WATU wawili wakazi wa Jijini Mbeya wamefariki katika matukio mawili tofati likiwemo la mtu kumfumania binamu yake na mpenzi wake nyumbani kwake katika maeneo ya Inyala jijini hapa.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya, Ahmed Msangi alisema, tukio la kwanza lilitokea siku ya mwaka Mpya (Juzi) majira ya saa 10:00 katika maeneo ya Inyala halmashauri ya jiji la Mbeya.
Alisema kuwa katika tukio hilo, Huruma Laiton alikufa wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa mkoa wa Mbeya baada ya kupigwa mateke na Mme wake baada ya kufumaniwa akiwa chumbani na binamu wa mumewe.
Alisema kuwa marehemu alifumaniwa na mumewe, Mwakabenga Ezekiel mke wake akiwa ndani na Binadamu yake.
Alisema kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika huspitali ya rufaa jijini Mbeya.
Msangi alisema kuwa katika tukio la Pili lilitokea katika maeneo ya Itezi mashariki kata ya Itezi Jijini Mbeya Christopher Myamba, alifariki dunia baada ya kuchomwa kisu shingoni na Ndele baada ya kuzuka ugomvi.
Mgogoro huo ulitokea baada ya marehemu kukutana na kundi la vijana wakiwa wamelewa na kuzuka ugomvi ambao ulisababisha marehemu kuchomwa kisu.
Msangi alisema kuwa mara baada kifo cha marehemu mwili wake umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Rufaa Mbeya.
Alisema kuwa kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linamtafuta mtuhumiwa na ametoa wito kwa wakazi wa Jiji la Mbeya kuwa mwenye taarifa atoe taarifa ili kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo.
Ijumaa, Januari 03, 2014
Unknown
0 comments :
Chapisha Maoni