Ijumaa, 3 Januari 2014

MKUU wa Mkoa wa Mbeya,Abbas Kandoro, ameviagiza, Chama cha Mapinduzi (CCM)mkoa  na chama cha soka(Mrefa) kukutana na kuweka njia bora ya kukusanya michango ya fedha inayotolewa na wadau kwa ajili ya kazi ya upandaji nyasi katika wa Sokoine, baada ya kuibuka hisia za ubadhirifu wa fedha hizo.


Ukarabati wa uwanja wa sokoine Mbeya ukiendelea kwa kasi ndogo

Hii ndiyo hali halisi kwa sasa katika uwanja huo






MKUU wa Mkoa wa Mbeya,Abbas Kandoro, ameviagiza, Chama cha Mapinduzi (CCM)mkoa  na chama cha soka(Mrefa) kukutana na kuweka njia bora ya kukusanya michango ya fedha inayotolewa na wadau kwa ajili ya kazi ya upandaji nyasi katika wa Sokoine, baada ya kuibuka hisia za ubadhirifu wa fedha hizo.

Alitoa Agizo hilo baada ya kutembelea uwanjani hapo, hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku chache baada ya Clouds fm kutangaza  habari iliyomtaka kuingilia kati zoezi hilo la upandaji nyasi baada ya kuonekana kusuasua.

Kandoro baada ya kufika uwanjani hapo na kukuta kazi ikisuasua, aliomba maelezo ya kina kutoka kwa viongozi wa CCM na Mrefa, pamoja na sababu zinazokwamisha kazik hiyo kufanyika kwa ufanisi ili kuendana na ratiba ya bodi ya ligi iliyoamuru kufungiwa kwa uwanja huo kutokana na kasoro nyingi.

Akitoa maelezo, M wenyekiti wa CCM  mkoa, Godfrey Zambi, alisema zoiezi hilo limeendelea kusuasua kutokana na kukosekana nguvu kazi ya kutosha na usimamizi duni wa shughulli hiyo.

“Mkuu wa mkoa kule ndani ya kikao tulipata maelezo ambayo yako tofauti na hali tuliyoikuta hapas na kwa hali hii kuna uwezekano ikasababisha watu kukosa kuona mechi katika mzunguko wa pili” alilalamika kwa hasira Zambi.
Kabla ya Zambi kumaliza kutoa maelezo, ghafla mafundi waliokuwepo uwanjani hapo walikatiza maezo na kuanza kulalamika kutolipwa fedha zao, pamoja na sababu nyingine zinazokwamisha kuendelea kufanyika kwa haraka kwa zoezi hilo.

“Mfano leo tumekosa kabisa nyasi za kupanda….maana wanakijiji wamezuia mzigo wa nyasi zilizokatwa usib ebwe mpaka walipwe fedha zao , jambo ambalo limekwamisha zoezi zima” alisema mmoja wa vibarua haol.

Kibarua mwingine alisema walilazimika kuhama kijiji cha wali walikokuwa wakichimba nyasi hizo na kuhamia kungine kutokana na serikali ya kijiji kuchachamaa kutokana na kutolipwa fedha zao za wiki mbili zilizopita.
Kutokana na maelezo hayo ya vibarua, Mkuu wa Mkoa aliwatataka Mkurugenzi wa Jiji, Mussa  Nzungiza, na viongozi wa chama cha soka watoe majibu.

Hata hivyo katika hali iliyojaa mkanganyiko, Mkurugenzi wa Jiji alisema kuwa wao wamekuwa wakitoa fedha kila siku kadiri ya Mrefa wanavyopeleka mahitaji, jambo lililopingwa hapo hapo na M akamu mwenyekiti wa Mrefa,Omary Mahinya.

“Mkuu wa Mkoa naomba niweke sawa maelezo ya mkurugenzi, sisi kama Mrefa hatujapekea fedha hizo, kwani sisi tulichofanywa ni kmuk,opeshwa kiasi cha shilingi milioni tano na TFF(Shirikisho la soka hapa nchiniP)” alifafanua Mahinya na kumshangaza mkuu wa mkoa.

Baada ya kuona sarakasi zinaendelea katika maelezo hayo, ndipo Mkuu wa Mkoa aliamua kutoa agizo “kuanzia sasa naomba CCM na mrefa make chini na kupan ga utaratibu mzuri wa hizi fedha na mimi naahidi kufuatilia hatua kwa hatua, haiwezekani mtuharibie mambo hapa” alihitimisha Kandoro.

Hata hivyo katika kuonesha kuguswa na hali hiyo, MKandoro alianzisha ziara ya kushitukmiza hadi katika vijiji zinakochimbwa nyasi hizo umbali wa kilometa 40, ambapo Alikutana na malalamiko ya wananchi kutolipwa fedha zao kiasi cha shilingi 600,000 na kuamua kutoa nusu ya fedha hizo na kuwaahidi kiasi kilichobaki kulipwa ndani ya siku mbili.

Siku chache zilizopita, Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Mbeya, elius Mwanjala, alisema zoezi hilo lingekamilika leo baada ya kupata kiasi cha shilingi milioni 8 kati ya 10 walizokuwa  wakizihitaji.


Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa Kandoro alipokea ombi la wadau la kutaka kazi ya upandaji nyasi ichukuliwe na Jeshi la kujenga Taifa (JKT) kwa kushirikiana na wataalamu kmwa kuahidi kulifanyia kazi haraka iwezekanavyo.

Kwa upande wake, mtaalam wa kupanda nyasi ndani ya uwanja huo, Siddy Ibrahim , alisema kama yale yalioashidiwa na viongozi yatatekelezwa na hadi kufikia Januari 3 zoezi likakamilika, uwezekano wa wa mechi za mzunguko wa pili kuchezewa katika uwanja huo utakuwepo.


Picha na Mbeya yetu

0 comments :

Chapisha Maoni