Jumamosi, 7 Novemba 2015


Mh Katule Kingamkono akitembelea miundombinu ya vyanzo vya maji katika kata ya Ikimba vilivyopo katika Kitongoji cha london huko mpakani mwa Kyela na ILEJE

Wakiendelea na zoezi la kuangalia hali ya miundombinu ya vyanzo vya maji


Hii ni sehemu ya bomba linalotakiwa kutiririsha maji kutoka kwenye chanzo hicho cha maji kama anavolionesha Mheshimiwa Kingamkono  


*******************************************************************************
Mheshimiwa Katule Kingamkono jana tarehe 06 Novemba 2015 ameanza rasmi utekelezaji wa Ilani ya CCM chama kilichomuweka madarakani kwa  ridhaa  ya wananchi wa kata ya Ikimba kupitia sanduku la kura katika uchaguzi mkuu  uliofanyika Octoba 25 mwaka huu Tanzania nzima.. 
Diwani huyo  ametembelea chanzo cha maji katika mto mwega kilichopo  katika kijiji cha Kapeta kitongoji cha London wilayani Ileje ambayo muda mrefu hayatoki kwenye mabomba hasa ya wananchi wa kata ya Ikimba.
Akiongea na Mwandishi mkuu wa mtandao wako wa nyumbani mheshimiwa Kingamkono amesema"Lengo la kutembelea vyanzo hivyo amesema kuwa anataka kujua changamoto na kujua sababu kwanini wananchi hawapati maji ili akiapishwa akajenge hoja kwenye vikao vya baraza la madiwani vitakapoanza". 
Mheshimiwa Katule aliongeza kwa kusema katika ziara hiyo ya uchunguzi amegundua   kuna baadhi ya maeneo kuna mabomba ambayo yametoboka yaliokuwa yakipeleka maji Ikimba yanahitaji kuyarejesha kwenye hali ya kawaida. 
Wakati huo huo mheshimiwa Katule Kingamkono ni miongoni mwa Madiwani waliochukua fomu ya kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kyela ambayo ilikuwa ikishikiliwa na Gabriel Martin Kipija aliemaliza muda wake

Imeandikwa na; Puyol B Mwasampeta  (0757337870)
Imehaririwa na ; Martin Emanuel  (0716879949)

0 comments :

Chapisha Maoni