Jumatano, 18 Desemba 2013

Kijana mmoja wilayani humu aliyejulikana kwa jina  la Robert John Mbembela amehukumiwa kutumikia kifungo cha maisha jela na Hakimu wa mahakama ya Wilaya ya Kyela kwa kosa la kumbaka na kumlawiti binti wa miaka 9 na kumharibu vibaya sehemu zake mbili za siri.
Shuhuda wa tukio hilo aliyekuwepo katika mahakama ya wilaya ya Kyela ambapo kesi hiyo ilikuwa ikiendeshwa  ameeleza kuwa kijana Robert ambaye ni mkazi wa mikoroshoni / Ndandalo wilayani Kyela alitoroka gerezani Tukuyu alikokuwa anatumikia kifungo cha miezi mitatu(3) kwa kosa la wizi.
Baadaye akiwa anatafutwa na jeshi la Magereza ndipo alipofanya tukio hilo na hapo ndipo alipokamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya Sheria.
Huko alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja kwa kosa la kutoroka Gerezani na kusomewa shitaka la kumbaka na kumlawiti binti wa miaka 9 ambayo hukumu yake ndio iliyotolewa leo hii mchana
Kyela Nyumbani inaendelea kufuatilia zaidi habari hizi kutoka mahakani Kyela tutawaletea habari zaidi
       KYELA Nyumbani "Hapa ndio Asili yangu"

0 comments :

Chapisha Maoni