Jumapili, 25 Mei 2014

IMG_2090
Kama unakumbuka ule moto wa Mbeya City katika michuano ya ligi kuu soka Tanzania bara msimu uliopita basi ndio umehamia huko Sudani katika michuano ya 
Wawakilishi hao wa Tanzania wamehamishia kasi yao katika michuano mipya ya CECAFA Nile Basin Cup, ambapo wameanza vyema mashindano hayo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Academie Tchite ya Burundi.
Mabao ya Mbeya City yamefungwa na washambuliaji hatari Paul Nonga katika dakika ya 15, Mwegane Yeya dakika ya 27 na nyota mpya Them Felix katika dakika ya 37.
Mechi hiyo muhimu kwa Mbeya City fc iliyosuasua kuwasili Sudan kutokana na kucheleweshewa tiketi za ndege imepigwa katika uwanja wa Khartoum-Sudan.
Kikosi cha Mbeya City kilichoanza leo ni Barhan David, Kabanda John, Kibopile Hamad, Julius Deogratius, Yohana Morris, Antony Matogolo, Deus Kaseke, Mazanda Steven, Paul Nonga, Mwegane Yeya na Them Felix `Mnyama`.
 Mbali na mchezo wa Mbeya City fc, majira ya saa 2:00 usiku  AFC Leopard ya Kenya itakabiliana na Enticelles ya Rwanda.

Jumatatu, 12 Mei 2014

MAHABUSU wawili kati ya sita wanaotuhumiwa kwa kesi za mauaji, wameleta kizaazaa baada ya kujaribu kutoroka na kukimbilia kwenye mlingoti wa Bendera ya Taifa na kuing’ang’ania kisha kuvua nguo na mmoja wao kubaki mtupu.
Tukio hilo limetokea may 8 2014 majira ya saa 4:00 asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza, wakati mahabusu hao walipofikishwa kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi zao, lakini ghafla walipofika kwenye viwanja vya mahakama hiyo walitimua mbiyo kuelekea kwenye mlingoti wa Bendera hiyo ya Taifa na kuvua nguo.
Inspector Henry akiwasihi mahabusu hao wawili wanaotuhumiwa kwa kesi za mauaji, kuachia mlingoti wa Bendera ya Taifa na kurudi kwenye chumba cha mahakama kwaajiri ya taratibu za kesi.
Inspector Henry akiwasihi mahabusu hao wawili wanaotuhumiwa kwa kesi za mauaji, kuachia mlingoti wa Bendera ya Taifa na kurudi kwenye chumba cha mahakama kwaajiri ya taratibu za kesi.
Askari polisi wakiwalinda mahabusu wawili kati ya sita wanaotuhumiwa kwa kesi za mauaji
Askari polisi wakiwalinda mahabusu wawili kati ya sita wanaotuhumiwa kwa kesi za mauaji
Inspector Henry (shati la bahari) akiwa na Inspector Veda (mwenye koti) wakisikiliza hoja za  Thobiasi Warioba (35), aliyeamua kuvua nguo zote na kubaki mtupu akiwa ameng'ang'ania mlingoti wa Bendera ya Taifa
Inspector Henry (shati la bahari) akiwa na Inspector Veda (mwenye koti) wakisikiliza hoja za Thobiasi Warioba (35), aliyeamua kuvua nguo zote na kubaki mtupu akiwa ameng’ang’ania mlingoti wa Bendera ya Taifa
Ushawishi ukiendelea.
Ushawishi ukiendelea.
Mahabusu Thobiasi Warioba (aliye mtupu) pamoja na mwenzake Hamis Ramadhani katu katu waking'ang'ania mlingoti wa bendera ya Taifa huku wakishinikiza kuzungumza na waandishi wa Habari.
Mahabusu Thobiasi Warioba (aliye mtupu) pamoja na mwenzake Hamis Ramadhani katu katu waking’ang’ania mlingoti wa bendera ya Taifa huku wakishinikiza kuzungumza na waandishi wa Habari.
Wananchi wakiwa wamefurika viwanja vya mahakama.
Wananchi wakiwa wamefurika viwanja vya mahakama.
Baada ya kuzungumza na waandishi wa habari mahabusu hao walikubali kurejea chumba cha Mahakama.
Baada ya kuzungumza na waandishi wa habari mahabusu hao walikubali kurejea chumba cha Mahakama.
Nje ya Mahakama kuelekea lango kuu.
Nje ya Mahakama kuelekea lango kuu.
Wananchi wamefurika viwanja vya mahakama.
Wananchi wamefurika viwanja vya mahakama.
Mashuhuda.
Mashuhuda.
 
Wananchi waliokuwa katika viwanja vya mahakamani hapo waliachwa midomo wazi na hali ya mshangao, mara baada ya mmoja kati ya hao wawili wakifanikiwa kuufikia mlingoti huo na kuvua nguo kisha kuanza kupiga kelele kwa kupaza sauti kudai haki itendeke.
 
Tukio hilo pia lilishuhudiwa na watumishi wa Mahakama ya Wilaya, Mahakama ya Mwanzo, Mamlaka ya Maji Safi na Majitaka ya jijini hapa (MWAUWASA), Askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), na taasisi zingine zilizo jirani na majengo ya mahakamani hapo na wananchi waliokuwa wakisubilia kesi zao kutajwa.
 
Mahabusu hao sita waliojaribu kutoroka na kuishia kudhibitiwa vyombo vya dola, walitajwa kwa majina kuwa ni Thobiasi Warioba (35), aliyeamua kuvua nguo zote na kubaki mtupu eneo la mlingoti wa Bendera ya Taifa, ambaye anakabiliwa na kesi ya mauaji Na. 32/2012.
 
Watuhumiwa wengine waliojaribu kutoroka ni Hamis Ramadani (30), Anthony Petro (35), Marwa Mwita (38), na Chacha Wangwe (35), na mwingine ambaye hakufahamika majina yake mara moja, wote wanakabiliwa na kesi ya Jinai Na. 215/2013  na walikamatwa tangu mwaka 2011.
 
Wakiwa katika viwanja vya mahakama hiyo baada ya kudhibitiwa na askari polisi, mmoja wa mahabusu hao walisikika wakisema:
“Haiwezekani, tangu mwaka 2011 tulipokamatwa hadi sasa kesi zetu hazijasikilizwa. Wengine tumebambikiziwa kesi.  “Tunaomba haki zetu, polisi mnatuonea, vyombo vya habari tunaomba mtusaidie  tumekaa muda mrefu bila kusikilizwa na hatujui hatma yetu tangu 2011 tulipo kamatwa tumechoka kukaa mahabusu, tunaomba kesi zetu zisikilizwe”.
 
Baada ya malalamiko yao, ndipo askari  mmoja aliyejitambulisha kuwa ni Inspekta Henry akiwa na wenzake sita waliokuwa wakiwadhibiti wasikimbie na kuwahoji kuhusiana na madai yao, huku askari hao wakiwataka kuondoka katika mlingoti huo na kumtaka Warioba avae nguo ili waweze kuingia mahakamani.
 
“Pamoja na maamuzi yenu haya, lakini mtambue mnavunja sheria na hili ni kosa jingine la jinai, hivyo ni vema mkaondoka kwenye mlingoti huu na kuingia mahakamani. Malalamiko yenu tumeyasikia na yatashughulikiwa,” alisema Inspekta Henry.
 
Mmoja wa maofisa waandamizi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, ambaye alikataa kutajwa jina lake, alidai ushahidi wa kesi za watuhumiwa hao bado haujakamilika, na kwamba kesi zao haziwezi kusikilizwa na mahakama ya wilaya kwani haina uwezo na badala yake zitatajwa tu kisha kuhamishiwa Mahakama Kuu.
 
“Bado hiyo ni Criminal Case (kesi ya mauaji) au PI Case hivyo Mahakama Kuu haiwezi kuzungumzia hilo kwa sasa kwa kuwa utaratibu wa mahakama kuu ikisha kuwa tayari huitwa ‘Criminary Session Case’, ambapo sasa hupangiwa namba ya kesi na Jaji wa kuisikiliza,”
Mbunge machachari wa Mwibara, Alphaxard Kangi Lugola, amedai kuwa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambayo yeye ni mbunge wake, inaendeshwa kisanii.
Lugola ambaye katika Bunge lililopita aliwaongoza wabunge wenzake kuichachafya Serikali hadi mawaziri wanne kujiuzulu nyadhifa zao, jana aligeuka tena mwiba kwa Serikali ya CCM.
Akichangia hotuba ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Lugola alisema anashangaa Waziri mwenye dhamana, Christopher Chizza kuendelea kuwa waziri wakati hotuba yake imejaa blabla.
Pia alimgeukia naibu wa wizara hiyo, Godfrey Zambi na kumwambia kuwa amejisahau kwamba naye alikuwa akikaa kiti cha nyuma bungeni akipaza sauti, lakini baada ya kupata madaraka amewageuka na kushirikiana na waziri.
Akichangia kwa hisia kali, Lugola alihoji inakuwaje wakulima wanapelekewa pembejeo feki, dawa feki na skimu za umwagiliaji zinachakachuliwa na bado Chizza anaendelea kubaki ofisini kama Waziri.
Lugola
“Hakuna lolote humu ni blabla tu… Mheshimiwa Zambi wewe ulikuwa ‘backbencher’ (kiti cha nyuma) kama mimi ulikuwa unapiga muziki kama kasuku juu ya wizara hii, leo unashirikiana na waziri wako unakuja na vitu ambavyo havina majibu, maana yake nini?
“Waziri huyuhuyu ndiye anayezindua mbegu aina ya Chutoni ambayo haioti, bado ni Waziri. Waziri huyu huyu analipa ruzuku mbegu ya pamba isiyoota bado ni Waziri,” alisema Lugola.
Lugola alihoji kama Mchina aliyekuwa akijenga daraja la Kilombero alijiua kwa sababu tu ya kuhofia kupigwa risasi atakaporudi kwao, hata Waziri Chizza alipaswa awe ameiacha kazi hiyo.

Lugola


“Simshauri waziri ajiue, lakini kwa vitendo vyote hivi waziri huyu angekuwa ameacha wizara hii na kupumzika na kufanya kazi nyingine mbadala,” alisema Lugola huku akipigiwa makofi.
Lugola alikumbushia Chizza alikuwa ni miongoni mwa mawaziri waliotajwa kuwa ni mizigo na kusema mambo yanayofanywa na wizara hiyo yatakigharimu Chama Cha Mapinduzi.
Mbunge huyo alibainisha kuwa, katika hotuba yake mwaka jana, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema Serikali iko kwenye mchakato wa kuanzisha mfuko wa kinga ya pamba ili kuwasaidia wakulima.
Hata hivyo, alisema katika hotuba ya Waziri Mkuu juzi, hakuna sehemu aliyozungumzia mfuko huo wala Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika katika hotuba yake ya mwaka huu, naye hajazungumzia mfuko huo.
“Hivi nchi hii tunaiendesha kwa usanii mpaka lini? Usanii juu ya usanii… Hatuwezi kuwadanganya wananchi kwa kiwango hiki. Itakuwaje mimi mbunge niunge mkono bajeti ya namna hii?” alihoji.
Alimgeukia Zambi na kumweleza kuwa aliwahi kumtahadharisha kuwa atakapokuja na bajeti yake ahakikishe anampa majibu ya asilimia 20 ya malipo waliyoahidiwa wakulima waliotumia mbegu ya chutoni.
“Uniambie asilimia 20 ya malipo ya wakulima ambayo waliahidiwa kwamba wakitumia chutoni walipwe kama sehemu ya malipo yao, lakini hili halimo kwenye bajeti,” alisema na kuongeza:
“Hakuna lolote humu ni blabla tu… Mheshimiwa Zambi wewe ulikuwa ‘backbencher’ (kiti cha nyuma) kama mimi ulikuwa unapiga muziki kama kasuku juu ya wizara hii, leo unashirikiana na waziri wako unakuja na vitu ambavyo havina majibu, maana yake nini?”
Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa (CCM), alisema wakati Zambi akiwa mbunge, alikuwa msitari wa mbele kupinga matumizi ya mbolea ya minjingu na kumtaka aeleze kama bado ana msimamo huo.
Kwa upande wake, Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda (Chadema), aliwashukia wakuu wa mikoa ya Simiyu na Geita kuwa ni chanzo cha tatizo kwa wakulima wa pamba.
Mbali na hilo, amemtaka Balozi wa Uingereza nchini ajitokeze kueleza misaada inayotolewa na nchi yake inavyotumiwa kwenye sekta ya pamba kwani imekuwa ni sehemu ya ubabaishaji kwa kuendeshwa semina zisizo na maana.
Shibuda alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akichangia maoni kwenye hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kwa mwaka 2014/15.
Aliwatuhumu wakuu hao kuwa walimpeleka Waziri Mkuu katika kampuni ya Kiotoni wakamdanganya kuwa mbegu hizo ni nzuri, lakini kumbe hazikuwa zimefanyiwa utafiti wa kina na kuwasababishia hasara kubwa wakulima.
Shibuda alisema mbegu za kiotoni zina udhalimu mkubwa na hazina tija yoyote kwa wakulima lakini kila siku wakuu wa mikoa na wilaya wanazipigia debe licha ya kuwa wanatambua kwamba wakulima wanaumizwa.
Magdalena Sakaya aliifananisha Serikali kuwa ni sawa na sikio la kufa kwa kuwa kila wakati imeshindwa kuwa na majibu ya ukombozi kwa wakulima wa Tanzania ambao ndio wapigakura wao.
Mbunge wa Kasulu, Moses Machali (NCCR-Mageuzi) aliwapongeza wabunge wa CCM wanaoonyesha ujasiri wa kuisema Serikali yao kuwa inaendesha mambo kisanii na hivyo kushindwa kuwaletea wananchi maendeleo.
“Serikali imekuwa ikidanganya katika kutatua matatizo ya wananchi ndiyo maana tunaona ni Serikali ya maigizo… Ukisoma hotuba ya bajeti hapa haijibu matatizo ya wananchi,” alisema.
Wakati wabunge hao wakiiponda bajeti hiyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeitaka Serikali, kueleza ni lini na vipi wakulima walioathirika na mbegu feki watafidiwa.
Msemaji wa Kambi hiyo wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Rose Kamili, alisema tayari wakulima wameshapata hasara na bado wako wanaoendelea kuathirika na tatizo la mbegu kutoota.
Habari hii imeandikwa na Daniel Mjema, Habel Chidawali na Fidelis Butahe

Jumamosi, 10 Mei 2014

Kutokana na kufanya vizuri kwa timu iliyoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania kwa mara ya kwanza na kufanya vizuri sana Shirikisho la Soka Afrika Mashariki na kati kupitia kwa katibu mkuu wake Bwana Nicholaus Musonye imeiteua timu ya soka Mbeya City Fc iliyomaliza ligi kuu Tanzania bara kwa kushika nafasi ya tau nyuma ya Yanga Fc 
Katika taarifa aliyoitoa kwa vyombo vya habari jijini Mbeya FREDDY JACKSON  alisema "
Ndugu wadau timu yenu ya Mbeya City Fc imepewa nafasi na katibu mkuu wa SECAFA ndugu Nicholaus Mufonye kushiriki michuano ya kombe la mto Nile "SECAFA NILE BASIN CUP" yatakayofanyika Hatoom Sudan kuanzia tarehe 22/5/2014 hii ni heshima iliyotokana na timu yenu kufanya vizuri na kuleta changamoto katika tigi kuu.
Ifuatayo ni orodha ya timu zitakazoshiriki na nchi zinakotoka.
El-shandy, El-arab, Merreck. zote za Sudan
Victoria university ya Uganda
Ports ya Djibouti
Ismailia ya Misiri
Polisi ya Zanzibar
Mbeya city ya Tanzania
polisi ya Ruanda
Fumbiue ya Burundi
A F C Leopards ya Kenya
De fence forces ya Ethiopia
El- mereck ya Sudan kusin
El-man yaSomalia.
timu hizo zitashindania Dollar 30,000.
maombi yenu ndio mafanikio ya timu yetu, tutakujulisha siku ya timu kuondoka kuelekea Sudan."
                                                           
Anaeonekana pichani juu kulia ni katibu mkuu wa SECAFA Bw.Nicholaus Musonye 


Jumatano, 7 Mei 2014

ZILE tuzo saba alizotwaa nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwenye mkesha wa Jumapili iliyopita ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam zimezua balaa! Ni balaa gani hilo? Risasi Jumatano linakumegea.

Kwa mujibu wa chanzo makini, baadhi ya ndugu wa Diamond walicharuka kufuatia staa huyo aliyeshinda nafasi ya Msanii Bora wa Kiume wa Bongo Fleva 2014, kuzibeba tuzo hizo na kwenda kulala nazo kwa Wema Sepetu anayemtaja kuwa ni mpenzi wake kwa sasa.
di1Nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akipokea tuzo kutoka kwa Wema Sepetu.

MANENOMANENO YA BAADHI YA NDUGU
“Unajua kilichowakwaza sana baadhi ya ndugu ni kitendo cha Diamond kwenda kulala kwa Wema, Kijitonyama na tuzo zote saba.

“Wanasema alichotakiwa kukifanya, mara baada ya kutoka ukumbini angekwenda nazo nyumbani kwao (Sinza-Mori) akaziacha kisha ndiyo aende kwa huyo Wema wake,” kilisema chanzo hicho.
Kikaongeza:
di2…Akipokea tuzo kutoka kwa George Kavishe.

“Ujue Diamond anakoelekea anaanza kupotoka kwani mwanzo alikuwa haachani na mama yake hasa kwenye ishu kubwa kama hizo, mwaka huu ameonesha utovu wa nidhamu, maana ndugu wanaamini hakutaka kwenda na mama yake ukumbini kwa sababu alijua atakuwa na Wema.”

MARAFIKI PIA WASHANGAZWA
Chanzo kiliendelea kuanika kwamba baadhi ya  marafiki wa Diamond nao walionesha kushangazwa na kitendo cha mama Diamond (Sanura Kasim) kutoonekana kwenye ukumbi wakati mwanaye akipokea tuzo badala yake nyota huyo kuwa beneti na Wema.
di3Diamond akipokea tuzo kutoka kwa prodyuza Tuddy Thomas.

“Baadhi ya marafiki wamesema kuna kitu, kwa vile wanavyojua wao, shoo au jambo lolote ambalo Diamond anahusika, mama yake lazima aibuke naye. Wengi wanaamini uhusiano wa mama na mwanaye umevurugwa na kitendo cha Wema kurudiana na baby wake huyo,” kilisema chanzo hicho.

Kikaendelea: “Lakini kuna watu wanadai mama Diamond siku hiyo aliamua kwenda kwenye bethidei ya mpenzi wa zamani wa Diamond, yule Penny kwa sababu alipuuza uwepo wa Wema ukumbini.”
di4Mama yake Diamond akiwa na mtangazaji wa DTV Penny ambaye ni mpenzi wa zamani wa Diamond.

NDUGU WASAKWA
Baada ya paparazi wetu kuzinyaka taarifa hizo, alianza kuwasaka baadhi ya ndugu hao ili kujua ukweli wa madai yote.

WA KWANZA MAMA DIAMOND
Mtu wa kwanza kupatikana kwenye familia hiyo ni mama Diamond mwenyewe ambapo alibanwa kwa maswali kadhaa kama ifuatavyo:
Paparazi: “Mama Nasibu nimekuja kwa mambo mawili matatu. Kwanza nataka kujua ni kwa nini hukuonekana ukumbini siku ya Tuzo za Kili wakati mwanao anazoa tuzo saba? Maana wengine wanasema uliogopa uwepo wa Timu Wema, wengine wanasema ulikwenda kwenye bethidei ya Penny.
di5Penny akiwa katika pozi.

Pia kuna minong’ono kwamba, familia imechukizwa na kitendo cha Diamond kwenda kulala na tuzo zake nyumbani kwa Wema, ni kweli?

Mama: “Kwanza kabisa, siku ile mimi sikuwa na mpango wa kwenda kwenye shughuli hiyo, hasa niliposikia itaoneshwa laivu kwenye runinga.

“Napenda kukwambia kwamba kuanzia sasa huo ndiyo utakuwa utaratibu wangu. Zamani nilikuwa nikienda kwenye shoo, hasa zinazomuhusisha Diamond  kwa vile nilikuwa sijamuona namna ya utendaji kazi wake lakini sasa namwamini anaweza kuchapa kazi hata mimi nisipokuwepo.
di6…akipozi na mpenzi wake wema Sepetu.

KUHUSU TIMU WEMA, BETHIDEI YA PENNY
“Wanaosema mimi sijaenda ukumbini kwa sababu eti nilikuwa nikihofia Timu Wema si kweli na wala sikwenda kwenye bethidei ya Penny kama wasemavyo.

“Ninaomba itambulike kwamba mimi siko kwenye timu yoyote ile, kama timu basi mimi nipo Wasafi (ya Diamond) kwa maana ninamsapoti mwanangu kwa kila kazi yake na wala sina kitu tofauti na hicho.”

DIAMOND SASA
Diamond naye alikutwa nyumbani kwao siku hiyo akiwa na tuzo hizo ambazo ilidaiwa alikwenda nazo asubuhi iliyofuata baada ya kuamka kwa Wema, alipoulizwa juu ya kupitiliza nazo hadi nyumbani kwa Wema badala ya kuzipeleka kwa mama yake, alionekana kushindwa kujibu zaidi ya kucheka na kusema:

“Wabongo bwana, hawakosi sababu na maneno ya kuongea kwa kila kitu hata kama ningefanya nini lazima wangepata tu kipya cha kunizungmzia hivyo kwa hilo sina hata cha kujibu ila tuzo zipo hapa nyumbani kwa mama.”
di7
Add caption

KUHUSU MAMA YAKE KUTOKWENDA UKUMBINI
“Kuhusu mama kutokwenda ukumbini mimi najua wazi kwamba hakuhitaji na aliomba aangalizie nyumbani kupitia runinga na kusema kweli nimefurahi sana kupata tuzo hizi ingawa pia furaha yangu itakuwa kubwa sana kama nitanyakua na tuzo ya Channel O,” alisema Diamond.

HALIMA KIMWANA
Baada ya Diamond kuweka wazi, paparazi wetu alimtafuta Halima Kimwana ambaye naye alidaiwa kukacha kuzama ukumbini hapo kwa kuwa tu hana uhusiano mzuri na Wema na kwamba siku hiyo anadaiwa kwenda kwenye bethidei ya Penny ambaye ndiye rafiki yake kipenzi kwa sasa tangu alipoachika kwenye penzi la Diamond, msikilize Halima:

“Jumamosi siku tuzo zinatolewa mimi nilikuwa safarini Morogoro ambapo nilikwenda kufanya mambo yangu na mjini nilirudi Jumapili na mchana huohuo nilikwenda kweli kwenye bethidei ya Penny.
“Naomba ieleweke kwamba mimi sijakimbia timu yoyote na wala sitambui kama kuna kitu kinaitwa Timu Wema ila najua tu kaka Diamond ana uhusiano na Wema Sepetu, sijui hiyo Timu Wema ndiyo chombo gani?
CHANZO; GPL
boko
Hofu inazidi kutanda nchini Nigeria na matumaini ya kuwapata wanafunzi wa kike zaidi ya 200 waliotekwa nyara na kundi la Boko Haram yanapungua baada ya kiongozi wa kundi hilo kutangaza kuwa amepanga kuwauza.
“Nimewateka nyara wasichana wenu. Nitawauza sokoni, kwa jina la Mungu.”Alisema kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau kwenye video ambapo aliongea kwa lugha ya Hausa na tafsiri yake imetolewa na CNN.
“Kuna soko la kuuza binadamu. Mungu anasema inabidi niwauze. Ameniamuru niwauze. Nitawauza wanawake. Huwa nauza wanawake.” Aliongeza mtu huyo.

Takribani watu 1,500 wameuawa mwaka huu na kundi hilo ambalo maafisa wa Marekani wameeleza kuwa linasaidiwa kimafunzo na watu wenye uhusiano na kundi la Al Qaeda.
Kundi hilo limedai linawateka wanafunzi wa kike ikiwa ni mkakati wao haramu wa kupinga elimu ya magharibi.
Wananchi nchini Nigeria wameendelea kuandamana wakiishinikiza serikali kuharakisha mpango wa kuwaokoa na kuwalinda watoto wao na kundi hilo hatari.
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan amesema atafanya awezalo kuwaokoa wasichana hao.

Jumatatu, 5 Mei 2014


Kamati ya kuratibu Harambee ya kuchangia maafa wilayani Kyela katika picha ya pamoja

Miss Tanzania 2001 na mwanamitindo aishie nchini Marekani Happiness Magesse akikabidhi fedha Taslimu shilingi milioni moja kwa Mwenyekiti wa Kamati ya kuratibu Harambee Prof .Leonard  Mwaikambo



Miss na Mwanamitindo Happiness Magesse akiteta jambo na Martin Emanuel (Mwanzilishi na blogger wa KYELANyumbani blog)  

 Mbunge na Waziri wa Uchukuzi Dr.Harrison Mwakyembe ameowaongoza wanaKyela waishio jijini Dar Es Salaam na miji ya karibu katika Harambee ya uchangiaji kusaidia wananchi wilayani Kyela walioatirika na mafuriko makubwa na yaliyoleta athari mbalimbali na kubwa sana yaliyotokea mwishoni mwa mwezi April mwaka huu.
Prof Leonard Mwaikambo wenyekiti wa Kamati iliyoundwa na wanakyela kuratibu Harambee hiyo akitoa taarifa ya tathmini ya iliyofanyika na Ofisi ya mkuu wa wilaya katika harambee hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa mkabala na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM)amesema"Mafuriko hayo ambayo hayajawahi kutokea wilayani kwa miongo zaidi ya 4 yameleta athari mbalimbali kwa jamii kiuchumi na kijamii.Mfano Shule zaidi ya 3 za sekondari na msingi zimeathirika vibaya ,pia miundombinu imeharibiwa vibaya ikiwemo madaraja na barabara.Prof.Mwaikambo aliongeza kuwa tathmini hiyo inaeleza kuwa watu zaidi ya elfu ishirini na nne (24000) wameathirika kutokana na maafa hayo
Hivyo jumla ya kiasi cha zaidi ya bilioni 2 na milioni 800 zinahitajika kukabiliana na athari za mafuriko wilayani humo"
Baada ya taarifa hiyo kwa ufupi Waziri na mbunge wa jimbo la Kyela Dr.Harrison Mwakyembe aliongeza na kusema kuwa hali ni mbaya sana kwani yeye alifika wilayani na kushuhudia hali ilivyokuwa mbaya .Mfanoalishindwa kwenda Bujonde kwa sababu maji yalikuwa ni mengi kiasi cha mtu wa futi 6 anazama.Hadi nyumbani kwa Diwani wa kata hiyo kulikuwa kumejaa maji ambapo mashamba na mali kama mifugo vilikuwa vimeathirika sana.Waziri aliongeza kusema"Tunamshukuru Mungu mamba hawakuweza kuwaathiri binadamu maana kasi ya amaji ilikuwa kubwa sana kiasi ambacho mamba walishindwa kuishi kwa uhuru na kusababisha madhara zaidi "
Dr.Mwakyembe aliongeza kuwa Shule ya sekondari Mwaya imeathirika zaidi ambapo vitabu na vifaa vya maabara vimeharibika kabisa hivyo wanafunzi kushindwa kusoma Sayansi kabisa.
Dr Mwakyembe pia aliwashukuru watu,makundi na Taasisi mbalimbali zilizochangia kusaidia wahanga wa maafa haya kama Kanisa la Moraviana Tanzania,Kanisa la Roman Catholic Kyela ,Taasisi ya Pambana Saidia Jamii (SCSA) ,Kyela Media na Kyela Members,Umoja wa Wasanii Kyela,SUMATRA na wengine wengi
Baada ya maelezo hayo mafupi Mwenyekiti wa kamati ya Harambee Prof.Mwaikambo aliongoza Harambee hiyo ambapo watu wengi walitoa pesa na nguo na watu kuchangia mawazo pia.
Pia aliyekuwa Miss Tanzania 2001 Happiness Magese alichangia sare za shule 200 na kiasi cha pesa cha Shilingi milioni moja kwa kuanzia.
Hadi mwisho wa harambee ambayo itafanyika tena tarehe 1 mwezi wa 6 2014 kiasi cha shilingi milioni hamsini na tisa zilikuwa zimepatika ikiwa ni fedha Taslim na ahadi.
 Jaji Mwaikugile akitoke kijiji cha Itunge  akiongea kwenye Harambee












Mzee na mfanyabiara Mwamafupa akichangia shilingi laki moja








Ijumaa, 2 Mei 2014



Tukiwa tumesherekea miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar je unamjua mtu aliyetunga jina la Tanzania??? Pata historia ya namna mtu alivyofanikiwa kupata jina la T A N Z A N I A.
Sherehe za Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar huwa tunasherekea kila Mwaka Tarehe 26/04/ lakini Tangu mimi binafsi nipate ufahamu na kuanza kushuhudia sherehe za Muungano nimekuwa nikisikia kuwa jina la Tanzania lilipendekezwa na Watanganyika, Wazanzibar na Raia wengine wa nje lakini sikuwahi kumjua mtu ambae alibuni jina hili tamu la Tanzania.
Huyu bwana aliyebuni jina la Tanzania ni Muhindi na Dini yake ni AHMADIYA MUSLIM JAMAAT TANZANIA majina yake ni MOHAMMED IQBAL DAR.
Mohammed alizaliwa Mkoani Tanga miaka ya 1944,Baba mzazi wa Mohammed alikuwa Daktari huko mkoani Morogoro alikuwa anaitwa Dr. T  A DAR  alikuwa Tanganyika kuanzia mwaka 1930.
Mohammed Iqbal Dar alipata elimu yake ya Msingi Mkoani Morogoro shule ya Msingi H H D AGAKAN kwa sasa ni Shule ya Serikali na baada ya Hapo alikuja baadae kujiunga na Chuocha Mzumbe akasoma Kidato cha Kwanza mpaka cha Sita.
Aliingiaje kwenye shindano la kupendekeza  jina la Muungano kati Tanganyika na Zanzibar,Mohammed anasema alikuwa Maktaba akijisoma gazeti la Tanganyika Standard siku hizi Daily News akaona Tangazo linasema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unafahamika kama Republic of Tanganyika and Zanzibar jina likaonekana refu sana kwa hiyo Wananchi wote wakaombwa Washiriki kwenye shindano la Kupendekeza jina moja litakalo zitaja nchi zote mbili yaani Tanganyika na Zanzibar
Mohammed Iqbal Dar anasema aliamua kuingia kwenye Shindano na hivi ndivyo alianza Safari ya Kubuni Jina la Muungano,Kwanza anasema alichukua karatasi akaandika Bismillah Raahman Rahimu hii ni kutokana na Imani yake na baada ya hapo akaandika jina laTanganyika baada ya hapo akaandika Zanzibar halafu akaandika jina lake Iqbal halafu akaandika jina la Jumuiya yake ya Ahmadiya baada ya Hapo akamrudia tena Mwenyezi Mungu akamwomba amsaidie ili apate jina zuri kutoka katika majina hayo aliyokuwa ameyaandika.
Baada ya hapo Mohammed Iqbal Dar alichukua herufi tatu kutoka Tanganyika yaani TAN na kwa upande wa Zanzibar akachukua Herufi tatu za Mwanzo ZAN ukiunganisha unapataTANZAN alivyoona hivyo akachukua  herufi ya kwanza katika jina lake la Iqbal na akachukua A kutoka jina la dini yake yaani Ahmadiyya kwa maana hiyo ukiongeza herufi hizi mbili na A kwenye TANZAN unapata jina kamili TANZANIA akalisoma jina akaliona ni zuri lakini akajiridhisha pia kwamba akiongeza herufi hizo za na kwenye TANZAN italeta maana kwakuwa nchi nyingi za Afrika zinaishia na IA.
 mfano EthiopIA,ZambIA,NigerIA,TunisIA,SomalIA,GambIA,NamibIA,LiberIA,MauritanIAalivyoona hivyo akaamua apendekeze kuwa jina TANZANIA ndio litumike kuwakilisha nnchi hizi mbili yaani Tanganyika na Zanzibar kwa maana hiyo jina TANZANIA limezaliwa kutoka majina manne majina hayo ni Tanganyika,Zanzibar,Iqbal na Ahmadiyya
Mohammed Iqbal  Dar baada ya kupata jina hilo akalituma jina hilo kwenye kamati ya kuratibu  Shindano
Baada ya Muda mwingi kupita  baba yake na Mohammed Iqbal Dar alipokea Barua nzito kutoka serikalini ikiwa inasomeka kama ifuatavyo….
                                                               

                                                     REPRESENTED BY THE
                                MINISTRY OF INFORMATION AND TOURISM,TANZANIA
                                                                     TO
                                                  MOHAMED IQBAL DAR
                 IN RECOGNATION OF THE ACHIEVEMENT OF CHOOSING THE NEW NAME FOR THE
                                    UNITED REPUBLIC OF TANGANYIKA AND ZANZIBAR NAMELY
                                                  “REPUBLIC OF TANZANIA”
                 DURING THE NATIONAL COMPETITION DAY IN 19TH NOVEMBER 1964
                                                            I A WAKAL
                              MINISTER FOR INFORMATION AND TOURRISM
Barua hiyo pia ilisema..
Utakumbuka kuwa miezi michache iliyopita ulituandikia kutupa ushauri kuhusu jina jipya la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar  na wewe pamoja na wananchi wenzio 16 ulishauri nnchi yetu iitwe Tanzania.Nafurahi kukuarifu kuwa mshirikiane ile Zawadi y ash.200 iliyoahidiwa na leo nakuletea check ya sh.12/50 ikiwa ni hisa yako katika zile sh.200.Nashukuru sana kwa jitihada ya kufikiri jina la Jamuhuri yetu
Barua ikasainiwa na Idrisa Abdul Wakil Waziri wa Habari na utalii kipindi hicho.
Sasa kwa nini Mohamedi Iqbal Dar anadai yeye kuwa mshindi pekee wakati Barua ilikuwa inaonyeshakulikuwa na washindi wengine 15 ambao nao walishinda,Jibu ni kuwa wakati wa kutolewa kwa Zawadi hizo hakuna aliyejitokeza zaidi ya Bwana Mohammed Iqbal Dar na Bwana Yusufal Pir Mohamed ambaye hata hivyo alikosa sifa baada ya kushindwa kutoa barua ya kumpongeza kuwa ameshinda kwa madai kuwa Barua ameipoteza,hivyo Wizara ya Habari na Utalii iliamua kumtangaza bwana Mohammed Iqbal Dar kuwa Mshindi na kumpatia zawadi yote y ash.200/:pamoja na Ngao.
Bwana Mohammedi Iqbal Dar anasema anachosikitika ni kuwa Mchango wake bado Watanzania hawathamini mchango wake lakini yeye anaipenda Tanzania na anajivunia kuwa Mtanzania japo anadhani dini yake ya Uislamu ndio tatizo hawataki kutambua mchango wake ila anaamini kuwa siku moja ukweli utajulikana
Hayo ni maelezo ya Mohammed Iqbal Dar ambaye kwa sasa anaishi Uingereza kwa kuwa huko ndiko alipata kazi eneo la Birmigham b35 6ps UK,Dar –es-Salaam House,18 TURNHOUSE ROAD,PHONE 44 121-747-9822