Jumapili, 6 Septemba 2015



Mgombea wa Ubunge jimbo la Kyela Bwana Abraham Mwanyamaki akiwasili katika viwanja vya Mchaga almaarufu Uwanja wa SUGU katika uzinduzi wa Kampeni za Ubunge wilayani Kyela kwa tiketi ya CHADEMA na UKAWA

Mheshimiwa Joseph Mbilinyi akiunguruma katika uzinduzi wa kampeni jimboni Kyela kwa CHADEMA









Mara baada ya kipyenga cha kampeni kupulizwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi kampeni zimeanza rasmi ambapo jana ilikuwa ni zamu ya UKAWA kuzindua kampeni zao za Udiwani.Wananchi wilayani Kyela wamekuwa wakijitokeza kusikiliza sera za wagombea mbalimbali wa nafasi za ubunge na udiwani. Mgombea ubunge wa jimbo la kyela kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na UKAWA Bwana Abraham Mwanyamaki amesema kuwa wanakyela wanajukumu moja tu la kumuunga mkono awaongoze katika kufanya mabadiliko ili wilaya isonge mbele kimaendeleo.
Mwanyamaki amesema kuwa endapo atapewa ridhaa ya kuwa mbunge atahakikisha wilaya ya Kyela inapiga hatua kubwa katika nyanja mbalimbali ikiwemo ELIMU,KILIMO ,UVUVI ,MIUNDOMBINU na BIASHARA kwa ujumla.Pia amegusia suala la kufungiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kwa radio ya jamii wilayani Kyela radio KYELA FM kuwa atahakikisha inafunguliwa ili iendelee kuwahudumia wanajamii wa kyela na maeneo jirani kwa kutambua umuhimu na haki ya mwananchi kupata habari.
Kwa upande wake mgombea ubunge jimbo la mbeya mjini Joseph Mbilinyi (Sugu) amesema kuwa kyela ina rasilimali nyingi lakini imekosa msimamizi wa kutafuta wahisani wa kununua amesema endapo wanakyela wataipatia chadema kura za kuongoza jimbo hilo basi Kyela itazaliwa upya. Pia mwanahabari nguli nchini aliyekuwepo katika uzinduzi wa kampeni hizo Bwana Saed Kubenea ambaye pia ni mgombea wa jimbo la Ubungo kupitia CHADEMA aliyegusa zaidi upande wa ufisadi wa CCM huku akitumia nyaraka mbalimbali aliwaomba wananchi wa Kyela kumchagua Bwana Mwanyamaki ili aweze kupeperusha na kuifanyia kazi Ilani ya CHADEMA kwa mabadiliko ya Kyela..........
LEO CHADEMA WANAENDELEA NA KAMPENI ZAO HUKO NGONGAAAAAAA
eNDELEA KUTUFUATILIAAAAAAAA.....MTANDAO WAKO WA NYUMBANI

0 comments :

Chapisha Maoni