Jumamosi, 5 Septemba 2015


Mkuu wa wilaya akiwa maeneo ya katikati ya mji wa Kyela kuhamasisha usafi wa mazingira wilayani Kyela
Mkuu wa wilaya ya Kyela Bi Thea Ntara amesema kuwa ni wajibu wa kila mtu kufanya usafi maeneo yake ya kazi au anapoishi ili kuondokana na magonjwa ya mlipuko.Mkuu huyo wa wilaya ameyasema hayo katika mahojiano maalum na mwandishi wa mtandao wako wa Nyumbani KYELA Nyumbani katika kuhamasisha usafi wa mazingira wilayani Kyela.
Hata hivyo Ntara amewataka wananchi kufanya usafi bila kusimamiwa ili kuondokana na adhabu zinazoweza kutolewa kwa watakaoshindwa kufanya usafi wa mazingira.

Wilaya ya Kyela kupitia mamlaka ya mji mdogo wa Kyela imejiwekea utaratibu wa kuhamasisha wananchi wake kuhusu usafi wa mazingira kila juma mosi ya kwanza ya mwezi. Katika kampeni hiyo ya kufanya usafi viongozi wa wilaya wanapita kuangalia zoezi hilo linavyotekelezwa ili kuhakikisha utekelezaji wake unatimizwa .
Maeneo aliyopitia mkuu wa wilaya kukagua ni Kalumbulu,Salama, Mikoroshini,Kyela Kati na maeneo mengine mengi. Utafiti uliofanywa na Mtandao wako wa Nyumbani umegundua kuwa mara baada ya mkuu wa wilaya kuamua kuacha ofisini kusubiria taarifa na kwenda moja kwa moja mitaani kuhamasisha na kuangalia zoezi hilo linavyotekelezwa mafanikio yameonekana kwa maeneo mengi kuwa na kiwango kinachotakiwa katika usafi wa mazingira.KYELA Nyumbani inampongeza sana mkuu wa wilaya kwa hatua aliyoichukua na kuwahamasisha viongozi wengine kuacha kukaa ofisini na kwenda mitaani kusimamia na kuhmasisha shughuli mbalimbali za maendeleo
Imeandikwa na ;PUYOL B MWASAMPETA
Imehaririwa na ;MARTIN EMANUEL

0 comments :

Chapisha Maoni