Katika mbio za kumrithi Dr Jakaya Mrisho Kikwete zikiendelea ambapo leo Mheshimiwa Edward Lowasa anatangaza nia yake ya kuomba ridhaa ya Chama kugombea Urais jijini Arusha WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, (Kazi Maalum), Profesa Mark Mwandosya, anatarajia kuchukua fomu kuwania urais Juni tatu mwaka huu.
Mwandosya ambaye tayari ametangaza kuacha kuwania ubunge katika Jimbo la Rungwe Mashariki (BUSOKELO), anakusudia kutangaza nia yake ya kusaka safari ya kuelekea Ikulu kupitia Chama cha Mapinduzi, Juni Mosi, mwaka huu.
Akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari jana nje ya viwanja vya Bunge, Profesa Mwandosya alisema sababu zilizomsukuma kuwania urais, atazitaja Juni Mosi atakapotangaza nia mkoani Mbeya.
” Sababu za kutaka kuwania urais na nini nitawafanyia Watanzania, nikiingia madarakani nitaeleza siku ya kutangaza nia Juni Mosi,”alisema Profesa Mwandosya.
Waziri Mwandosya ni mmoja kati ya makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambao kwa muda mrefu wameonesha nia ya kutaka kumrithi Rais Jakaya Kikwete anayemaliza muda wake.
Ikumbukwe kuwa Waziri Mwandosya alipata kuwania kuteliwa na chama cha mapinduzi kugombea urais mwaka 2005 na aliingia kwenye kundi la tatu bora miongoni mwa wagombea 11 waliowania nafasi hiyo.Mnamo mwaka 2005 akiwa nyuma ya Dr.Salim Ahmed Salim na Dr.Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ni Rais anayemaliza mda wake mwaka huu
Pia Profesa Mwandosya amekuwa waziri katika uongozi wa awamu ya tatu na nne akiwa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi,Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Raisi Mazingira,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (Kazi Maalum),
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
0 comments :
Chapisha Maoni