Jumatano, 7 Januari 2015

Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya kyela wamekiri kuiingiza serikali hasara kwa kutosimamia ipasavyo utekelezaji wa miradi ya TASAF awamu ya kwanza na ya pili, hali iliyosababisha baadhi ya miradi hiyo kujengwa kwa kiwango cha chini kwenye maeneo mbalimbali katika kata zao. Wakizungumza wakati wa uzinduzi wa awamu ya tatu ya mradi wa TASAF wilayani Kyela, madiwani wa halmashauri hiyo wamesema sababu kubwa zilizosababisha Hasara hizo ni pamoja na Ukosefu wa elimu ya kutosha kwa madiwani pamoja na Uelewa mdogo wa wananchi kuhusiana na miradi ya TASAF ulisababisha awamu ya kwanza na ya pili kutotekelezwa kwa kiwango kinachotakiwa, lakini katika awamu ya tatu ya TASAF baada ya kuelimishwa pamoja na uzoefu walionao hawakusudii kurudia makosa. Waratibu wa TASAF ngazi ya wilaya, mkoa na taifa wamesema kuwa awamu ya tatu inakusudiwa kuzisaidia kaya masikini ambazo zitakidhi vigezo vilivyowekwa.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya kyela, Gabriel Kipija ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa awamu ya tatu ya TASAF wilayani kyela amewataka madiwani na watendaji wa halmashauri hiyo kujipanga upya ili wasirudie makosa yaliyojitokeza kwenye awamu zilizotangulia.

0 comments :

Chapisha Maoni