Meneja wa NMB Kanda ya nyanda za Juu kusini akishikana mkono na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela GABRIEL KIPIJA
Meneja wa NMB Kanda ya nyanda za juu kusini LUCRESIA MAKIRIYE akikabidhi madawati serikali ya wilaya ya kyela akishikana mkono na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela CLEMENCE KASSONGO.
Katika uwajibikaji kwa jamii Kampuni ya kifedha ya National Microfinance Bank(NMB) imeendelea kuchangia katika kushirikiana na serikali kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya Elimu Wilayani Kyela.
Kutokana na uhaba wa Madawati katika shule za msingi mkoani Mbeya,Benki ya NMB Nyanda za Juu Kusini kupitia kwa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya nyanda za Juu kusini,LUCRESIA MAKIRIE amesema benki hiyo itaendelea kuunga mkono Juhudi zinazofanywa na serikali katika uboreshaji wa sekta ya elimu nchini.
MAKIRIE ametoa kauli hiyo wakati wa Hafla ya kukabidhi Madawati 60 katika shule ya msingi Lubele iliyopo Kasumulu boda mjini Kyela yenye thamani ya zaidi shilingi milioni tano,na kuongeza kuwa NMB Bank wataendelea kuchangia uimarishaji wa miundombinu katika shule za msingi na sekondari wilayani Kyela.
Alisema Benki hiyo itaendelea kuhakikisha sekta ya elimu inaimarika kwa kutoa misaada mbali mbali pale inapokuwa inahitajika na kuongeza kuwa msaada huo ni sehemu ya utaratibu wa benki hiyo kurudisha fadhila kwa wateja wake kupitia huduma za kijamii.
Wakipokea msaada huo kwa niaba ya Serikali wilayani Kyela ,Mkuu wa Wilaya Kyela Dkt THEA NTARA,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela ndugu CLEMENCE KASSONGO na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Mheshimiwa GABRIEL KIPIJA wameishukuru Benki ya NMB kwa kuendelea kuchangia katika maendeleo ya Elimu na jumla wilayani Kyela.
Kutokana na msaada huo, Utakuwa umepunguza pengo la upungufu wa madawati katika Shule za Wilaya ya Kyela ambayo hadi sasa inakabiliwa na upungufu wa madawati 1600 na kupelekea wanafunzi kusoma kwa shida baada ya kubanana darasani.
0 comments :
Chapisha Maoni