Mkuu wa Wilaya ya Kyela Bi Simalenga katikati mwenye suti Nyekundu,kushoto ni mwakilishi wa Mwenyekiti Kamati ya shule na Nyuma kabisa ni Mkuu wa Shule Bwana N.Sedekia pamoja na Wanafunzi na Wageni Wengine katika picha ya pamoja kwenye Tranfoma walipochukulia Umeme kuupeleka Shuleni mita chache kutoka hapo
Mkuu wa Wilaya akizindua kwa kuwasha Swichi kuu(Main Switch) Shuleni Mwaya
Mkuu wa Wilaya , Mwenyekiti wa Kamati ya shule, mkuu wa Wilaya na Kiongozi wa Skauti shuleni wakielekea kwenye Tranfoma palipochukuliwa Umeme
Mkuu wa wilaya ya Kyela Bi Magreth Simalenga leo asubuhi amezindua Nishati ya umeme katika Shule ya Sekondari Mwaya iliyopo Tarafa ya Ntebela Wilayani Kyela.Nishati ya Umeme katika Shule hiyo imekuwa ni moja ya changamoto ya muda mrefu kwa Waalimu na Wanafunzi hasa kwa kuzingatia kuwa shule hii imekuwa ikipata msaada kutoka kwa wadau mbalimbali. Miaka michache iliyopita Shule ya sekondari Mwaya ilipata msaada wa Kompyuta Mpakato kutoka shirika la Kimataifa lililoko nchini Marekani liitwalo Chocolate.
Hata hivyo licha ya msaada huo na mingine mingine mingi shule hiyo imekuwa ikikutana na Changamoto kubwa ya nishati hasa ya Umeme kwa ajili ya kusaidia uendeshaji na uendelezaji wa misaada hiyo ili kuleta tija kwa Wanafunzi hao. Umeme huo uliochukuliwa kutoka mita chache shuleni umezinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kyela na kushuhudiwa na wanafunzi na Mkuu wa Shule Bwana.N.Sedekia na Mwenyekiti wa Kamati ya shule.
Kupatikana kwa Umeme huo kunatarajiwa kuchangia kuongezeka kwa kiwango cha ubora wa Elimu itolewayo shuleni hapo na pia kupunguza Uzembe wa wanafunzi kwa maendeleo yao Binafsi.
0 comments :
Chapisha Maoni