Viongozi waandamizi wa Asasi ya kiraia ya SWOLO wakiwa katika picha ya pamoja nje ya Ofisi .Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa asasi hiyo Mzee Abel Ambakisye
Mkurugenzi wa Asasi ya kiraia wilayani Kyela inayojihusisha na huduma na usaidizi kwa Watoto yatima,wajane na wazee wilayani Kyela ijulikanayo kama SWOLO Mzee Abel Ambakisye amewaasa wanasiasa nchini na wilayani Kyela kwa ujumla kutokutumia lugha chafu wakati wa kampeni zao zaidi wajenge na kutetea hoja zao.Ameyasema hayo ofisini kwake alipotembelewa na mwandishi wa mtandao wako wa Nyumbani KYELA Nyumbani Bwana Puyol Mwasampeta siku ya tarehe 7 septe,mba mwaka huu
Mzee Ambakisye pia amewataka vijana kupunguza ushabiki wa kisiasa wenye mihemko ya hali ya juu inaopelekea vijana kupigana kitu ambacho kinaweza kuleta machafuko na kuvuruga amani ya wilaya na nchi kwa ujumla hapa.Amesisitiza kila kitu kifanywe kwa kiasi kwani hata waingereza walisema"Too Much is harmful "
Amemaliza kwa kuwaomba viongozi na waumini wa dini wakiongozwa na wachungaji na mashehe kuiombea nchi yetu ifanye uchaguzi kwa amani na usalama na zaidi kuombea Uchaguzi wa Huru na Haki ili Haki ionekane imetendeka.
Imeandikwa na Puyol Mwasampeta
Imehaririwa na Martin Emanuel
Ijumaa, 11 Septemba 2015
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
0 comments :
Chapisha Maoni