Jumamosi, 14 Februari 2015


Kikao cha CCM kilichowahusisha Vijana,Waujumbe wa CCM Kata na viongozi wengine wa CCM Wilayani 12/0215 akiwemo Mheshimiwa Waziri na Mbunge wa Jimbo la Kyela Dkt Harrison G.Mwakyembe na Mwenyekiti wa Chama Wilaya mheshimiwa Hunter Mwakifuna. Tumefanikiwa kupata kile kilichozungumzwa ndani ya kikao hicho na wazungumzaji wawili. 1.Mwenyekiti wa CCM wa CCM wilaya ndugu Hunter Mwakifuna
Kikao kilifunguliwa na Mwenyekiti wa CCM Wilayani. Mwenyekiti alitumia muda mwingi kwa kumpamba Mh. Mwakyembe na kusema kwamba CCM Kyela tayari ina Mtambua Mwakyembe kama Mgombea wao 2015,hakuna aja ya kubadilisha wakati anafanya vizuri kwani hii ni nguo? Aliuliza Mwenyekiti.Nimetembea nchi nzima kila mtu anasema Kyela tuna bahati sana kwa kupata Mbunge kama Mwakyembe,Maendeleo aliyoyaleta Mbunge wetu hakuna mbunge mwingine Tanzania,aliendelea kutamba huyo Mwenyekiti.
2.Mbunge waJimbo la Kyela Mh. Dr.Harrison Mwakyembe Mh,Alianza kwa kujigamba mbele ya Wajumbe na kama kawaida yake akanza na ahadi kibao na mambo waliyoyafanya mpaka sasa hivi -Kuna nafasi za kazi 200 zinasubiri vijana wa Kyela
-Mgodi wa makaa ya mawe utafunguliwa mwaka huu na kazi zote watapewa wana Kyela.
-Kila kata tutatoa pikipiki ili kuendeleza chama na kusaidia wakati wa kampeni
-Kila kijiji baiskeli
-Tumetengeneza barabara nzuri na za kudumu na tunaendelea kujenga kwa viwango bora.
-Watu wanasema daraja walijenga wanajeshi wakati mi ndo niliongea na mkuu wa majeshi ili wanajeshi wasaidie.
-Watu wengi Tanzania wananiomba mimi nigombee urais maana wajua kwamba mimi ni mchapa kazi na ninauwezo na kama ikitokea kwamba sitagombea ubunge kyela,nitaakikisha nawaletea mtu wa maana na mchapa kazi kama mimi.
-Kuna upoteshaji mwingi kuhusu mabadiliko ya wizara.Nikwamba kuna matatizo mengi ndani ya huu umoja wetu wa Afrika Mashariki.sasa rais akaona amtume mtu makini na mwenye uwezo na uzoefu si mnajua nilikuwa uko kabla ya kugombea hapa. Mwisho sisi wanyakyusa tukikutana tunapeana maji ya kunywa kama hakuna chakula,kwahiyo kila mjumbe atapata elfu kumi za maji.Asanteni Mwenyekiti alisimama na kufunga kikao kwa kusema HAKUNA MASWALI KIKAO KIMEFUNGWA. Source Mjumbe wa CCM Kata aliyekuwemo ndani ya Kikao