Jumanne, 9 Juni 2015

Kibao cha shule ya Msingi kikionesha uelekeo wa shule ya msingi Mwakikome ilipo
Jengo mojawapo la shule ya Msingi Mwakikome
Katibu wa Chadema Kijiji cha Mpunguti bwana Elias Mwaijuni
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kijiji cha Mpunguti kata ya Katumbasongwe wilayani Kyela kimewataka wananchi wa kijiji hicho kuwa na subira juu ya kutimiza ahadi yao ya ujenzi wa kisima bora cha maji katika shule ya Msingi Mwakikome kijijini hapo.
Viongozi wa CHADEMA waliwahidi wananchi kuchimba kisima na kukijengea ukuta wa matofali na saruji katika shule ya msingi Mwakikome wakati wa kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika decemba 14 mwaka jana.
Chama hicho kilidai kuwa kitakamilisha ujenzi wa kisima hicho kabla ya kufungua shule mwezi januari mwaka huu lakini mpaka sasa kisima hicho hakijakamilika.
Akilitolea maelezo jambo hili mbele ya Mwandishi wa Mtandao wako wa nyumbani KYELA Nyumbani Katibu wa chama hicho tawi la mpunguti BwanaElias Mwaijuni amesema kuwa tayari wamenunua saruji na matofali kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kisima hicho na wao wanasubiri wakati wa kiangazi ili kisima hicho kiongezwe kuchimbwa ndipo wakijenge kwa ubora mkubwa.bwana Mwaijuni aliendelea kwa kuwahamasisha zaidi wananchi wa Mpunguti na Kyela kwa ujumla kushirikiana na viongozi wao ili kuyafikia maendeleo ya jamii yao kwa faida yao yote.Alimaliza kwa kusema CHADEMA wanaamini katika nguvu ya umma katika mabadiliko ya jamii.
Mtandao wako wa Nyumbani utaendelea kulifuatilia hili na litakapokamilika tutawaletea mrejesho watu wetu wa Nyumbani
Imeandaliwa na PUYOL B MWASAMPETA

0 comments :

Chapisha Maoni