Wanafunzi Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya,Halmashauri hiyo imeanzisha mkakati maalumu wa kuwakamata watoto watoro. Hayo yalibainishwa juzi na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Gabriel Kipija, alipokuwa akizungumza na Mbeya yetu kuhusu mikakati ya kuongeza ufaulu kwa Wilaya hiyo. Kipija alisema hali ya utoro kwa wanafunzi ilikithiri sana kwa kutohudhuria masomo na kuzurura ovyo mitaani jambo lililopelekea Halmashauri hiyo kushika nafasi ya mwisho kimkoa katika matokeo ya hivi karibuni ya kidato cha Nne. Alisema katika Operesheni iliyofanyika wiki mbili zilizopita ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Magreth Malenga, yeye mwenyewe na Mkurugenzi wa Halmashauri walifanikiwa kuwakamata wanafunzi 500 wa shule za Sekondari ndani ya siku moja. Alisema katika siku hiyo Wanafunzi wa shule mbali mbali za Sekondari Kyela Mjini walikamatwa kwa uzururaji wengi wao wakiwa kwenye sare za shule lakini hawakuhudhuria masomo na kuwafikisha kituo cha polisi kwa kosa la utovu wa nidhamu. Alisema kitendo cha kuwafikisha polisi wanafunzi hao kimeibua mwamko mkubwa wa wanafunzi kuhudhuria masomo darasani pamoja na kuwahi ambapo hivi sasa hakuna mwanafunzi anayeonekana barabarani kuanzia saa moja asubuhi tofauti na awali. Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Keifo iliyopo Wilayani Kyela ambao walikumbwa na mkasa huo, mbali na kukiri kufanya vitendo hivyo tofauti na matarajio ya wazazi pia walipongeza kitendo cha Halmashauri cha kuwakamata na kuwapeleka Polisi. Livingstone Msusi(15) mwanafunzi wa kidato cha Kwanza Keifo Sekondari alisema yeye binafsi alikumbwa na kamata kamata hiyo lakini hivi sasa amejirekebisha na kuwa wa kwanza kuwahi shule tofauti na awali ambapo alikuwa hafiki kabisa. Salome Mwaiposa(14) alisema tangu operesheni hiyo ifanyike amekuwa na maendeleo mazuri darasani kutokana na kuhudhuria vipindi vyote na kwa wakati unaostahili. Aidha baadhi ya wanafunzi waliwatupia lawama wazazi kwa kutofuatilia maendeleo ya watoto wao mashuleni ikiwa ni pamoja na kuwahimiza kwenda shule jambo lililochangia kuongezeka kwa utoro na kujiingiza katika shughuli hatarishi mitaani. Walisema ili kukomesha kabisa utoro wa wanafunzi mashuleni ni bora wazazi wakatoa ushirikiaono kwa Serikali kwa kutoa taarifa endapo wanakuwa na watoto ambao husumbua kusoma na kuwaletea kesi wazazi kutokana na kujiingiza katika magenge ya uhalifu. CREDIT;MBEYA YETU