Jumanne, 11 Februari 2014

VIGOGO wa Wakala wa Majengo (TBA), Makumba Kimweri na Richard Maliyaga walioruhusu ujenzi wa jengo linalochungulia Ikulu wamehukumiwa kwenda jela miaka 9 kila mmoja au kulipa faini ya shilingi milioni 15 kila mmoja na Hakimu Sundi Fimbo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar!
Maofisa hao wa serikali kwa sasa wapo mahabusu kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo ndugu na jamaa wanaangaika kutafuta fedha za kuwalipia dhamana.
VIGOGOVigogo wa TBA, Makumba Kimweri (kulia) na Richard Maliyaga (kushoto) wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar! (Picha na Maktaba).

Jumapili, 2 Februari 2014


Wachezaji wa Young Africans wakiwa mazoezini nchini Uturuki
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Young Africans kesho siku ya jumapili itashuka dimbani kuivaa timu ya Mbeya City FC kutoka jijini Mbeya katika muendelezo wa michezo ya mzunguko wa pili, mechi itakaofanyika katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Young Africans ambayo kwa sasa inakamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa VPL ikiwa na pointi 32, pointi moja nyuma ya vinara wanaongoza timu ya Azam FC huku Mbeya City wakiwa nafasi ya tatu na pointi 31.
Kikosi cha Young Africans kimeendelea na mazoezi yake leo asubuhi mjini Bagamoyo kujiandaa na mchezo huo wa kesho ambao ni muhimu kwa vijana wa Jangwani kupata pointi 3 na kuweza kujiweka katika nafasi nzuri ya kurejea kileleni.
Kocha mkuu Hans Van der Pluijm amesema wameendelea kufanyia marekebisho kwa makosa yaliyojitokeza katika mchezo uliopita dhidi ya timu ya Coastal Union na kusema anaamini vijana wake watafanya vizuri katika mchezo wa kesho.
Kuna mapungufu yalijitokeza katika mchezo uliopita mjini Tanga dhidi ya Coastal, tulipata nafasi kadhaa za kufunga tukashindwa kuzitumia pia umakini haukuwa mzuri sana, tumeendelea kufanyia marekebisho mapungufu hayo ili tuweze kufanya vizuri.
Katika mchezo wa awali uliofanyika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya mwezi Septemba mwaka jana, timu hizi zilitoka sare ya mabao 1-1 huku bao la Young Africans likifungwa na Didier Kavumbagu.
Mwenyekiti wa mkutano huo Msumba Mdesa wa Mbeya mjini

 Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa kupitia UVCCM mkoa wa Mbeya, Rabson Mwaipula alisema kuwa Malecela ni kiongozi aliyestaafu hapaswi kuingilia masuala ya vijana na badala yake akae atulie na kula pensheni yake kwa amani.


Edward Kakwale toka Momba

David Mwakalinga, ambaye alijitambulisha kuwa ni Mwenyekiti wa UVCCM kata ya Maendel.eo Jijini Mbeya, alisema Makonda anapaswa kujua hisitoria za viongozi wa wa juu wa CCM badaya ya kuibuka kwenye vyombo vya habari na kuropoka.











WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikiwa katikati ya sherehe za maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwake, baadhi ya vijana ambao ni wanachama wa Umoja wa Vijana (UVCCM) mkoa wa Mbeya wameibuka  wakiwa na mabango kumshinikiza Waziri Mkuu mstaafu John Samwel Malecela kuacha kuingilia masuala ya vijana ndani ya Chama Cha Mapinduzi.

Vijana hao pia wamemtaka Katibu wa Uenezi wa UVCCM, Paulo Makonda kumwomba radhi Lowassa kwa maneno aliyoyatoa hivi karibuni kwenye vyombo vya habari kwa madai hawakumtuma afanye hivyo na kauli zake zinalenga kukigawa chama.

 Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa kupitia UVCCM mkoa wa Mbeya, Rabson Mwaipula alisema kuwa Malecela ni kiongozi aliyestaafu hapaswi kuingilia masuala ya vijana na badala yake akae atulie na kula pensheni yake kwa amani.

“Malecela kwa hili amekuwa kama mchezaji ambaye yupo uwanjani lakini hajui anacheza namba ngapi na hajui anacheza na nani, tunamshauri aache kucheza mchezo ambao haumfai na badala yake atulie atushauri vizuri, sisi vijana yale tunayo tenda” alisema Mwaipula.

Alisema kitendo cha Malecela kuanza kuingilia kati masuala ya vijana na kumshambulia Waziri Mkuu mwenzake mstaafu, Edward Lowassa kinaonyesha jinsi Malecela asivyotumia vizuri busara zake kukiunganisha chama na badala yake anakigawa.

Alisema Malecela kama anataka aache posho anazolipwa kama Waziri Mkuu Mstaafu arejee kwenye ulingo wa Siasa kwani anaonekana bado anautamani licha ya kuangushwa vibaya kwenye jimbo lake la Mtera mwaka 2010.

Mwanachama mwingine wa UVCCM, Kisumba Mdesa ambaye alikuwa mwenyekiti wa mkutano wa vijana hao na wandishi wa habari jana jijini Mbeya alisema Makonda haijui vizuri CCM na historia ya viongozi wa CCM katika mchango wao wa kukijenga chama, hivyo kitendo chake cha kumshambulia Lowassa kwenye vyombo vya Habari ni utovu wa nidhamu.

Alisema kuwa Makonda hana sifa ya kuizungumzia UVCCM kwa kuwa yeye alichaguliwa kuongoza Chipukizi, lakini yeye amejingiza na kujifanya kuwa ni msemaji wa UVCCM.

Naye David Mwakalinga, ambaye alijitambulisha kuwa ni Mwenyekiti wa UVCCM kata ya Maendel.eo Jijini Mbeya, alisema Makonda anapaswa kujua hisitoria za viongozi wa wa juu wa CCM badaya ya kuibuka kwenye vyombo vya habari na kuropoka.

Alisema kiongozi kama Lowassa, amefanya mambo makubwa hapa nchini hasa kwa kusimamia maamuzi magumu, pamoja na miradi ya maendeleo kama shule za kata.

Alisema enzi za uongozi wa Lowassa kama waziri Mkuu alisimamia kwa nguvu zote ujenzi wa shule za kata ambazo sasa zimeonesha matunda kwa vijana wa kitanzania kupata elimu katika mazingira safi na kwa gharama nafuu.

Kutokana na hali hiyo wote kwa pamoja waliwaomba radhi viongozi wa dini, kwani maneno yaliyotewa na wenzao hao ndani ya chama hicho si msimamo wa wanachama wote.

Na Mbeya yetu