Na baraka mbolembole
Kocha mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic tayari ameonesha kufanya
mabadiliko katika upangaji wa kikosi chake, huku yule wa timu ya
Yanga, Ernie Brandts akiongeza suala la stamina kwa kikosi chake.
Logarusic alimpanga kiungo, Henry Joseph katika nafasi ya ulinzi wa
kati wakati wa mchezo wa kirafiki dhidi ya KMKM, wikiendi iliyopita na
mchezaji huyo alionesha kiwango kizuri.
Kwa upande wa Yanga, kuwasili nchini na kujiunga na kambi ya timu
hiyo iliyopo katika hotel ya Protea kwa mshambuliaji, Emmanuel Okwi
kunataraji kuongeza ufanisi na makali zaidi safu ya mashambulizi ambayo mara kwa mara kocha, Brandts amekuwa akisema kuwa ni ' butu' na inayopoteza nafasi nyingi za kufunga, Okwi ni silaha ya hatari, huku
ushirikiano wake na washambuliaji Hamis Kizza na Mrisho Ngassa
ukisubiriwa kwa hamu.
MARA YA MWISHO...
April 20, 2003, mabao ya harakaharaka yaliyofungwa na kiungo, Salumu
Athumani, na mshambuliaji, Herry Morris katika dakika za 30 na 32, na
lile la dakika ya pili baada ya kuanza kwa kipindi cha pili la
kiungo-mshambuliaji, Kudra Omary yaliweza kuipatia ushindi wa mabao 3-0 Yanga katika uwanja wa CCM Kirumba, awali wiki mbili nyuma timu hizo zilifungana bao 1-1 katika mchezo wa kwanza wa kirafiki katika uwanja wa Uhuru. Simba ilitangulia kufunga kupitia kwa mshambuliaji Jumanne Shengo Tondola, na Yanga wakasawazisha kupitia kwa kiungo, Mrundi, Mwinyi Rajab.
Kuongezwa kwa Okwi, na Said Dilunga katika kikosi cha Yanga kunaweza
kuwa kumeipa timu hiyo uimara zaidi katikati na bunduki muhimu mbele.
Lakini hakutasahihisha udhaifu mkubwa wa safu ya ulinzi. Kwa kuwa hata mabeki chaguo la kwanza wanapokuwa fiti, safu ya ulinzi huonekana kupwaya, waliruhusu mabao matatu dhidi ya Azam FC, na baadae Simba wakachomoa mabao yao matatu. Nahodha wa kikosi hicho, Nadir Haroub
amekuwa akionesha dhahiri uwezo wake katika mchezo wa ' man to man',
ila si mzuri katika kujipanga na kuzuhia njia za hatari,
David Luhende bado anajaribu kiwango ambacho kilimfanya kuwa mchezaji wakutumainiwa katika nafasi ya ulinzi wa kushoto, Mbuyu Twite ni namba mbilI mzuri, anashambulia na kuzuhia kwa haraka, mtaalamu wa mipira ya kurushwa na mwenye uwezo mkubwa kwa kupiga mipira iliyokufa. Kocha, Brandts mara nyingi alikuwa akipiga kelele kuwa anahitaji mshambuliaji, na golikipa, na tayari amewapata Okwi na Juma Kaseja, ila hakuonekana kudai nyongeza yoyote ya mlinzi, hasa yule wa kati. Ni Kelvin Yondan pekee anayeweza kucheza mfululizo katika kinachoweza kuitwa kiwango cha juu. Uwepo wa washambuliaji kama Betram Mombeki, Hamis Tambwe, Edward Christopher kunaweza kumkumbusha kocha huyo kosa alilolifanya.
SIMBA KAMA BARCELONA, YANGA KAMA REAL MADRID
Barcelona, mara zote huwa wanatoa matokeo ya kushangaza, pale wanapotabiriwa kufanya vyema huwa wanaanguka vibaya, na pele wasipotarajiwa huwa wanafanya maajabu. Wakiwa na mchezaji bora zaidi duniani, mahasimu wao wanao wachezaji wa bei mbaya ndani ya uwanja. Katika mchezo wao wa kwanza wa ' clasico', Real Madrid ilitota mbele ya Barca. Na sasa, pengine uwepo wa Haruna Niyonzima, Okwi, Hamis Kiza, Didier Kavumbagu, Twite, Kelvin, Nadir, Yanga wakawa na thamani kubwa zaidi ndani ya uwanja, kipesa. Ila Simba imekuwa timu yenye vipaji vinavyoendana na utamadunia wao wa mchezo wa pasi za chini chini.
Herry Joseph atasogea katika nafasi ya kiungo wa ulinzi ili kumpisha mlinzi, Donald Musoti kucheza na Joseph Owino. Uchezaji wa Amri Kiemba unaweza kuwa silaha, au maangamizi kwa Simba endapo atakuwa katika kiwango cha juu Simba itaendelea kuwa timu ile ile inayojiamini ikicheza na Yanga, na endapo itatokea kucheza kwa kiwango cha chini, timu itapotea uwanjani kama ilivyokuwa mwezi oktoba, wakati ule Jonas Mkude aliposhindwa kujiamini.
4-3-3
Timu ya Yanga inaweza kuwapanga kwa pamoja, Okwi, Kiza, na Ngassa katika safu ya mashambilizi jambo ambalo litawachanga walinzi wa pembeni wa Simba, ambao kwa sasa hawapo katika viwango vya juu. Simba inataraji kutumia mfumo huo pia, na uwepo wa kiungo Awadg Juma utaunganisha nguvu na viungo, Mkude na Henry, na kuwaacha Tambwe, Mombeki, na Kiemba katika safu ya mbele.
Kwa kuwa ni mechi ambayo Yanga wanaitumia kuipanga timu yao katika usawa, ni wakati mzuri wa kuwapanga pamoja, Chuji, Domayo na Niyonzima katika kiungo ili kuuchezesha mfumo huo kwa mwendo unaotakiwa, kasi na pasi za uhakika, fupi fupi au zile zenye urefu na macho ya kuangaza. Yanga wanao wachezaji hao na Simba kwa sasa ni timu inayotakiwa kujiendesha kwa mfumo wa 4-4-2 kwa kuwatumia mawinga kupiga krosi kwa washambuliaji wao ambao wanaonekana ni wazuri kwa mipira hiyo.
YANGA, JUMA KASEJA GOLINI
Ni kipa mzuri, kama ambavyo ameweza kudhihirisha hilo kwa kipindi cha miaka 11 sasa, Kaseja atasimama katika mchezo wake wa kwanza wa uhakika tangu mwezi, septemba alipoiwakilisha timu ya taifa katika mchezo wa kufuzu kwa fainali za kombe la dunia dhidi ya Gambia. Aliruhusu mabao mawili wakati Yanga iliposhinda kwa mabao 3-2 dhidi ya KMKM ya Zanzibar, wiki iliyopita. Ataongeza kitu katika lango la Yanga na safu nzima ya ulinzi. Kuwakumbusha majukumu yao mara kwa mara walinzi, kucheza mipira ya kona na krosi ambayo iliwapa sare ya 3-3 katika mchezo wa mwisho wa mahasimu hao.
0 comments :
Chapisha Maoni