Ijumaa, 10 Aprili 2015




Diwani wa kata ya Bujonde Paul Rameck Mwambafula ameunga mkono jitihada zinazofanywa na Asasi isiyokuwa ya Kiserikari ya TUZA FOUNDATION kwa kushirikiana na ofisi ya Maliasili kung’oa mitego yote ya samaki katika kijito Mangala kilichopo kijiji cha Isanga.
Kauli hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na mwaandishi wa habari baada ya TUZA kufanya zoezi hilo hivi karibuni katika kijito hicho ambacho kinamwaga maji yake kwenye ziwa nyasa.
Amesema yeye binafsi pamoja na wananchi wa kijiji cha Isanga hawakuwa na uwelewa kuwa kuweka mitego kwenye kijito hicho kilikuwa ndiyo chanzo cha maji kujaa kwenye mashamba na kusababisha mafuriko kwenye makazi ya watu,pamoja na magonjwa ya milipuko na ameomba zoezi hilo liwe endelevu.
Kwa upande wake mwananchi wa kijiji hicho BONFACE MWAKYALABA,amewapongeza Ofisi ya Maliasili kwa kazi hiyo,amesema kuondolewa kwa mitego hiyo imesaidia kuondoa adha ya mafuriko na itasaidia kuondokana na magonjwa ya Malaria,Taifodi na Fangasi.
CREDIT TUYAJUE HAYA!!!