Jumatano, 3 Juni 2015

Mwenyekiti wa Chama cha soka wilayani Kyela James Mwakilema
Chama cha mpira wa miguu wilayani Kyela (KDFA) kimevitaka vilabu vya soka wilayani kuvuta subira kuhusiana na ratiba ya ligi ya PAMBANA SAIDIA JAMII ilizinduliwa hivi karibuni ambayo bado haijatoka.Ratiba hiyo hapo awali iliahidiwa na KDFA kuwa ingetoka jana tarehe moja mwezi wa sita (juni 01) na ligi kuanza tarehe tatu mwezi wa sita (juni 03).Vilabu vimeingiwa na hofu kutokana na ligi nyingi kuzinduliwa na kuishia hapo hapo ikiwemo ligi ya LIHUNDI CUP na KYUSA CUP ambazo zilizinduliwa bila kuendelea.Mpaka sasa ratiba haijatoka.
Akizungumza na mtandao wako wa Nyumbani ,KYELA Nyumbani mwenyekiti wa KDFA Bwana James Mwakilema amesema ratiba ya ligi hiyo itatoka tarehe (juni 04) na ligi itaanza tarehe tano mwezi wa sita (juni 05) katika viwanja vya ambavyo vimegawanywa kutokana na tarafa ambapo tarafa ya Unyakyusa ni Shule ya Msingi Katumbasongwe, Shule ya sekondari Mwigo,Shule ya Msingi Kapwili, Shule ya Msingi Mpanda. Tarafa ya Ntebela vituo vilivyoanishwa na Mwenyekiti huyo ni pamoja na Shule ya Msingi Tenende, Shule ya Sekondari Ipinda , Shule ya Msingi Mpunguti, Shule ya Msingi Mababu.

Jumanne, 2 Juni 2015

Kikosi cha MPUNGUTI SPORTS ACADEMY wakiomba dua kabla ya kuumana na KILASILO SPORTS ACADEMY
Mkurugenzi wa MPUNGTI SPORTS ACADEMY PUYOL MWASAMPETA katika harakati za kutafuta vifaa vya wachezaji kwa wadau mbalimbali mjini Kyela
Kikosi cha MPUNGUTI SPORTS ACADEMY kimetoKa sare ya kufungana magoli 2-2 ugenini dhidi ya KILASILO SPORTS ACADEMY siku ya may 30 2015 jumapili iliyopita, KILASILO SPORTS ACADEMY ndio walikuwa wa kwanza kuandika goli kupitia kwa Ally Kipupa mnamo dakika ya 11 .MPUNGUTI SPORTS ACADEMY walisawazisha kupitia kwa Edom Jevu dakika 23'. Mpaka timu zinakwenda mapumziko zilikuwa zimefungana goli 1-1.
Kipindi cha pili dakika ya 57 KILASILO SPORTS ACADEMY waliandika goli la pili lililofungwa na Samweli Hans kwa njia ya penati baada ya mabeki kufanya madhambi ndani ya eneo la hatari la golikipa (eneo la 18),huku mashabiki wengi wakiamini kuwa KILASILO SPORTS ACADEMY ndio washindi wa mchezo huo kunako dakika ya 88 nahodha wa MPUNGUTI SPORTS ACADEMY Asukile Edwin kijana mwenye umri wa miaka 11 aliunganisha krosi iliopigwa na Albert Mwanyela na kuiandikia MPUNGTI SPORTS ACADEMY goli la 2 na kuifanya itoke uwanjana kwa kutoshana nguvu na KILASILO SPORTS ACADEMY Jumatano ya tarehe 03.06.2015 kikosi cha MPUNGUTI SPORTS ACADEMY kitacheza mchezo wa kirafiki na ITENYA.Mchezo huo ni maalumu kwa ajili ya kupokea jezi kutoka kwa mdau wa soka Chans Kayila ambae amevutiwa sana na kikosi hicho, Mkurugenzi wa timu hiyo Puyol Mwasampeta ambae ni mtangazaji wa radio ya jamii wilayani Kyela KYELA FM COMMUNITY RADIO alimuomba mdau huyo msaada huo ambae mpaka dakika hii jezi kanunua zipo ndani anasubiri juma tano kwenda kuwakabidhi vijana hao

Jumatatu, 1 Juni 2015

Mkuu wa wilaya Kyela bi Thea Ntara akisalimiana na wachezaji kabla ya mpira kuanza
Mwenyekiti wa Asasi ya Pambana Saidia Jamii Bwana Abraham Mwanyamaki akiongea na mwanahabari wetu baada ya ufunguzi wa ligi hiyo
Mkuu wa Wilaya Kyela Bi Thea Ntara akiongea na mwanahabari wetu
Meza kuu wakifuatilia mchezo kati ya Kapasyula Fc na Bondeni Fc
Wachezaji wa Kapasyula Fc na baadhi ya mashabiki wao wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka meza kuu
Wachezaji wa Bondeni Fc na baadhi ya mashabiki wakisikiliza kwa makini kutoka meza kuu
Ligi ya Pambana Saidia Jamii msimu wa mwaka 2015 Wilayani Kyela itakayoshirikisha timu za mpira wa miguu zipatazo 50 imefunguliwa leo na Mkuu Wilaya Mhe. Thea Ntara.
Akizungumza na mtandao wako wa nyumbani KYELA Nyumbani Mwenyekiti Mtendaji wa Asasi ya Pambana Saidia Jamii (SCSA) Bwana Abraham Mwanyamaki amesema "nimeshiriki ufunguzi wa Ligi hii ambayo kwenye fainali zawadi kwa timu mshindi wa kwanza itajinyakulia shilingi milioni Moja, mshindi wa pili laki saba, mshindi wa 3 laki tano na mshindi wa 4 laki mbili. Aidha, kutakuwa na zawadi nyingine kama mipira ,jezi n.k.
Ameendelea kueleza kuwa ligi hii ni endelevu na ni kubwa sana wilayani Kyela kwani inashirikisha timu kutoka wilaya nzima ya Kyela.
Bwana Mwanyamaki aliongeza kwa kuwashukuru wachezaji,wadau wa michezo ,wanahabari na wananchi wa Kyela kwa ujumla kwa kutambua umuhimu wa michezo kwa afya na faida nyingine nyingi sana.
Mkuu wa Wilaya Kyela pia akiongea na mwandishi wa KYELA Nyumbani mara baada ya kufungua rasmi ligi hiyo amesema ni muhimu kwa vijana kushiriki katika michezo maana michezo ni ajira.Pia ameishukuru asasi ya Pambana Saidia Jamii kwa kuianzisha na kuiendeleza ligi hiyo kwa maendeleo ya Michezo Kyela
Katika ufunguzi wa ligi hiyo ambapo timu ya National ya Makwale kutoka Ntebela na timu ya Bondeni ya Kyela mjini ambao ndio mabingwa watetezi kutoka Unyakyusa zilimenyana vikali kwenye uwanja wa Mwakangale Kyela mjini. Timu ya Bondeni ilishinda kwa goli 3 kwa 1.