Mwili wa kichanga huyo ukiwa umetupwa mferejini.
Mwili wa kichanga ukiwa katika gari la polisi
Watu mbalimbali wakishuhudia tukio hilo la kinyama na kikatili
Gari la polisi likiwasili eneo la tukio kwa ajili ya kuuchukua mwili wa kiichanga huyo
Katika hali inayoonesha ni jinsi gani Dunia imefikia mwisho jioni ya tarehe 30 agosti 2014 kumetokea tukio lililowashtua watu wengi kwani ni UKATILI wa hali ya juu.
Katika eneo la Kyela mjini maeneo ya uwanja wa wazi maarufu kama uwanja wa Roma kuna mfereji mkubwa uliojengwa kwa msaada wa TASAF kumekutwa kichanga kimetupwa kikiwa kimeviringishwa kwenye mfuko wa plastiki na salfeti.
Inasemekana kichanga huyo ametupwa na mtu aliyekuwa na bodaboda na kisha akakimbia na asijulikane ni nani na ametokea wapi.Baada ya kuona hivyo ndipo taarifa zikafika Kituo cha polisi Kyela na askari kuja kuuchukua mwili wa kichanga huyo kwa taratibu za kitaalamu zaidi.
KYELA Nyumbani inalaani vikali kitendo hiki kisichovumilika katika jamii na kuwaomba wananchi wenye taarifa kuhusu tukio hili kuzifikisha kituoni Polisi mapema zaidi ili wahusika waweze kupelekwa mbele ya vyombo vya sheria na Haki iweze kutendeka
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
0 comments :
Chapisha Maoni