Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la MIICO Bwana ADAM SIWINGWA akiwaelekeza jambo baadhi ya wakulima waliohudhuria semina hiyo wilayanio Kyela juzi |
Bi Catherine Mlaga akiwezesha semina kwa wanakijiji waliohudhuria semina iliyoandaliwa na shirika la MIICO |
Mkuu wa wilaya akiwa na Kaimu afisa kilimo wa wilaya ya Kyela Bwana Paulo Sheyo wakati wa Semina hiyo |
Mkuu wa wilaya Kyela akiwakabidhi baiskeli zilizotolewa na shirika la MIICO kwa wakulima waliohudhuria semina hiyo ya uwezeshaji wakulima wa kilimo cha mpunga wilayani Kyela |
Semina hiypo iliyojumuisha washiriki ambao ni Wakulima kutoka vijiji kumi na sita ambavyo ni Katumba,Mpunguti, Isanga,Tenende, Bwato, Isuba,Makwale, Mahenge, Ngeleka, Katela, Kanga,Kafundo, Mubunga, Kingili,Ngana na Mpunguti ya Makwale.
Mfanyakazi na mwezeshaji wa shirika la Miico lenye makao makuu jijini Mbeya nane nane Bi Catherine Mlaga amesema kuwa shirika hilo linafanya kazi na wakulima wa mikoa minne ambayo ni Morogoro,Iringa, Rukwa na Mbeya na wilaya sita zinanufaika na miradi yao.
Pamoja na kuwapatia wakulima mafunzo jinsi ya uzalishaji wa mpunga pia shirika la MIICO limetoa baiskeli kumi na sita (16) kwa vijiji vinavyonufaika na mradi huo.
Akikabidhi baiskeli hizo mkuu wa wilaya ya Kyela bi Thea Ntara amelishukuru shirika la MIICO kwa kuja wilayani Kyela na kuwafundisha wakulima wa zao la mpunga na kuwaomba MIICO kuendelea kufanya hivyo mara kwa mara wilayani Kyela.
Ameliomba shirika hilo kuwapeleka baadhi ya wakulima nje ya nchi ili wakajifunze na kubadilishana mawazo na wakulima wa mpunga wa nje ya Tanzania.
Mkuu wa wilaya pia amewaomba wakulima hasa wanaume kutowanyanyasa wake zao hasa kipindi cha mavuno ambapo amesema kuwa wanaume wengi wakivuna mpunga wanakuwa wakali kitu ambacho kinasababisha mpunga kuisha bila mwanamke kujua na kuleta mfalakano ndani ya nyumba.
Mkuuwa wilaya hakusita kuwaomba wananchi wa wilayani Kyela na Nchini kwa ujumla kushiriki kwa amani katika zoezi lijalo la Uchaguzio mkuu Tanzania kwa kutimiza wajibu wao na kufuata na kutii sheria za uchaguzi...Amesisitiza sana wajibu wa wananchi katika kuilinda amani yao....
Mwandishi ;Aidan Mwasampeta 0757337870
Mhariri; Martin Emanuel 0769858521
0 comments :
Chapisha Maoni