Mvua zinazoendelea kunyesha wilayani Kyela zinaendelea kuleta maafa mbalimbali ikiwemo watu kupteza maisha na wakazi kupoteza mali na makazi yao.
Mwandishi wa mtandao huu akiwa anatembelea maeneo mbalimbali yaliyoathirika sana ambayo ni BUJONDE,KATUMBASONGWE(NDWANGA) MWAYA (MMWAJA) KAJUNJUMELE(NKILWA) na mengine mengi hadi hivi sasa anasema inakisiwa watu wasiopungua wanne wamepoteza maisha.Mtu mmmoja aliyejulikana kwa jina la MALINDO MWAIPOPO amekufa maji baada ya kusombwa na maji eneo la LUGOMBO MWAYA akijaribu kuvuka kuelekea Mwaya.Pia maeneo ya KATUMBASONGWE(ndwanga) kumeripotiwa kuwa kunadhaniwa watu wapatao watatu wamekufa maji.
"Uswe tukumilwa umwe mkusalala uko"Hii ni kauli ya mama mmoja aliekuwa akiongea kwenye simu akiwajulisha ndugu hali tete ya mafuriko wanavyo athirika, eneo daraja la mto Kiwila lililopo Ipyana maji yakipita juu ya daraja

hili ni eneo la barabara ya kuelekea bandarini huko Kajunjumele


vijana mbalimbali wakujitolea kusafisha daraja la Ipyana.
Hapa ni mbuga ya Tenende watu wakijaribu kupita.Ni hatari sana
hapa ni Kyela jamani na mafuriko ndo hayo

hapa ni eneo la makaburi ya Kyela mjini yamemezwa na mafuriko
EWE MWENYEZI MUNGU TUNAIWEKA KYELA MIKONONI MWAKO.
Jumatatu, Aprili 21, 2014
Unknown
0 comments :
Chapisha Maoni