Jengo lililokabidhiwa leo na CRDB Wilayani Kyela
Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Thea Ntala akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi madarasa pamoja na madawati katika Shule ya Msingi ya Talatala iliyopo wilayani Kyela
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi madarasa matatu kwa Shule ya msingi Talatala
Mkuu wa Shule ya Talatala, Boniface Jackson akitoa hotuba yake
Wanafunzi wa shle ya msingi Talatala wakitumbuiza katika hafla za kukabidhiwa jengo la vyumba vya madarasa
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Kyela, Lugano Mwambaja (kushoto) akiwa na Meneja wa Benki hiyo tawi la Mbalali, Chibby Chibby (kulia)
Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Thea Ntala akipongezwa na Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Mkoa wa Mbeya, Benson Mwakyusa baada ya kutoa hotuba yake
Wazazi na Wazee wakifuatilia hafla ya kukabidhi jengo la vyuma vitatu vya madarasa
Bank ya CRDB wilayani kyela imekabidhi vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya msingi Talatala wilayani Kyela juzi tarehe 03 June 2015.Pamoja na vyumba hivyo vilivyogharimu zaidi ya shilingi za kitanzania milioni 60 pia Benki hiyo imekabidhi jumla ya madawati 60.
Wakikabidhi vyumba hivyo meneja wa bank ya CRDB tawi la Kyela Lugano Mwambaja amesema kuwa benki hiyo inatenga asilimia moja(1%) ya mapato kila mwaka na kusaidia sekta ya Elimu, Mazingira na Afya katika jamii husika.
Pia Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB nchini bi Tully Mwambapa amesema uamuzi huo wa kusaidia kujenga vyumba hivyo vya madarasa umetokana na majengo ya Madarasa ya shule hiyo kuezuliwa na upepo wakati wa mvua
Akipokea vyumba hivyo mkuu wa wilaya ya Kyela bi Thea Ntara ameipongeza benki hiyo kwa msaada wao na kuwataka kuendelea kusaidia shule nyingine ambazo zina hali mbaya. Ntara pia amewaagiza walimu kuacha tabia ya kuwalazimisha wanafunzi kusoma masomo ya ziada (tuition) ambazo wanafundisha mda wa jioni.Aliendelea kwa kuwaasa wanafunzi kujituma katika katika masomo kwa kutumia vizuri miundombinu hiyo.
Mkuu wa Wilaya amemaliza kwa kuwataka walimu kuacha kabisa kuwalubuni wanafunzi na kufanya nao mapenzi kitu ambacho hakiwezi kusongesha eli. mu mbele.
Shule ya msingi Talatala ni miongoni mwa shule zinazofanya vizuri ambapo matokeo ya mwaka 2014 ilikuwemo katika shule kumi zilizofanya vizuri wilayani kyela yaani kumi bora.
Imeandaliwa na PUYOL B MWASAMPETA

0 comments :
Chapisha Maoni