Jumamosi, 10 Oktoba 2015




 Meneja wa Benki ya CRDB Kyela Bwana Lugano Mwambaja akiwa amevalia fulana yenye ujumbe wa kauli mbiu ya Benki hiyo katika kuadhimisha siku ya wateja duniani...AHSANTE SANA
 Wafanyakazi mbalimbali wa Hospitali ya Wilaya Kyela wakiwasikiliza kwa makini wafanyakazi wa Benki ya CRDB Kyekla wakiongozwa na Meneja wao walipoiwakilisha benki ya CRDB katika kuadhimisha WIKI YA MTEJA DUNIANI..

 Wafanyakazi wa benki ya CRDB Kyela wakiwa wamebeba vitu mbalimbali kwa ajili ya msaada kwa wagonjwa  wakiwasili katika hospitali ya wilaya Kyela 
 Meneja wa Mikopo midogo na mikopo ya kati benki ya CRDB Kyela  Bi Akwilina Shirati akiwa ameongozana na mfanyakazi mwenzie walipokuwa wakiwasili hospitalini kutoa msaada wa Sabuni,Vyakula na Mashuka kwa wagonjwa
 Meneja wa benki ya CRDB tawi la Kyela Bwana Lugano Mwambaja akikabidhi msaada wa mashuka uliotolewa na Benki hiyo katika kuadhimisha WIKI YA  MTEJA DUNIANI kwa Muuguzi katika hospitali ya Wilaya Kyela.Picha ya pili akitandika shuka katika kitanda kimojawapo hospitalini hapo .
 Moja kati ya mashuka yaliyotolewa na kukabidhiwa na Benki ya CRDB katika kuonesha jinsi wanavyowajali wateja na wanajamii wanaowazunguka likiwa limetandikwa katika moja ya vitanda katika wodi za Hospitali ya wilaya ya Kyela
 Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya CRDB Kyela wakiwa na baadhi ya Wateja wa benki hiyo walipokuwa katika maadhimisho ya WIKI YA MTEJA DUNIANI yenye kauli mbiu ya AHSANTE SANA katika ofisi za benki hiyo zilizopofanyikia sherehe hizo  
 Vinywaji na vitafunwa maalumu kwa ajili ya kuwashukuru wateja wa benki ya CRDB Kyela


 Meneja wa Benki ya CRDB katika tukio la kulishana keki  na wateja wa benki hiyo tawi la Kyela katika maadhimisho ya WIKI  YA MTEJA DUNIANI 






 Meneja was benki ya CRDB akimkabidhi zawadi ya saa ya ukutani  na fulana yenye ujumbe wa AHSANTE SANA mteja Bwana Charles Luhwavi katika sherehe zilzofanyika katika ofisi za crdb tawi la Kyela

 ******************************************************************************************************************************************************************
Katika kuadhimisha WIKI YA MTEJA DUNIANI jana tarehe 09.10.2015 Benki ya CRDB tawi la Kyela imefanya matukio mawili maalum ikiwa ni kutambua mchango wa wateja na wananchi wa wilaya katika ukuaji na ustawi wa benki hiyo wilayani Kyela ikiongozwa na kauli mbiu iliyobeba ujumbe wa shukrani yaani AHSANTE SANA
Tukio la kwanza lililofanyika mnamo majira ya asubuhi lilikuwa ni kukabidhi misaada mbalimbali kama Sukari , Sabuni,  na Mashuka kwa wagonjwa wa Hospitali ya Wilaya ya Kyela..
 Akikabidhi msaada huo meneja wa Benki ya CRDB tawi la Kyela Bwana Lugano Mwambaja amesema kuwa katika kusherekea WIKI YA WATEJA DUNIANI wao wameona ni vyema wasiwatenge wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya wilaya ya Kyela kwa kuwakabidhi sukari,sabuni,na mashuka na benki hiyo inatambua na kuthamini mchango wao.
Bwana Mwambaja amesema kuwa benki hiyo imekuwa  ikisaidia mambo  mbalimbali ya kijamii kama vile ujenzi wa vyumba vya madarasa vya shule za msingi na sekondari na kusaidia pia madawati , misaada mbalimbali kwa watoto yatima na vitu vingine vingi vinavyoikumba jamii katika kile alichokiita kuthamini mchango wa jamii inayowazunguka katika ukuaji na ustawi kwa benki hiyo wilayani Kyela


Katika hatua nyingine baada ya kutoa msaada katika hospitali ya wilaya ya Kyela wakaendelea kusherekea siku kuu ya WIKI YA WATEJA DUNIANI  ailiyobebwa na kauli mbiu  AHSANTE SANA iliyofanyika   ndani ya jengo la ofisi za Benki hiyo kwa kuwapatia zawadi mbalimbali wateja wao kama vile vitenge, pochi za kiume na za kike,saa za ukutani na za mkononi na vitu vingine mbali mbali. 
Meneja wa biashara wa benki ya CRDB Bwana Misape Tindwa amesema kuwa wanatambua na kuuthamini mchango wa wateja wao ndio maana kila tukio wanashirikiana nao.
Meneja wa Biashara wa benki hiyo amewahamasisha wananchi wa wilaya hiyo kuja kupata huduma mbalimbali za kibenki katika benki hiyo kwa manufaa zaidi ya kiuchumi kama kufungua akaunti na kupata ushauri mbalimbali wa kitaalam
Pia meneja wa Mikopo midogomidogo na ya kati Bi Akwilina Shirati  amewakaribisha sana wananchi mbalimbali kuja kupatiwa  huduma za  Mikopo yenye riba na masharti  nafuu 


*****************************************************************************
Imeandikwa na; Puyol B Mwasampeta 0757337870
Imehaririwa na ; Martin Emanuel 0769858521

0 comments :

Chapisha Maoni