Jumapili, 25 Mei 2014

IMG_2090
Kama unakumbuka ule moto wa Mbeya City katika michuano ya ligi kuu soka Tanzania bara msimu uliopita basi ndio umehamia huko Sudani katika michuano ya 
Wawakilishi hao wa Tanzania wamehamishia kasi yao katika michuano mipya ya CECAFA Nile Basin Cup, ambapo wameanza vyema mashindano hayo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Academie Tchite ya Burundi.
Mabao ya Mbeya City yamefungwa na washambuliaji hatari Paul Nonga katika dakika ya 15, Mwegane Yeya dakika ya 27 na nyota mpya Them Felix katika dakika ya 37.
Mechi hiyo muhimu kwa Mbeya City fc iliyosuasua kuwasili Sudan kutokana na kucheleweshewa tiketi za ndege imepigwa katika uwanja wa Khartoum-Sudan.
Kikosi cha Mbeya City kilichoanza leo ni Barhan David, Kabanda John, Kibopile Hamad, Julius Deogratius, Yohana Morris, Antony Matogolo, Deus Kaseke, Mazanda Steven, Paul Nonga, Mwegane Yeya na Them Felix `Mnyama`.
 Mbali na mchezo wa Mbeya City fc, majira ya saa 2:00 usiku  AFC Leopard ya Kenya itakabiliana na Enticelles ya Rwanda.

0 comments :

Chapisha Maoni