Jumanne, 3 Desemba 2013

 Kocha Simba, Zdravko Logarusic akiwasili kwenye mazoezi ya timu hiyo  katika Uwanja wa Kinesi jijini Dar es Salaam. Kocha huyo amesaini mkataba wa miezi sita kuchukua nafasi ya Abdallah Kibadeni.
  Zdravko Logarusic akiingia uwanjani kuanza kazi yake.
Akiwasalimia mashabiki wa Simba.
 Akisalimiana na viongozi wa Simba.
 Wachezaji wa Simba wakijitambulisha kwa kocha wa timu hiyo kabla ya kuanza mazoezi.
 Zoezi la kujitambulisha kwa kocha likiendelea.
 Wachezaji wa Simba wakimsikiliza kocha mpya wa hiyo, Zdravko Logarusic wakati wa mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Kinesi jijini Dar es Salaam.
 Maelekezo ya kocha.
 Kusikiliza maelekezo.
 Wachezaji wakianza mazoezi.
 Aliyekuwa kipa wa timu ya Yanga, Yew Berko (kushoto) akijifua na wenzake wakati ea mazoezi ya Simba.
 Aliyekuwa kipa wa timu ya Yanga, Yew Berko (kushoto) akijifua na wenzake wakati ea mazoezi ya Simba.
 Kocha mpya wa Azam FC akiwa na msaidizi wake Kali Ongalla.
 .....Akizungumza na wachezaji...




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Engineer Felchesmi Mramba kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar Es Salaam jana, Jumatatu, Desemba 2, 2013, na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Florens Turuka inasema kuwa uteuzi huo umeanza  jana.

Kabla ya uteuzi wake, Eng. Mramba alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo la TANESCO.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
2 Desemba, 2013