Kocha mkuu wa Azam mwingerezaStewart Hall
Dakika chache baada ya mechi ya Ligi Kuu
Bara kati ya Azam FC na Mbeya City ambapo Azam imechomoa dakika za mwishoni na kuishia sare ya bao 3 kwa 3, Kocha Stewart Hall ametangaza kuachana na
Azam FC.
Hall amesema anaachana na Azam FC baada
ya kupata ofa kubwa iliyomshawishi kuichukua.
Hata hivyo, kabla KYELA Nyumbani ilipata
taarifa za uongozi wa Azam FC kumuambia Hall kwamba hahitajiki.
Hii ni mara ya pili anaondoka, kabla
aliachishwa kazi na kurejea kwao England, baadaye akarudi na kutoa Kenya ambako
aliifundisha Sofapaka.
Azam FC iliyomchukua Boris Bunjac wa
Serbia walishindwana naye na baadaye na kumuita tena ainoe.
 Wachezaji wa Mbeya City wakifanya mazoezi mepesi kabla ya kuanza kwa mchezo wao dhidi ya Azam FC. 
 Mashabiki wengi wao wa Mbeya City
 wakiwa katika misururu mirefu kuingia uwanjani kushuhudia pambano la 
Azam na Mbeya City kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam. 
 Golikipa
 wa Mbeya City akiokoa moja ya hatari zilizoelekezwa langoni mwake 
katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara dhidi ya Azam FC 
unaoendelea kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.
 Mashabiki wa Mbeya City wakishangilia kwa hamasa kubwa.
Alhamisi, Novemba 07, 2013
Unknown


0 comments :
Chapisha Maoni