Wakati maafa ya mafuriko yakiendelea wilayani humu japo kwa kasi ndogo kumetokea na hali ya kustaajabisha ambapo katika bwawa maarufu kama caterpillar(Katapila) lililopo katika eneo la Mpanda kata ya Kyela mkabala na shule ya msingi Mpanda.Hali hiyo imewastaajabisha wakazi wengi kanakwamba wengine wamehusisha tukio hilo na imani za kishirikina.
Mamba huyo inasemekana kuwa waalikuwa wawili ambao walikuwa wanawasumbua sana watu kwa muda mrefu sasa.Watu wakaripoti katika mamlaka husika na ndipo maafisa wa maliasili wa wilaya wakaanza zoezi la kuwasaka mamba hao na kufanikiwa kumuua mmoja tarehe 22.4.2014 saa 10 jioni mwingine akiendelea kusakwa.
Kwa sasa amehifadhiwa katika ofisi za UJENZI wilaya zilizopo karibu na Uwanja wa mpira wa Mwakangale.
IMANI ZA KISHIRIKINA HAZIJAKOSEKANA
Mwandishi wa mtandao huu wa KYELANyumbani akizungumza na shuhuda mmoja eneo la tukio amesema "huyu mamba(aliyeuawa) na anaesakwa walikuwa wa mtu (mmliki kishirikina) aliyekuwa amewahifadhi kwenye hilo bwawa na walikuwa wanasumbua watu alafu watu wakienda kuwashangaa ikiwa ni hali ya kustaajabu basi kila mtu atakaeenda kuwaona mamba hao anazalisha gunia moja la mpunga shambani kwa mwenye mamba hao".Kama watu waliowahi kuwashangaa mamba hao ni 200 basi huyo mwenye Mamba hao atavuna gunia 200 za mpunga.Hatari sana na mazao yameharibiwa na mafuriko tusubiri watakao tuhumiwa
Mamba huyo anatarajiwa kuwa kitoweo kwa watumiaji kuanzia kesho kwani inasemekana mkuu wa wilaya bi.Magreth Simalenga ameagiza asichinjwe na kuchunwa hadi atakapomuona hiyo kesho tarehe 23.04.2014.ambapo watu waliokuwa wakisubiri kitoweo wameghadhibika kwa kucheleweshewa kitoweo chao.
Tunaendelea kufuatilia zaidi

0 comments :
Chapisha Maoni