Alhamisi, 11 Juni 2015

Mkuu wa wilaya,Mganga mkuu wa wilaya na mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima Wakiwa nyumbani kwa mgonjwa mzee Aloisi
Mradi wa maji ulioonekana maji yake hayafai kwa matumizi ya binadamu

Mkuu wa wilaya Kyela Bi Thea Ntara leo jana ametembelea kijiji cha Ngonga kwa mambo mbalimbali ya kijamii.Mkuu wa wilaya amegusa mambo mbalimbali ambayo ni kama ifuatvyo
Amemtembelea mzee anayesumbuliwa na ugonjwa kwa muda mrefu na akitakiwa kufanyiwa upasaji mkubwa.Katika ziara hiyo iliyotokana na juhudi za aliyekuwa mwandishi na mtangazaji wa Radio ya Jamii KYELA FM na sasa ni mwandishi wa CHAI FM aliongozana na Mganga mkuu wa H Wilaya Daktari Festo.Katika kumtemebelea mzee Alosi Daktari amependekeza apatiwe Rufaa ya kwenda Hospitali ya rufaa Mbeya kwani ugonjwa umekuwa wa muda mrefu kanakwamba unahitaji upasuaji mkubwa. Ametembelea makazi na mashamba ya kokoa ya wananchi na kutoa ushauri mbalimbali.Amewashauri wananchi kujenga nyumba za kudumu na kuachana na nyumba za mianzi na kuezekwa kwa nyasi.Pia ameashauri wakulima wa kokoa kupogolea miti ya kokoa ili izae matunda mengi zaidi.
Pia mkuu wa wilaya ametolea maelezo mradi wa maji uliojengwa na WACHINA kijijini hapo na hadi sasa haujaanza kufanya kazi na serikali ya kijiji haijakabidhiwa funguo.Amesema"Mradi huo umefungwa na wachina kwa sababu maji yanayopatikana hapo yameonekana hayafai kwa matumizi ya binadamu na wameahidi kurudi tena na kuchimba chanzo kingine"
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

0 comments :

Chapisha Maoni