Jumamosi, 30 Mei 2015

Kikosi cha Mpunguti Sports Academy wakiwa na kocha wao
Vijana wa Mpunguti wakiwa katika mazoezi katika hali ya changamoto ya Vifaa vya michezo
Vijana wakisiliza kwa makini mawaidha kutoka kwa Wadau wakiongozwa na Mkurugenzi Puyol Mwasampeta
Katika maendeleo ya soka duniani kote uwekezaji wa muda mrefu unahitajika sana hasa katika kutambua ,kutengeneza na kuendeleza vipaji. Katika kulifanyia kazi hilo Wadau wa Maendeleo ya Soka wilayani Kyela Kata ya Katumba songwe kijiji cha Mpunguti wakiongozwa na Puyol B Mwansampeta ambaye ni Mkurugenzi wa MPUNGUTI SPORTS ACADEMY iliyo chini ya kocha SAMOLA MWAKABONA wameamua kuliweka hilo katika matendo kwa maendeleo endelevu ya Soka la Kyela. Akizungumza jana jioni na mtandao wako wa nyumbani KYELA Nyumbani Mkurugenzi wa kituo hicho ndugu Puyol B Mwasampeta amesema MPUNGUTI SPORTS ACADEMY siku ya jumapili(kesho) wanatarajia kwenda kukipiga na KILASILO SPORTS ACADEMY huko Ikimba huku wakikabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo usafiri wa kuwafikisha huko. Mkurugenzi huyo amesema licha ya changamoto zinazoikabili timu hiyo ila anamshukuru sana kocha wa Timu hiyo Bwana Samola Mwakabona(Mwangake) kwa moyo wa kujitolea katika kuviendeleza vipaji vya watoto hao . Bwana Puyol aliendelea kwa kuwashukuru sana wadau wote walioweza kuichangia timu hiyo hasa Mipira kwani hadi sasa wana mipira mitatu ambayo bado ni changamoto.Changamoto nyingine ni jezi,viatu na Semina kwa Kocha na wachezaji ili kuzidi kuendeleza upande wa Nadharia ya Michezo. Bwana Puyol ametoa wito kwa Wadau walio ndani na nje ya Kyela kuisaidia timu hiyo kwani changamoto zinazowakabili ni kubwa sana katika maendeleo ya Kituo hicho.pia amewakaribisha wadau wa Michezo kuitembelea MPUNGUTI SPORTS ACADEMY na kujionea vipaji vinavyokuja. .Waweza wasiliana na Bwana Puyol kwa namba 0757 337870 au 0716501334 kwa msaada wa hali na mali. KYELA Nyumbani inampongeza sana Mkurugenzi na kocha wa kituo hicho pamoja na kutoa wito kwa wadau mbalimbali wa michezo kusaidia kituo hicho

0 comments :

Chapisha Maoni