Mkuu wa wilaya ya Rungwe Bi Zainab Mbuussi akiwavalisha vijana fulana zenye nembo ya FEMA |
Mkuu wa wilaya akiwa na baadhi ya watoto katika picha ya pamoja |
Mkuu wa wilaya ya Rungwe akiwa meza kuu akifuatilia kwa makini matukio mbalimbali siku ya Tamasha la kuombea Amani |
Wachezaji wa ngoma ya asili ya kinyakyusa maarufu LING'OMA wakitumbuiza siku ya Tamasha |
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Tukuyu wakifikisha ujumbe kwa hadhira iliyohudhuria Tamasha hilo kwa njia ya sanaa ya Maigizo. |
Vijana wakionyesha vipaji vyao kwa njia ya Sarakasi |
Shirika la Karibu Tanzania likishirikiana na UNDP ana Fema waliandaa tamasha la kuombea amani kwa Taifa letu la Tanzania kuelekea Uchaguzi mkuu wa Rais ,Wabunge na Madiwani
Tamasha hilo lilifanyika tarehe 11.10.2015 siku ya jumapili katika chuo cha maendeleo ya wananchi Katumba kilichopo nje kidogo ya mji wa Rungwe ambapo mgeni rasmi wa tamasha hilio la kuhamasisha amani alikuwa mkuu wa wilaya ya Rungwe bi Zainabu Mbussi. Amewataka vijana kutotumika na wanasiasa kuvunja amani kwani bila amani hakuna maendeleo yatakayofanyika.
Ameyasema hayo kwenye tamasha liloandaliwa na shirika hilo na kufadhiliwa na UNDP amesema kuwa lengo la tamasha hilo ni kuhamasisha amani ya Tanzania.
Kwa upande wake mgeni rasmi huyo amewashukuru waandaaji wa tamasha hilo kwa kuichagua wilaya yake kufanyia tamasha hilo.
Katika tamasha hilo kulikuwa na burudani mbali mbali kama vile maigizo, mziki na vingine vingi vya burudani katika vikundi hivyo vilionekana kumvutia mkuu wa wilaya na kumuagiza mkuu wa chuo hicho kumtafuta mwalimu wa sanaa ili kuzalisha wasanii na waigizaji watakaoitangaza wilaya ya Rungwe.
Mwandishi ;Aidan Mwasampeta 0757337870
Mhariri; Martin Emanuel 0769858521

0 comments :
Chapisha Maoni