MAITI ya kijana aliyejulikana kama Kassim Said Mboya (36), mkazi wa Jijini Dar es Salaam, imekutwa na kete 65 za zinazodhaniwa kuwa ni dawa za kulevya.
Taarifa
zilizolifikia Tanzania daima tangu jana jioni, zilieleza kuwa maiti ya 
kijana huyo, ilikutwa katika basi la kampuni ya Taqwa eneo la Kasulumu 
lililokuwa likitokea Jijini Dar es Salaam nchini Tanzania na kuelekea 
nchini Malawi.
KYELA NYUMBANI blog ilifuatilia na kujua ukweli wake kisha kuwasiliana na kamanda wa 
polisi mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani leo asubuhi, ambaye pia alikiri 
kuwepo kwa maiti hiyo na kumwambia mwandishi wakutane eneo la chumba cha
maiti cha hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya kuona mwili wa 
marehemu huyo.
Kamanda
wa polisi wa mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani, alisema kuwa kijana huyo 
kabla hajafariki, alikamatwa Novemba 7, mwaka huu akiwa ndani ya basi 
hilo lenye namba za usajili T 319 BLZ akiwa na tiketi yenye jina la 
Kassim Mueck Michael.
‘’Awali
basi hilo kabla ya kufika mpakani Kasumulu na abiria kushuka na kuanza 
kufanya taratibu za kuvuka mpaka na kuingia nchini Malawi, marehemu 
alibaki kwenye gari huku afya yake ikizidi kudhoofika’’ alisema Kamanda 
Dwani Athumani.
Alisema
baada ya kuona hivyo, wahusika wa basi hilo walitoa taarifa kituo cha 
polisi ambapo kijana huyo alichukuliwa na kupelekwa katika hospitali ya 
wilaya ya Kyela na kabla hajapata matibabu alifariki dunia.
Alieleza
kuwa, kwa kuwa kijana huyo kabla hajaaga dunia alikuwa na dalili 
zilizogundulika kuwa alikuwa na dawa za kulevya, iliamuliwa mwili huo 
kusafirishwa mpaka hospitali ya Rufaa ya Mbeya ambako ulipasuliwa na 
kukutwa na pipi 65 zinazodhaniwa kuwa ni dawa za kulevya na moja ikiwa 
imepasuka.
‘’Natoa
rai kwa wananchi wa mkoa wa Mbeya na nchi nzima kwa ujumla kufika 
hospitali ya rufaa ya Mbeya kwa ajili ya utambuzi wa mwili wa marehemu 
na kwamba ijulikane kuwa usafirishaji na utumiaji wa dawa za kulevya ni 
hatari kwa afya ya mtumiaji’’ alisema Kamanda Diwani.
Alipoulizwa
kuwa kutokana na mkanganyiko uliowahi kujitokeza katika upotevu na kuwa
dawa zilizowahi kukamatwa awali hazikuwa dawa, alisema kuwa kikosi kazi
chake kimejipanga vema na jitihada za kupeleka kwa mkemia mkuu 
zinafanywa chini ya kikosi kidogo cha ulinzi na usalama cha mpaka wa 
Kasumulu.
Hii
ni maiti ya tatu kukamatwa na dawa zinazodhaniwa kuwa ni za kulevya 
mkoani Mbeya, ambapo shehena ya kwanza ya dawa hizo ilikamatwa mwaka 
mjini Tunduma mkoani hapa mwaka 2006 ikiwa kwenye tumbo la marehemu 
Kombo Siriri.
Shehena
ya pili ya dawa hizo ilikamatwa Desemba 5, 2011 katika hotel ya High 
Class mjini Tunduma, ikiwa katika tumbo la maiti ya Mshanga Mwasala.
Licha
ya ukamataji wa dawa hizo na baadhi ya watuhumiwa wakiwa haia, hakuna 
mtuhumiwa aliyewahi kupatikana na hatia tangu mfululizo wa ukamata dawa 
hizo zinazodhaniwa kuwa ni dawa za kulevya mkoani Mbeya.

 Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani, akitoa 
taarifa kwa waandishi wa habari nje ya ofisi yake huku akiwa na baadhi 
ya askari wa jeshi hilo mkoani hapa.

 Pasi ya kusafiria kijana huyo alizokutwa nazo...


 Kete zilizokutwa tumboni mwa kijana huyo baada ya kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya Mbeya. 

 Kulia ni kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani, 
akiwa amevalia mavazi maalum, kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika 
hospitali ya rufaa ya Mbeya kwa ajili
ya kuona maiti hiyo.

 Maiti ya kijana Kassim Said
Mboya ukiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa
 ya Mbeya baada ya kufanyiwa upasuaji na kutolewa dawa zinazodhaniwa 
kuwa ni za kulevya.

*Wananachi watakiwa kufika Rufaa Mbeya kuitambua maiti ya kijana huyo
*Ni maiti ya tatu kukamatwa ikiwa na kete za namna hiyo
Jumamosi, Novemba 09, 2013
Unknown



0 comments :
Chapisha Maoni