Jumatatu, 1 Septemba 2014


Wanafunzi wakipakizwa kwenye lori kupelekwa Kittuo cha Polisi

Akari kituo cha polisi Kyelai wakijadili jambo

Wanafunzi wakiwa kwenye lori tayari kupelekwa kituoni

Wanafunzi wakiwa wamefikishwa nje ya Kituo cha polisi Kyela

Viongozi wa Serikali Kyela wakiongea na wanafunzi kituoni Polisi Kyela.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya aya Kyela ndugu Gabriel Mwakalinga(KIPIJA)akiongea na Mwandishi wetu

Mwanafunzi wa KEIFO Livingstone Msusi akiishukuru Serikali kwa kumrekebisha

Mwanafunzi Salome Mwaiposa akizungumzia tukio hilo kwa kuwaasa wazazi washirikiane na Serikali
KATIKA kuhakikisha elimu inapewa kipaumbele na kuongeza ufaulu kwa Wanafunzi Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya,Halmashauri hiyo imeanzisha mkakati maalumu wa kuwakamata watoto watoro. Hayo yalibainishwa juzi na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Gabriel Kipija, alipokuwa akizungumza na Mbeya yetu kuhusu mikakati ya kuongeza ufaulu kwa Wilaya hiyo. Kipija alisema hali ya utoro kwa wanafunzi ilikithiri sana kwa kutohudhuria masomo na kuzurura ovyo mitaani jambo lililopelekea Halmashauri hiyo kushika nafasi ya mwisho kimkoa katika matokeo ya hivi karibuni ya kidato cha Nne. Alisema katika Operesheni iliyofanyika wiki mbili zilizopita ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Magreth Malenga, yeye mwenyewe na Mkurugenzi wa Halmashauri walifanikiwa kuwakamata wanafunzi 500 wa shule za Sekondari ndani ya siku moja. Alisema katika siku hiyo Wanafunzi wa shule mbali mbali za Sekondari Kyela Mjini walikamatwa kwa uzururaji wengi wao wakiwa kwenye sare za shule lakini hawakuhudhuria masomo na kuwafikisha kituo cha polisi kwa kosa la utovu wa nidhamu. Alisema kitendo cha kuwafikisha polisi wanafunzi hao kimeibua mwamko mkubwa wa wanafunzi kuhudhuria masomo darasani pamoja na kuwahi ambapo hivi sasa hakuna mwanafunzi anayeonekana barabarani kuanzia saa moja asubuhi tofauti na awali. Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Keifo iliyopo Wilayani Kyela ambao walikumbwa na mkasa huo, mbali na kukiri kufanya vitendo hivyo tofauti na matarajio ya wazazi pia walipongeza kitendo cha Halmashauri cha kuwakamata na kuwapeleka Polisi. Livingstone Msusi(15) mwanafunzi wa kidato cha Kwanza Keifo Sekondari alisema yeye binafsi alikumbwa na kamata kamata hiyo lakini hivi sasa amejirekebisha na kuwa wa kwanza kuwahi shule tofauti na awali ambapo alikuwa hafiki kabisa. Salome Mwaiposa(14) alisema tangu operesheni hiyo ifanyike amekuwa na maendeleo mazuri darasani kutokana na kuhudhuria vipindi vyote na kwa wakati unaostahili. Aidha baadhi ya wanafunzi waliwatupia lawama wazazi kwa kutofuatilia maendeleo ya watoto wao mashuleni ikiwa ni pamoja na kuwahimiza kwenda shule jambo lililochangia kuongezeka kwa utoro na kujiingiza katika shughuli hatarishi mitaani. Walisema ili kukomesha kabisa utoro wa wanafunzi mashuleni ni bora wazazi wakatoa ushirikiaono kwa Serikali kwa kutoa taarifa endapo wanakuwa na watoto ambao husumbua kusoma na kuwaletea kesi wazazi kutokana na kujiingiza katika magenge ya uhalifu. CREDIT;MBEYA YETU

Jumapili, 31 Agosti 2014


Mwili wa kichanga huyo ukiwa umetupwa mferejini.

Mwili wa kichanga ukiwa katika gari la polisi

Watu mbalimbali wakishuhudia tukio hilo la kinyama na kikatili

Gari la polisi likiwasili eneo la tukio kwa ajili ya kuuchukua mwili wa kiichanga huyo
Katika hali inayoonesha ni jinsi gani Dunia imefikia mwisho jioni ya tarehe 30 agosti 2014 kumetokea tukio lililowashtua watu wengi kwani ni UKATILI wa hali ya juu. Katika eneo la Kyela mjini maeneo ya uwanja wa wazi maarufu kama uwanja wa Roma kuna mfereji mkubwa uliojengwa kwa msaada wa TASAF kumekutwa kichanga kimetupwa kikiwa kimeviringishwa kwenye mfuko wa plastiki na salfeti. Inasemekana kichanga huyo ametupwa na mtu aliyekuwa na bodaboda na kisha akakimbia na asijulikane ni nani na ametokea wapi.Baada ya kuona hivyo ndipo taarifa zikafika Kituo cha polisi Kyela na askari kuja kuuchukua mwili wa kichanga huyo kwa taratibu za kitaalamu zaidi.
KYELA Nyumbani inalaani vikali kitendo hiki kisichovumilika katika jamii na kuwaomba wananchi wenye taarifa kuhusu tukio hili kuzifikisha kituoni Polisi mapema zaidi ili wahusika waweze kupelekwa mbele ya vyombo vya sheria na Haki iweze kutendeka

Ijumaa, 29 Agosti 2014


Mkuu wa wilaya bi Magreth Malenga akiongea na wananchi waliohudhuria katika sherehe za makabidhiano hayo

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Kyela ndugu Clemence Kasongo akitoa salamu

Mganga mkuu mkoa wa mbeya Dk Seif Mhina akitoa shukrani zake kwa kampuni ya Bioland
meneja wa Bioland tawi la Kyeal ndugu Erasto Kilongo akisoma Risala kwa Mkuu wa wilaya na meza kuu kwa ujumla
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Kyela ndugu Gabriel Mwakalinga(KIPIJA)akitoa shukrani kwa kampuni ya Bioland Tanzania

KAMPUNI ya Biolands International Ltd imetoa msaada wa gari ya kubebea wagonjwa (Ambulance) aina ya Nissan Patrol kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela lenye thamani ya shilingi zaidi ya Milion 76. Hafla ya makabidhiano ya gari hilo imefanyika katika viwanja vya Halmashauri hiyo baina ya Mkuu wa Wilaya ya Kyela Magreth Esther Malenga, Meneja wa Bioland Felix Mtawa na Mwenyekiti wa uhamasishaji wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya Afya, Dk.Charles Mbwaji wakishuhudiwa na mganga mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dk. Seif Mhina. Katika Risala ya Bioland iliyosomwa na Meneja wa Tawi, Erasto Kilongo, alisema lengo la msaada huo ni kutambua mchango wa wananchi katika maeneo wanayofanya kazi. Alisema Bioland ni Kampuni Binafsi inayojishughulisha na ununuzi wa Kakao katika Wilaya za Kyela na Rungwe ambapo inafanya kazi na na wakulima zaidi ya 20,000 katika vituo 137 vilivyopo katika wilaya hizo mbili. Alisema Kampuni hiyo inafanya kazi moja kwa moja na wakulima katika kufanikisha shughuli za vyeti mbalimbali ambavyo vinasaidia kuwepo kwa uhakika wa soko la kakao, vyeti kama vile kilimo hai (organic farming), Kilimo endelevu (Rain forest Allience),na Usawa wa kibiashara katika jamii (social and Fare Trade). Alisema katika sekta ya Afya na usalama wa wazalishaji, Kampuni imenuia kuhakikisha afya za wakulima na familia zao zinaendelea kuimarika wakati wote na kupata huduma za afya kwa gharama nafuu kupitia mradi wa Bima ya afya ya jamii. Alisema katika kufanikisha mradi huo, Kampuni ilikubali kutenga kiasi cha dolla 60,000 za kimarekani kwa kipindi cha miaka 5 toka 2010 hadi 2014 kwa ajili ya kutoa ruzuku kwa wakulima wanaojiunga na bima ya afya ya jamii. Aliongeza kuwa Kutokana na umuhimu huu wa kuhakikasha afya za wakulima na familia zao zinaimarika pia Biolands imefadhili ununuzi wa gari la wagonjwa (Ambulance) lenye thamani Shilingi Milioni 76,140,000/=, ambalo limekabidhiwa kwa Halmashauri kwa niaba ya CHIF, HIMSO, CIDR na wananchi wa Kyela. Awali akitoa salamu kwa niaba ya HIMSO, Dk. Charles Mwanji, alisema kazi ya HIMSO ambalo ni shirika lisilokuwa la kiserikali ni kuhakikisha wananchi wanajiunga na mfuko wa jamii na kupata huduma ipasavyo. Alisema moja ya majukumu yao ilikuwa ni kuwahamasisha Bioland kununua gari la wagonjwa kutokana na umuhimu kwa Wananchi wa Kyela ili waweze kupata huduma za mfuko wa bima kiufasaha. Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dk. Seif Mhina, alisema Kazi ya Bioland na HIMSO ilikuwa ni kutoa gari hivyo Halmashauri ihakikishe gari linatumika katika shughuli iliyokusudiwa. Alisema ili hayo yakamilike ni bora gari hilo likawa linashindwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Kyela ili kuepuka matumizi tofauti ya gari kama ilivyowahi kutokea kwa magari mengine. Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kyela ikishukuru kwa niaba ya Wananchi wa Wilaya ya Kyela, alisema Kampuni hiyo imemaliza kilio cha Wananchi wa Kyela cha kutaka gari la wagonjwa kilichokuwepo muda mrefu. Alisema kupitia hamasa walioonesha Bioland Wilaya yake itaanza kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya afya ili kuhakikisha kila mwananchi anatumia kadi kwenye matibabu. Aidha alitoa wito kwa watumishi wa vituo vya Afya na Mahospitali kutoa kipaumbele kwa wagonjwa wenye kadi kuliko wenye fedha mkononi ili wapate tiba kama serikali ilivyoagiza. CREDIT;Mbeya Yetu