Jumapili, 6 Septemba 2015



Mgombea wa Ubunge jimbo la Kyela Bwana Abraham Mwanyamaki akiwasili katika viwanja vya Mchaga almaarufu Uwanja wa SUGU katika uzinduzi wa Kampeni za Ubunge wilayani Kyela kwa tiketi ya CHADEMA na UKAWA

Mheshimiwa Joseph Mbilinyi akiunguruma katika uzinduzi wa kampeni jimboni Kyela kwa CHADEMA









Mara baada ya kipyenga cha kampeni kupulizwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi kampeni zimeanza rasmi ambapo jana ilikuwa ni zamu ya UKAWA kuzindua kampeni zao za Udiwani.Wananchi wilayani Kyela wamekuwa wakijitokeza kusikiliza sera za wagombea mbalimbali wa nafasi za ubunge na udiwani. Mgombea ubunge wa jimbo la kyela kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na UKAWA Bwana Abraham Mwanyamaki amesema kuwa wanakyela wanajukumu moja tu la kumuunga mkono awaongoze katika kufanya mabadiliko ili wilaya isonge mbele kimaendeleo.
Mwanyamaki amesema kuwa endapo atapewa ridhaa ya kuwa mbunge atahakikisha wilaya ya Kyela inapiga hatua kubwa katika nyanja mbalimbali ikiwemo ELIMU,KILIMO ,UVUVI ,MIUNDOMBINU na BIASHARA kwa ujumla.Pia amegusia suala la kufungiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kwa radio ya jamii wilayani Kyela radio KYELA FM kuwa atahakikisha inafunguliwa ili iendelee kuwahudumia wanajamii wa kyela na maeneo jirani kwa kutambua umuhimu na haki ya mwananchi kupata habari.
Kwa upande wake mgombea ubunge jimbo la mbeya mjini Joseph Mbilinyi (Sugu) amesema kuwa kyela ina rasilimali nyingi lakini imekosa msimamizi wa kutafuta wahisani wa kununua amesema endapo wanakyela wataipatia chadema kura za kuongoza jimbo hilo basi Kyela itazaliwa upya. Pia mwanahabari nguli nchini aliyekuwepo katika uzinduzi wa kampeni hizo Bwana Saed Kubenea ambaye pia ni mgombea wa jimbo la Ubungo kupitia CHADEMA aliyegusa zaidi upande wa ufisadi wa CCM huku akitumia nyaraka mbalimbali aliwaomba wananchi wa Kyela kumchagua Bwana Mwanyamaki ili aweze kupeperusha na kuifanyia kazi Ilani ya CHADEMA kwa mabadiliko ya Kyela..........
LEO CHADEMA WANAENDELEA NA KAMPENI ZAO HUKO NGONGAAAAAAA
eNDELEA KUTUFUATILIAAAAAAAA.....MTANDAO WAKO WA NYUMBANI

Jumamosi, 5 Septemba 2015


Mkuu wa wilaya akiwa maeneo ya katikati ya mji wa Kyela kuhamasisha usafi wa mazingira wilayani Kyela
Mkuu wa wilaya ya Kyela Bi Thea Ntara amesema kuwa ni wajibu wa kila mtu kufanya usafi maeneo yake ya kazi au anapoishi ili kuondokana na magonjwa ya mlipuko.Mkuu huyo wa wilaya ameyasema hayo katika mahojiano maalum na mwandishi wa mtandao wako wa Nyumbani KYELA Nyumbani katika kuhamasisha usafi wa mazingira wilayani Kyela.
Hata hivyo Ntara amewataka wananchi kufanya usafi bila kusimamiwa ili kuondokana na adhabu zinazoweza kutolewa kwa watakaoshindwa kufanya usafi wa mazingira.

Wilaya ya Kyela kupitia mamlaka ya mji mdogo wa Kyela imejiwekea utaratibu wa kuhamasisha wananchi wake kuhusu usafi wa mazingira kila juma mosi ya kwanza ya mwezi. Katika kampeni hiyo ya kufanya usafi viongozi wa wilaya wanapita kuangalia zoezi hilo linavyotekelezwa ili kuhakikisha utekelezaji wake unatimizwa .
Maeneo aliyopitia mkuu wa wilaya kukagua ni Kalumbulu,Salama, Mikoroshini,Kyela Kati na maeneo mengine mengi. Utafiti uliofanywa na Mtandao wako wa Nyumbani umegundua kuwa mara baada ya mkuu wa wilaya kuamua kuacha ofisini kusubiria taarifa na kwenda moja kwa moja mitaani kuhamasisha na kuangalia zoezi hilo linavyotekelezwa mafanikio yameonekana kwa maeneo mengi kuwa na kiwango kinachotakiwa katika usafi wa mazingira.KYELA Nyumbani inampongeza sana mkuu wa wilaya kwa hatua aliyoichukua na kuwahamasisha viongozi wengine kuacha kukaa ofisini na kwenda mitaani kusimamia na kuhmasisha shughuli mbalimbali za maendeleo
Imeandikwa na ;PUYOL B MWASAMPETA
Imehaririwa na ;MARTIN EMANUEL

Ijumaa, 17 Julai 2015


Bwana Katule Kingamkono akionesha fomu kwa wananchi wa kata ya Ikimba

  Bwana Katule Kingamkono akiwa na mkewe wakisaini fomu ya kuomba kuwania kuteuliwa na CCM kugombea udiwani kata ya Ikimba
Bwana Katule Kingamkono akipokea fomu ya kuwania kuteuliwa na CCM kugombea diwani wa kata ya Ikimba




Mtia nia ya kugombea udiwani kata ya Ikimba kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi Bwana Katule Kingamkono amechukua rasmi fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama cha Mapindzi kugombea udiwani kata ya Ikimba .Bwana Katule Kingamkono amechukua fomu hiyo katika ofisi za CCM kata ya Ikimba jana.Akiongea na wananchi na wanaCCM mamia waliomsindikiza katika hatua hiyo muhimu na adhimu kuelekea kuiwakilisha kata ya Ikimba pale Halmashauri ya Wilaya ya Kyela kwa mustakabali wa maendeleo ya Kata na wananchi wa Ikimba Bwana Katule Kingamkono amesema "atakuwa mwaminifu na mwadilifu kuwatumikia wananchi endapo atapewa ridhaa ya kupeperusha bendera ya  chama hicho."
Ameyasema hayo wakati anachukua formu ya kuomba ridhaa hiyo ambapo mamia  ya wanaikimba walijitokeza kumsindikiza mtia nia huyo.

Hata hivyo Katule Kingamkono ni mmoja aliesuruhisha mgogoro wa timu ya mpira ya Ilala uliodumu zaidi ya miezi sita pamoja na kusaidia mambo mbalimbali katika jamii ukiwemo ujenzi madaraja na kuinua vipaji vya mpira wa miguu kwa kuweka ligi mbalimbali ndani ya kata hiyo ya Ikimba
Bwana Katule Kingamkono  amewaomba wanaikimba kumpa ushirikiano ili kufanikisha maendeleo ya Ikimba endapo atachaguliwa.

Kauli mbiu ya Bwana Katule Kingamkono ni SASAFARI YA UHAKIKA.

Imeandikwa na PUYOL B MWASAMPETA (0757337870)
Imehaririwa na MARTIN EMANUEL(0769858521)