Anaitwa Thobias Mwankonda,Alizaliwa katika kijiji cha Itope kata ya Itope wilayani Kyela mkoani Mbeya.
Elimu ya msingi aliipata katika shule ya Msingi Kandete na kuhitimu rasmi mwaka 2003,
Elimu ya upili chini (sekondari)aliipata katika shule ya sekondari Itope ambapo alihitimu kidato cha nne mwaka 2007.
Akabahatika kuendelea na Elimu ya upili juu aliyoipata katika shule ya sekondari Mbalizi na kuhitimu mnamo mwaka 2010.
Kwa juhudi na bidii kubwa katika masomo yake baadae akabahatika kuendelea na masomo ya Elimu ya juu mwaka 2010 na amehitimu chuo kikuu cha Dar-res salam akisomea shahada ya Sayansi ya Siasa na Jamii.(Political Science and Public Adminstration) mwaka 2013
Amewahi kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanataaluma wanaotokea Kyela(Kyela intellectuall's Community) ikiitwa JUMUIYA YA WANAFUNZI ELIMU YA JUU KUTOKA KYELA ambapo aliiongoza kwa mafanikio mengi na makubwa sana ikiwemo kuwaongoza wanataaluma wenzake kujitolea kufundisha katika shule mbalimbali za sekondari wilayani Kyela kama Katumbasongwe sekondari,Nkuyu sekondari na nyingine nyingi,Kuhamasisha wanafunzi na wadau wa Elimu kuchangia msaada wa Vitabu vya ziada na kiada ambapo vilikabidhiwa chini ya uongozi wake katika shule ya sekondari Katumbasongwe mnamo mwaka wa masomo 2012/2013.
Hiyo ni historia fupi ya Thobias Mwamkonda ambae ni mgombea udiwani kata ya Itope kupitia CCM.
MAMBO AMBAYO ATAYASIMAMIA KWA NAFASI YA UDIWANI IWAPO ATAPATA RIDHAA YA WANAITOPE KUWAONGOZA.
Pamoja na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi Bwana Mwankonda anasema atahakikisha anatumia vipawa na Elimu na uwezo wake wote kuhakikisha mambo yafuatayo yanawanufaisha wanaItope na Watanzania kwa ujumla
1.MAJI,Kutatua changamoto ya maji kwa kuhakikisha wanaItope wanapata angalau maji safi,
2.UMEME,Kuhakikisha anashughulikia kuufikisha umeme katika maeneo karibia yote ndani ya kata ya Itope ,
3.ELIMU,kuhakikisha wanafunzi wa Itope wanapata elimu Bora,
4.AFYA, kuhimiza watu kutumia bima ya afya kama CHIEF na kadhalika, kupatikana madawa katika vituo vya afya vilivyopo ndani ya kata hiyo,
5.KILIMO, kuhakikisha wakulima wanapata mbolea za ruzuku kwa wakati,
6.MIUNDOMBINU kuboresha madaraja madogo madogo, michezo kuzikuza na kuziendeleza timu zilizopo ndani ya kata ya Itope
7.MICHEZO NA UTAMADUNI,kuunda timu za kata za wanaume na wanawake na watoto chini ya miaka 15 ambazo atazisajili na kutambulika kiwilaya mpaka kitaifa.pia kudumisha na kuendeleza utamaduni kama vile ngoma za asili
8.JAMII,Kuhamasisha usawa kwa wote, .
Mwamkonda amesema kama wanaitope watamchagua atahakisha changamoto zote anazitatua kwa kushirikiana na wananchi ili kata ya Itope isonge mbele.
Bwana Mwankonda amesisitiza kuwa Maendeleo yoyote hayawezi kupatikana bila ya UMOJA,KUJITUMA kwa ajili ya faida ya jamii yote ya wanaItope
Jumanne, 29 Septemba 2015
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hongera Thobias ila mlango ulioingilia
JibuFutabig up kijana #thobias mwamnkonda.........wanaItope tuko pamoja nawe
JibuFuta