Jumatatu, 8 Juni 2015

Ezekiel gwatengile akiwa tayari kwa kukabidhi vifaa vya michezo Busokelo
Ezekiel Gwatengile akikabidhi vifaa vya michezo
Akiongea na timu zilizopokea vifaa vya michezo
mwenyekiti wa kijiji cha Isange Lutengano Mwakyoma akimshukuru Gwatengile
Mdau wa michezo na maendeleo kwa ujumla wilayani Rungwe katika Halmashauri mpya ya Busokelo Bwana EZEKIEL GWATENGILE ameendelea kuchangia katika maendeleo ya michezo na jamii nzima kwa kukabidhi vifaa mbalimbali vya michezo
Akikabidhi vifaa hivyo Ezekiel Gwatengile amesema kuwa ligi hiyo itashirikisha timu kumi ambazo ni Sinkime,Matamba,Super market,Nkalisi, Isange, Ipyelugo,Wateule, Isabula na Mpunga city. katika timu kumi ni timu mbili tu ambazo hazijapata vifaa na ameahidi kuwapatia hivi karibuni wakati ligi ikiendelea kufanyika. Gwatengile amemaliza kwa kuwaomba vijana kujituma zaidi kwenye michezo ili kujiepusha na mambo yasiyofaa. Pia amewaomba kutofanya vurugu kwenye ligi hiyo huku akiwataka kama kuna wapiganaji ngumi basi wamwambie ili aweke mashindano ya ndondi kuliko kuleta vurugu kwenye mashindano ya mpira wa miguu. Mwenyekiti wa kijiji cha Isange Lutengano Mwakyoma amemshukuru Gwatengile kwa kuweka mashindano ya mpira wa miguu na amesema kuwa ni mara ya kwanza kujitokeza mdhamini wa ligi ambaye anatoa vifaa vya michezo kabla ya ligi. Mwenyekiti huyo amemaliza kwa kusema kuwa ligi hiyo itawaondolea vijana kushinda vijiweni na kuzurula mitaani. Zawadi kwa washindi GWATENGILE CUP ISANGE ni Mshindi wa kwanza kujipatia KOMBE NA JEZI SETI MOJA,mshindi wa pili JEZI SETI MOJA na mshindi wa tatu atajipatia MPIRA MMOJA
*********************************************************
Wakati huo huo Ezekiel Gwatengile amekabidhi vifaa vya michezo kwa timu ya Bwima iliyoshika nafasi ya pili katika mashindano ya GWATENGILE CUP.Akikabidhi vifaa hivyo amewataka viongozi wa timu hiyo kuwapa mashabiki semina ili wasipigane na mashabiki wenzao katika mechi za ligi na mechi za kirafiki.
Timu ya Bwima ilimuomba Gwatengile vifaa vya michezo zikiwemo jezi na mpira na vyote amewatekelezea na kuwataka vijana kutojihusisha na mambo yasiofaa katika jamii ukiwemo ulevi wa kupindukia na ngono zembe.
Akipokea vifaa hivyo katibu mkuu wa timu ya Bwima Michael Nzasule amemshukuru Ezekiel Gwatengile kwa kuendelea kukuza soka la Busokelo na ameahidi kuwa timu yao itafanya vizuri kwasababu walikuwa na mpira mmoja ambao walikuwa wanawekeana zamu na timu ya wanawake (Bwima Quens).
Pamoja na hayo EZEKIEL GWATENGILE amezindua bomba la maji katika shule ya msingi Ikama iliyopo kata ya Lwangwa Halmashauri ya Busokelo ambapo wananchi wa kijiji cha Kitali waliomuomba Gwatengile awasaidie kununua bomba la maji ambapo baada ya kununua bomba hilo na wananchi kulifunga walimuomba azindue kitu ambacho kimemfanya awafurahie wananchi kwa kutambua mchango wake. Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ikama Ernest Fransis amempogeza Gwatengile kwa msaada huo na kumuomba awasaidie ujenzi wa nyumba za walimu na jengo lenye vyumba viwili la darasa la awali na ofisi ya walimu.
Shule hiyo inakabiliwa na uhaba wa nyumba za walimu ambapo kulikuwa na nyumba mbili tu, moja imechoka na nyingine imeweka nyufa ambayo ni hatari na walimu wamepanga nje ya shule kutokana na uhaba nyumba za walimu.
Imeandaliwa na PUYOL B MWASAMPETA

0 comments :

Chapisha Maoni