Jumatano, 7 Mei 2014

boko
Hofu inazidi kutanda nchini Nigeria na matumaini ya kuwapata wanafunzi wa kike zaidi ya 200 waliotekwa nyara na kundi la Boko Haram yanapungua baada ya kiongozi wa kundi hilo kutangaza kuwa amepanga kuwauza.
“Nimewateka nyara wasichana wenu. Nitawauza sokoni, kwa jina la Mungu.”Alisema kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau kwenye video ambapo aliongea kwa lugha ya Hausa na tafsiri yake imetolewa na CNN.
“Kuna soko la kuuza binadamu. Mungu anasema inabidi niwauze. Ameniamuru niwauze. Nitawauza wanawake. Huwa nauza wanawake.” Aliongeza mtu huyo.

Takribani watu 1,500 wameuawa mwaka huu na kundi hilo ambalo maafisa wa Marekani wameeleza kuwa linasaidiwa kimafunzo na watu wenye uhusiano na kundi la Al Qaeda.
Kundi hilo limedai linawateka wanafunzi wa kike ikiwa ni mkakati wao haramu wa kupinga elimu ya magharibi.
Wananchi nchini Nigeria wameendelea kuandamana wakiishinikiza serikali kuharakisha mpango wa kuwaokoa na kuwalinda watoto wao na kundi hilo hatari.
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan amesema atafanya awezalo kuwaokoa wasichana hao.

Jumatatu, 5 Mei 2014


Kamati ya kuratibu Harambee ya kuchangia maafa wilayani Kyela katika picha ya pamoja

Miss Tanzania 2001 na mwanamitindo aishie nchini Marekani Happiness Magesse akikabidhi fedha Taslimu shilingi milioni moja kwa Mwenyekiti wa Kamati ya kuratibu Harambee Prof .Leonard  Mwaikambo



Miss na Mwanamitindo Happiness Magesse akiteta jambo na Martin Emanuel (Mwanzilishi na blogger wa KYELANyumbani blog)  

 Mbunge na Waziri wa Uchukuzi Dr.Harrison Mwakyembe ameowaongoza wanaKyela waishio jijini Dar Es Salaam na miji ya karibu katika Harambee ya uchangiaji kusaidia wananchi wilayani Kyela walioatirika na mafuriko makubwa na yaliyoleta athari mbalimbali na kubwa sana yaliyotokea mwishoni mwa mwezi April mwaka huu.
Prof Leonard Mwaikambo wenyekiti wa Kamati iliyoundwa na wanakyela kuratibu Harambee hiyo akitoa taarifa ya tathmini ya iliyofanyika na Ofisi ya mkuu wa wilaya katika harambee hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa mkabala na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM)amesema"Mafuriko hayo ambayo hayajawahi kutokea wilayani kwa miongo zaidi ya 4 yameleta athari mbalimbali kwa jamii kiuchumi na kijamii.Mfano Shule zaidi ya 3 za sekondari na msingi zimeathirika vibaya ,pia miundombinu imeharibiwa vibaya ikiwemo madaraja na barabara.Prof.Mwaikambo aliongeza kuwa tathmini hiyo inaeleza kuwa watu zaidi ya elfu ishirini na nne (24000) wameathirika kutokana na maafa hayo
Hivyo jumla ya kiasi cha zaidi ya bilioni 2 na milioni 800 zinahitajika kukabiliana na athari za mafuriko wilayani humo"
Baada ya taarifa hiyo kwa ufupi Waziri na mbunge wa jimbo la Kyela Dr.Harrison Mwakyembe aliongeza na kusema kuwa hali ni mbaya sana kwani yeye alifika wilayani na kushuhudia hali ilivyokuwa mbaya .Mfanoalishindwa kwenda Bujonde kwa sababu maji yalikuwa ni mengi kiasi cha mtu wa futi 6 anazama.Hadi nyumbani kwa Diwani wa kata hiyo kulikuwa kumejaa maji ambapo mashamba na mali kama mifugo vilikuwa vimeathirika sana.Waziri aliongeza kusema"Tunamshukuru Mungu mamba hawakuweza kuwaathiri binadamu maana kasi ya amaji ilikuwa kubwa sana kiasi ambacho mamba walishindwa kuishi kwa uhuru na kusababisha madhara zaidi "
Dr.Mwakyembe aliongeza kuwa Shule ya sekondari Mwaya imeathirika zaidi ambapo vitabu na vifaa vya maabara vimeharibika kabisa hivyo wanafunzi kushindwa kusoma Sayansi kabisa.
Dr Mwakyembe pia aliwashukuru watu,makundi na Taasisi mbalimbali zilizochangia kusaidia wahanga wa maafa haya kama Kanisa la Moraviana Tanzania,Kanisa la Roman Catholic Kyela ,Taasisi ya Pambana Saidia Jamii (SCSA) ,Kyela Media na Kyela Members,Umoja wa Wasanii Kyela,SUMATRA na wengine wengi
Baada ya maelezo hayo mafupi Mwenyekiti wa kamati ya Harambee Prof.Mwaikambo aliongoza Harambee hiyo ambapo watu wengi walitoa pesa na nguo na watu kuchangia mawazo pia.
Pia aliyekuwa Miss Tanzania 2001 Happiness Magese alichangia sare za shule 200 na kiasi cha pesa cha Shilingi milioni moja kwa kuanzia.
Hadi mwisho wa harambee ambayo itafanyika tena tarehe 1 mwezi wa 6 2014 kiasi cha shilingi milioni hamsini na tisa zilikuwa zimepatika ikiwa ni fedha Taslim na ahadi.
 Jaji Mwaikugile akitoke kijiji cha Itunge  akiongea kwenye Harambee












Mzee na mfanyabiara Mwamafupa akichangia shilingi laki moja








Ijumaa, 2 Mei 2014



Tukiwa tumesherekea miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar je unamjua mtu aliyetunga jina la Tanzania??? Pata historia ya namna mtu alivyofanikiwa kupata jina la T A N Z A N I A.
Sherehe za Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar huwa tunasherekea kila Mwaka Tarehe 26/04/ lakini Tangu mimi binafsi nipate ufahamu na kuanza kushuhudia sherehe za Muungano nimekuwa nikisikia kuwa jina la Tanzania lilipendekezwa na Watanganyika, Wazanzibar na Raia wengine wa nje lakini sikuwahi kumjua mtu ambae alibuni jina hili tamu la Tanzania.
Huyu bwana aliyebuni jina la Tanzania ni Muhindi na Dini yake ni AHMADIYA MUSLIM JAMAAT TANZANIA majina yake ni MOHAMMED IQBAL DAR.
Mohammed alizaliwa Mkoani Tanga miaka ya 1944,Baba mzazi wa Mohammed alikuwa Daktari huko mkoani Morogoro alikuwa anaitwa Dr. T  A DAR  alikuwa Tanganyika kuanzia mwaka 1930.
Mohammed Iqbal Dar alipata elimu yake ya Msingi Mkoani Morogoro shule ya Msingi H H D AGAKAN kwa sasa ni Shule ya Serikali na baada ya Hapo alikuja baadae kujiunga na Chuocha Mzumbe akasoma Kidato cha Kwanza mpaka cha Sita.
Aliingiaje kwenye shindano la kupendekeza  jina la Muungano kati Tanganyika na Zanzibar,Mohammed anasema alikuwa Maktaba akijisoma gazeti la Tanganyika Standard siku hizi Daily News akaona Tangazo linasema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unafahamika kama Republic of Tanganyika and Zanzibar jina likaonekana refu sana kwa hiyo Wananchi wote wakaombwa Washiriki kwenye shindano la Kupendekeza jina moja litakalo zitaja nchi zote mbili yaani Tanganyika na Zanzibar
Mohammed Iqbal Dar anasema aliamua kuingia kwenye Shindano na hivi ndivyo alianza Safari ya Kubuni Jina la Muungano,Kwanza anasema alichukua karatasi akaandika Bismillah Raahman Rahimu hii ni kutokana na Imani yake na baada ya hapo akaandika jina laTanganyika baada ya hapo akaandika Zanzibar halafu akaandika jina lake Iqbal halafu akaandika jina la Jumuiya yake ya Ahmadiya baada ya Hapo akamrudia tena Mwenyezi Mungu akamwomba amsaidie ili apate jina zuri kutoka katika majina hayo aliyokuwa ameyaandika.
Baada ya hapo Mohammed Iqbal Dar alichukua herufi tatu kutoka Tanganyika yaani TAN na kwa upande wa Zanzibar akachukua Herufi tatu za Mwanzo ZAN ukiunganisha unapataTANZAN alivyoona hivyo akachukua  herufi ya kwanza katika jina lake la Iqbal na akachukua A kutoka jina la dini yake yaani Ahmadiyya kwa maana hiyo ukiongeza herufi hizi mbili na A kwenye TANZAN unapata jina kamili TANZANIA akalisoma jina akaliona ni zuri lakini akajiridhisha pia kwamba akiongeza herufi hizo za na kwenye TANZAN italeta maana kwakuwa nchi nyingi za Afrika zinaishia na IA.
 mfano EthiopIA,ZambIA,NigerIA,TunisIA,SomalIA,GambIA,NamibIA,LiberIA,MauritanIAalivyoona hivyo akaamua apendekeze kuwa jina TANZANIA ndio litumike kuwakilisha nnchi hizi mbili yaani Tanganyika na Zanzibar kwa maana hiyo jina TANZANIA limezaliwa kutoka majina manne majina hayo ni Tanganyika,Zanzibar,Iqbal na Ahmadiyya
Mohammed Iqbal  Dar baada ya kupata jina hilo akalituma jina hilo kwenye kamati ya kuratibu  Shindano
Baada ya Muda mwingi kupita  baba yake na Mohammed Iqbal Dar alipokea Barua nzito kutoka serikalini ikiwa inasomeka kama ifuatavyo….
                                                               

                                                     REPRESENTED BY THE
                                MINISTRY OF INFORMATION AND TOURISM,TANZANIA
                                                                     TO
                                                  MOHAMED IQBAL DAR
                 IN RECOGNATION OF THE ACHIEVEMENT OF CHOOSING THE NEW NAME FOR THE
                                    UNITED REPUBLIC OF TANGANYIKA AND ZANZIBAR NAMELY
                                                  “REPUBLIC OF TANZANIA”
                 DURING THE NATIONAL COMPETITION DAY IN 19TH NOVEMBER 1964
                                                            I A WAKAL
                              MINISTER FOR INFORMATION AND TOURRISM
Barua hiyo pia ilisema..
Utakumbuka kuwa miezi michache iliyopita ulituandikia kutupa ushauri kuhusu jina jipya la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar  na wewe pamoja na wananchi wenzio 16 ulishauri nnchi yetu iitwe Tanzania.Nafurahi kukuarifu kuwa mshirikiane ile Zawadi y ash.200 iliyoahidiwa na leo nakuletea check ya sh.12/50 ikiwa ni hisa yako katika zile sh.200.Nashukuru sana kwa jitihada ya kufikiri jina la Jamuhuri yetu
Barua ikasainiwa na Idrisa Abdul Wakil Waziri wa Habari na utalii kipindi hicho.
Sasa kwa nini Mohamedi Iqbal Dar anadai yeye kuwa mshindi pekee wakati Barua ilikuwa inaonyeshakulikuwa na washindi wengine 15 ambao nao walishinda,Jibu ni kuwa wakati wa kutolewa kwa Zawadi hizo hakuna aliyejitokeza zaidi ya Bwana Mohammed Iqbal Dar na Bwana Yusufal Pir Mohamed ambaye hata hivyo alikosa sifa baada ya kushindwa kutoa barua ya kumpongeza kuwa ameshinda kwa madai kuwa Barua ameipoteza,hivyo Wizara ya Habari na Utalii iliamua kumtangaza bwana Mohammed Iqbal Dar kuwa Mshindi na kumpatia zawadi yote y ash.200/:pamoja na Ngao.
Bwana Mohammedi Iqbal Dar anasema anachosikitika ni kuwa Mchango wake bado Watanzania hawathamini mchango wake lakini yeye anaipenda Tanzania na anajivunia kuwa Mtanzania japo anadhani dini yake ya Uislamu ndio tatizo hawataki kutambua mchango wake ila anaamini kuwa siku moja ukweli utajulikana
Hayo ni maelezo ya Mohammed Iqbal Dar ambaye kwa sasa anaishi Uingereza kwa kuwa huko ndiko alipata kazi eneo la Birmigham b35 6ps UK,Dar –es-Salaam House,18 TURNHOUSE ROAD,PHONE 44 121-747-9822