Ijumaa, 30 Januari 2015


Mkuu wa Wilaya ya Kyela Bi Simalenga katikati mwenye suti Nyekundu,kushoto ni mwakilishi wa Mwenyekiti Kamati ya shule na Nyuma kabisa ni Mkuu wa Shule Bwana N.Sedekia pamoja na Wanafunzi na Wageni Wengine katika picha ya pamoja kwenye Tranfoma walipochukulia Umeme kuupeleka Shuleni mita chache kutoka hapo

Mkuu wa Wilaya akizindua kwa kuwasha Swichi kuu(Main Switch) Shuleni Mwaya

Mkuu wa Wilaya , Mwenyekiti wa Kamati ya shule, mkuu wa Wilaya na Kiongozi wa Skauti shuleni wakielekea kwenye Tranfoma palipochukuliwa Umeme
Mkuu wa wilaya ya Kyela Bi Magreth Simalenga leo asubuhi amezindua Nishati ya umeme katika Shule ya Sekondari Mwaya iliyopo Tarafa ya Ntebela Wilayani Kyela.Nishati ya Umeme katika Shule hiyo imekuwa ni moja ya changamoto ya muda mrefu kwa Waalimu na Wanafunzi hasa kwa kuzingatia kuwa shule hii imekuwa ikipata msaada kutoka kwa wadau mbalimbali. Miaka michache iliyopita Shule ya sekondari Mwaya ilipata msaada wa Kompyuta Mpakato kutoka shirika la Kimataifa lililoko nchini Marekani liitwalo Chocolate.
Hata hivyo licha ya msaada huo na mingine mingine mingi shule hiyo imekuwa ikikutana na Changamoto kubwa ya nishati hasa ya Umeme kwa ajili ya kusaidia uendeshaji na uendelezaji wa misaada hiyo ili kuleta tija kwa Wanafunzi hao. Umeme huo uliochukuliwa kutoka mita chache shuleni umezinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kyela na kushuhudiwa na wanafunzi na Mkuu wa Shule Bwana.N.Sedekia na Mwenyekiti wa Kamati ya shule.
Kupatikana kwa Umeme huo kunatarajiwa kuchangia kuongezeka kwa kiwango cha ubora wa Elimu itolewayo shuleni hapo na pia kupunguza Uzembe wa wanafunzi kwa maendeleo yao Binafsi.

Jumamosi, 10 Januari 2015

Hali ya Sintofahamau ilitokea wilayani Kyela siku a January 8 mida ya saa tisa alasiri katika mamlaka ya mji mdog na maeneo ya ofisi za CCM wilayani Kyela ambapo Askari wa kutuliza ghasia(FFU)kutoka jijini Mbeya ilibidi waingie kazini. Hayo yalifanyika mbele ya Mbunge na Waziri wa Uchukuzi Dr.Harison Mwakyembe
Mtandao wako wa Nyumbani ukiongea na baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wametuhabarisha kuwa Vurugu hizo zimesababishwa na Kitendo cha Chama chA Mapinduzi kutaka kuongeza wajumbe wanne katika uchaguzi wa Baraza la Mji mdogo waKyela ambao ni pamoja na mbunge wa jimbo hilo Dr.Harison Mwakyembe na madiwani wa CCM watatu hivyo kuwa na wajumbe wa ziada wanne . Mashuhuda wamezidi kudpokeza kuwa sababu kubwa za Vurugu na Tfrani hizo zilizopelekea Mheshimiwa mbunge kutupiwa mawe ni;
Kwanza, Kisheria wajumbe hao wanaruhusiwa kuwa wajumbe wa Baraza la Mamlaka ya mji mdogo lakini hawatakiwa kushiriki katika kuunda Baraza hilo maana bado halijaundwa .
Pili, Kwanini upande wa Madiwani watatu wote watoke Chama Cha Mapinduzi?
Hata hivyo uchaguzi huo uliahirishwa ili wataalamu wa Sheria wakatafsiri upya Sheria na kuwezesha Barza la mji mdogo kuundwa. Katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa ndani ya mamlaka hiyo Chama cha Demikrasia na M,aendeleo kimetwaa viti 29 na Cham cha Mapinduzi kimetwaa viti 26 hivyo kuonesha waziwazi kuwa CHADEMA Inaweza kushinda na kuliongoza Baraza la Mamlaka ya mji mdogo Kyela.
Wakati huohuo MWAKYEMBE AWAONYA CHADEMA
Jana akizungumza na clouds FM amewataka Chadema kuacha ujinga wa kuchukua watu toka mkoa wa kilimanjaro na kwenda kupiga kambi Kyela.
Mh Mwakyembe amesema CHADEMA Kyela iache kuwatumia vijana toka Moshi waliopiga kambi Kyela!! Ameyasema haya wakati akihojiwa na Clouds kwenye Power Breakfast!!
Amesema ni ujinga kwa chama kikuu cha upinzani kuendelea kutumia wakazi wa mkoa wa kilimanjaro kukinadi chama kwani hawajui tamaduni za makabila mengine hivyo ipo siku wataumbuka.
Amedai kama si huruma yake wachaga hawa toka machame walioenda Kyela kumchafua angeweza kuwapoteza kabisa na amewakanya kutokufika tena jimboni huko kwa shughuli za kisiasa kwani licha ya kuwa anapendwa na wanakyela wenyewe pia Tanzania nzima inaona kazi anayoifanya hivyo si rahisi kulipta jimbo hilo kama wanavyodhani.
Amewataka kutafuta watu wasomi wanaojua statistics/Takwimu ili wawaelekeze mahali pa kwenda kwa kutumia Takwimu si wanakurupuka tu

Jumatano, 7 Januari 2015

Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya kyela wamekiri kuiingiza serikali hasara kwa kutosimamia ipasavyo utekelezaji wa miradi ya TASAF awamu ya kwanza na ya pili, hali iliyosababisha baadhi ya miradi hiyo kujengwa kwa kiwango cha chini kwenye maeneo mbalimbali katika kata zao. Wakizungumza wakati wa uzinduzi wa awamu ya tatu ya mradi wa TASAF wilayani Kyela, madiwani wa halmashauri hiyo wamesema sababu kubwa zilizosababisha Hasara hizo ni pamoja na Ukosefu wa elimu ya kutosha kwa madiwani pamoja na Uelewa mdogo wa wananchi kuhusiana na miradi ya TASAF ulisababisha awamu ya kwanza na ya pili kutotekelezwa kwa kiwango kinachotakiwa, lakini katika awamu ya tatu ya TASAF baada ya kuelimishwa pamoja na uzoefu walionao hawakusudii kurudia makosa. Waratibu wa TASAF ngazi ya wilaya, mkoa na taifa wamesema kuwa awamu ya tatu inakusudiwa kuzisaidia kaya masikini ambazo zitakidhi vigezo vilivyowekwa.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya kyela, Gabriel Kipija ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa awamu ya tatu ya TASAF wilayani kyela amewataka madiwani na watendaji wa halmashauri hiyo kujipanga upya ili wasirudie makosa yaliyojitokeza kwenye awamu zilizotangulia.

Jumanne, 6 Januari 2015

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais (Kazi Maalum),Prof. Mark Mwandosya (wa pili kulia) akipata maelezo ya Mradi wa Umwagiliaji wa Mbaka.Utakapo kamilika Mradi huo utakuwa na uwezo wa kumwagilia hekta 600 kwenye vijiji vya Mbambo,Kambasegele,Katela,na Kapula-Mpunguti.Wananchi 1300 watanufaika na Skimu hii.Wengine pichani kutoka kulia ni Gideon Mapunda,Afisa Kilimo,Ndugu Said Mzeru,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Busokelo na Mhe. Alfred Mwakasapi,Diwani wa Kata ya Kambasegela;wakiwa kwenye banio la chanzo cha mradi kwenye Mto Mambwe.

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais (Kazi Maalum),Prof. Mark Mwandosya (wa pili kutoka kushoto) akipata maelezo ya utekeelezaji wa miradi ya umwagiliaji Busokelo kutoka kwa Afisa Umwagiliaji wa Halmashauri,Ssid Majula,wa nne kutoka kushoto.

Waziri Mwandosya akagua mfereji mkuu wa skimu ya umwahgiliaji ya Mbaka

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) Profesa Mark Mwandosya akipita kwenye kivusha maji cha Mradi wa umwagiliaji Katela - Ntaba wakati akikagua Miradi ya Ujenzi Busokelo,Rungwe Mashariki, mkoani Mbeya

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi maalumu) Profesa Mark Mwandosya (wa tano kulia) akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Ntaba, Bi. Rebecca Hyera (wa nne kulia) kuhusu sehemu ya Mradi wa Umwagiliaji maji wa Katela - Ntaba ambapo limejengwa ghala la mazao ya mpunga na kakao.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) Profesa Mark Mwandosya akipata maelezo ya Banio la mradi wa umwagiliaji wa Katela-Ntaba.wakati akikagua Miradi ya Ujenzi Busokelo,Rungwe Mashariki, mkoani Mbeya

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) Profesa Mark Mwandosya katika picha ya pamoja na watendaji,viongozi na wananchi baada ya kukagua ghala ya mazao ya Mrafi waumwagiliaji wa Kasysbone-Kisegese.