Ijumaa, 29 Mei 2015

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Bwana Abas Kandoro akiongea kwenye mkutano wa RCC
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Kyela Bwana Gabriel Kipija na wajumbe wengine wakifuatilia kwa makini mkutano wa RCC jijini Mbeya
KAMATI ya ushauri ya Mkoa wa Mbeya (RCC) imepitia na kupitisha mapendekezo ya Halmashauri za Mkoa huo ya kugawa majimbo na mengine kubadili majimbo ya uchaguzi. Jimbo la Kyela limekosa kigezo cha kugawanywa hivyo litaendelea kubaki jimbo moja kama ilivyokuwa awali likiungana na majimbo ya Ileje, Lupa,Songwe,Mbeya Mjini na Mbarali. Awali Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya Kyela walipitisha kwa kauli moja mapendekezo ya Jimbo la Kyela kugawanywa na kuwa majimbo mawili yaani Kyela Mjini na Kyela Vijijini Jimbo la Kyela limeshindwa kukidhi sifa mbili ambazo ni Jiografia na Idadi ya watu Akifafanua katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkapa uliopo Sokomatola jijini Mbeya, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bwana Abbas Kandoro alisema kikao hicho kimekubaliana na baadhi ya mapendekezo na mengine kuyakataa. Kandoro alisema mapendekezo hayo yamezingatia vigezo vilivyotolewa ambavyo ni idadi ya watu katika jimbo na hali ya Kijografia ambayo inamuwia vigumu Mbunge mmoja kuwafikia wananchi wake kwakati ikiwa ni pamoja na mawasiliano. Aliyataja majimbo waliyokubaliana kuyagawa kuwa ni pamoja na Jimbo la Mbozi Magharibi linalogawanywa kupata majimbo ya Momba na Tunduma, Mbozi Mashariki inakuwa na majimbo ya Vwawa na Mbozi. Kandoro alisema jimbo lingine lililopitishwa kugawanywa ni Jimbo la Mbeya vijijini linalokuwa na Jimbo la Santilya na Mbeya vijijini na kufafanua kuwa Jimbo hilo linakosa kigezo cha idadi ya watu lakini kutokana na hali ya Jografia na mawasiliano ni vigumu kuongozwa na Mbunge mmoja. Aliongeza kuwa Majimbo mengine yamebadilishwa majina kutokanana mapendekezo ya Halmashauri ambayo ni Jimbo la Rungwe Mashariki kuwa Jimbo la Busokelo na Jimbo la Rungwe Magharibi kuwa jimbo la Rungwe. Alisema Majimbo mengine yaliyopendekezwa na halmashari ni pamoja na Halmshauri ya Jiji la Mbeya lakini wazo lao limekataliwa kutokana na kukosa vigezo ambavyo ni kuwa na idadi ndogo ya watu, kuwa na mawasiliano mazuri na ukubwa wa eneo linalofikia kilomita za mraba 214. Aliongeza kuwa vigezo vingine vinavyoifanya Halmashauri ya jiji kushindwa kugawanywa ni kutokana na kutokuwa na changamoto nyingi zinazowakabili wananchi, muingiliano wa mamlaka kwa majimbo mawili kuwa chini ya Halmashauri moja.

Jumanne, 19 Mei 2015

Meneja wa NMB Kanda ya nyanda za Juu kusini LUCRESIA MAKIRIYE akikabidhi madawati 60 yenye thamani ya shilingi zaidi ya Milioni tano kwa mkuu wa wilaya ya Kyela, Dkt THEA NTARA kwaajili ya wanafunzi wa shule ya msingi LUBELE.
Meneja wa NMB Kanda ya nyanda za Juu kusini akishikana mkono na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela GABRIEL KIPIJA
Meneja wa NMB Kanda ya nyanda za juu kusini LUCRESIA MAKIRIYE akikabidhi madawati serikali ya wilaya ya kyela akishikana mkono na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela CLEMENCE KASSONGO.

Katika uwajibikaji kwa jamii Kampuni ya kifedha ya National Microfinance Bank(NMB) imeendelea kuchangia katika kushirikiana na serikali kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya Elimu Wilayani Kyela. Kutokana na uhaba wa Madawati katika shule za msingi mkoani Mbeya,Benki ya NMB Nyanda za Juu Kusini kupitia kwa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya nyanda za Juu kusini,LUCRESIA MAKIRIE amesema benki hiyo itaendelea kuunga mkono Juhudi zinazofanywa na serikali katika uboreshaji wa sekta ya elimu nchini. MAKIRIE ametoa kauli hiyo wakati wa Hafla ya kukabidhi Madawati 60 katika shule ya msingi Lubele iliyopo Kasumulu boda mjini Kyela yenye thamani ya zaidi shilingi milioni tano,na kuongeza kuwa NMB Bank wataendelea kuchangia uimarishaji wa miundombinu katika shule za msingi na sekondari wilayani Kyela. Alisema Benki hiyo itaendelea kuhakikisha sekta ya elimu inaimarika kwa kutoa misaada mbali mbali pale inapokuwa inahitajika na kuongeza kuwa msaada huo ni sehemu ya utaratibu wa benki hiyo kurudisha fadhila kwa wateja wake kupitia huduma za kijamii. Wakipokea msaada huo kwa niaba ya Serikali wilayani Kyela ,Mkuu wa Wilaya Kyela Dkt THEA NTARA,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela ndugu CLEMENCE KASSONGO na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Mheshimiwa GABRIEL KIPIJA wameishukuru Benki ya NMB kwa kuendelea kuchangia katika maendeleo ya Elimu na jumla wilayani Kyela. Kutokana na msaada huo, Utakuwa umepunguza pengo la upungufu wa madawati katika Shule za Wilaya ya Kyela ambayo hadi sasa inakabiliwa na upungufu wa madawati 1600 na kupelekea wanafunzi kusoma kwa shida baada ya kubanana darasani.

Alhamisi, 7 Mei 2015

Wafanyabiashara wa soko kuu wanafanya uchaguzi kuwapata viongozi watakaoongoza kwa miaka mitatu baada ya uongozi uliokuwepo kumaliza muda wake. Pamoja na hayo uchaguzi umefanyika nakuwapata viongozi lkn aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti BENARD KYANDO na kusema kuwa pamoja na kupata kura nyingi hayuko tayar kuwa mwenyekiti,huku wafanyabiashara wakimuhitaji kuwa kiongozi wao,Vikao vinaendelea kumshawishi kukubali maombi ya wafanyabiashara. Endelea kutufuatilia.............