Juu
 na chini, Dr. Mary Mwanjelwa akipandisha bendera katika tawi hilo la 
Mwanjelwa ambako mashabiki wa timu ya Mbeya City, walimwalika kuwa mgeni
 rasmi.
 Viongozi wa Jiji la Mbeya wakishangilia ilipokuwa ikipanda bendera....
 Mkurugenzi
 wa Jiji la Mbeya, Mussa Zungiza, akizungumza katika hafla hiyo fupi ya 
uzinduzi wa tawi la wakereketwa wa timu ya Mbeya City.
 Kulia
 ni Mwenyekiti wa mashabiki wa Mbeya City FC, Willy Mastala, akifurahia 
baada ya kukabidhiwa fedha taslmi Tsh. 500,000 na Mbunge wa viti maalum 
mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa.
 Mbeya City hoyeeeeee..hoyeeeeee...hoyeeeee
 Mashabiki wa tawi la Mbeya City wakiwa pamoja katika hafla hiyo...
 Meya
 wa Jiji la Mbeya, Athanas Kapunga, akielea protocal za kiuongozi, jambo
 ambalo vijana walionekana kutomwelewa huku wakipiga kelele za 
kutofurahia, baadae wakamshangilia baada ya kusema kuwa Jiji 
litawasafirisha mashabiki kuelekea Arusha tmu hiyo itakapoenda kucheza 
huko...
 Mbunge Dr. Mary Mwanjelwa akiwa ndani ya uzi wa MBEYA CITY
  | 
  
MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa,
amewachangia Sh. 500,000 mashabiki wa timu ya Mbeya City, walioamua kujiunga na
kufungua tawi lao katikati ya Jiji la Mbeya. 
 
Pesa hizo alizikabidhi juzi kwa mashabiki hao ambao walimwalika
kuwa mgeni rasmi wa kufungua tawi la mashabiki wa timu hiyo kutoka eneo la
Mwanjelwa na Kabwe. 
 
Dr. Mwanjelwa alisema kuwa, timu ya Mbeya City imewauganisha na
kutaka tawi hilo, liwe chachu ya umoja na mshikamano kwasababu huwezi
kuzungumza Mbeya bila kutaja Mwanjelwa. 
 
Mwenyekiti wa mashabiki hao, Willy Mastala, alisema tayari tawi
lao lina akiba ya Sh. 450,000 na mashabiki hao wamejipanga kusafiri na
kushangilia timu hiyo popote itakapoenda na gharama zote waliomba ziwe juu ya
Jiji la Mbeya. 
 
Meya wa Jiji la Mbeya, Athanas Kapunga, alisema kuwa Jiji lake
litasafirisha mashabiki wote na bajeti ya timu hiyo tayari ipo na kwamba
amefurahi kusikia kuwa Mbunge Mwanjelwa atakuwa mlezi wa tawi hilo. 
 
Mkurugenzi wa Jiji hilo Mussa Zungiza, alisema kuwa anajisikia
furaha kuona mashabiki wanaendelea kuunga mkono jitihada za Jiji lake
kuimarisha timu ya Mbeya City. 
 | 
 
0 comments :
Chapisha Maoni