Jumatatu, 1 Juni 2015

Mkuu wa wilaya Kyela bi Thea Ntara akisalimiana na wachezaji kabla ya mpira kuanza
Mwenyekiti wa Asasi ya Pambana Saidia Jamii Bwana Abraham Mwanyamaki akiongea na mwanahabari wetu baada ya ufunguzi wa ligi hiyo
Mkuu wa Wilaya Kyela Bi Thea Ntara akiongea na mwanahabari wetu
Meza kuu wakifuatilia mchezo kati ya Kapasyula Fc na Bondeni Fc
Wachezaji wa Kapasyula Fc na baadhi ya mashabiki wao wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka meza kuu
Wachezaji wa Bondeni Fc na baadhi ya mashabiki wakisikiliza kwa makini kutoka meza kuu
Ligi ya Pambana Saidia Jamii msimu wa mwaka 2015 Wilayani Kyela itakayoshirikisha timu za mpira wa miguu zipatazo 50 imefunguliwa leo na Mkuu Wilaya Mhe. Thea Ntara.
Akizungumza na mtandao wako wa nyumbani KYELA Nyumbani Mwenyekiti Mtendaji wa Asasi ya Pambana Saidia Jamii (SCSA) Bwana Abraham Mwanyamaki amesema "nimeshiriki ufunguzi wa Ligi hii ambayo kwenye fainali zawadi kwa timu mshindi wa kwanza itajinyakulia shilingi milioni Moja, mshindi wa pili laki saba, mshindi wa 3 laki tano na mshindi wa 4 laki mbili. Aidha, kutakuwa na zawadi nyingine kama mipira ,jezi n.k.
Ameendelea kueleza kuwa ligi hii ni endelevu na ni kubwa sana wilayani Kyela kwani inashirikisha timu kutoka wilaya nzima ya Kyela.
Bwana Mwanyamaki aliongeza kwa kuwashukuru wachezaji,wadau wa michezo ,wanahabari na wananchi wa Kyela kwa ujumla kwa kutambua umuhimu wa michezo kwa afya na faida nyingine nyingi sana.
Mkuu wa Wilaya Kyela pia akiongea na mwandishi wa KYELA Nyumbani mara baada ya kufungua rasmi ligi hiyo amesema ni muhimu kwa vijana kushiriki katika michezo maana michezo ni ajira.Pia ameishukuru asasi ya Pambana Saidia Jamii kwa kuianzisha na kuiendeleza ligi hiyo kwa maendeleo ya Michezo Kyela
Katika ufunguzi wa ligi hiyo ambapo timu ya National ya Makwale kutoka Ntebela na timu ya Bondeni ya Kyela mjini ambao ndio mabingwa watetezi kutoka Unyakyusa zilimenyana vikali kwenye uwanja wa Mwakangale Kyela mjini. Timu ya Bondeni ilishinda kwa goli 3 kwa 1.

0 comments :

Chapisha Maoni