Jumatano, 10 Juni 2015

Barabara ya kiwango cha udongo ilitengenezwa na Wanakijiji cha Malungo kwa nguvu za umoja wao
Madaraja ya mianzi ambayo yamekuwa changamoto kwa uchukuzi wa kijiji cha Malungo
MWENYEKITI WA KIJIJI CHA MALUNGO SETH MWAKASEKELE NA MWENYEKITI WA KITONGOJI CHA SERENGETI KILICHOPO NDANI YA KIJIJI CHA MALUNGO MBWELU MBAMBA WAKIWA SEHEMU KOROFI AMBAYO INAHITJIKA KUWEKA KARAVATI
Wananchi wa kijiji cha Malungo kata ya mwaya wilayano Kyela wameiomba serikali kuwasaidia katika juhudi zao za kukarabati miundombinu ya barabara hasa upande wa madaraja bora na ya kisasa
Wakiongea na mwandishi wa mtandao wako wa Nyumbani Mwenyekiti wa kijiji cha Malungo Seth Mwakasekele ameiomba serikali kuwasaidia madaraja ya kisasa katika maeneo korofi ya barabara za kijiji hicho. Kwa upande wake mwenyekiti wa kitongoji cha Serengeti bi Mbwelu Mbamba ameitaka serikali kusaidia sehemu ambazo nguvu kazi ya wananchi imeshindikana ikiwemo kuwawekea madaraja na makaravati. Kitongoji hicho asilimia kubwa kimetengeneza madaraja ya mianzi ambayo hayawezi kupitisha magari na pikipiki
Wananchi wa kitongoji cha Serengeti wameanza kutengeneza barabara za kitongoji hicho kwa kiwango cha udongo ambazo ni changamoto kubwa kwa muda mrefu. Mtandao wako wa Nyumbani unawaoma wananchi na serikali kwa ujumla kusaidia changamoto hii ya miundombinu kijiji Malungo
Imeandaliwa na Mwandishi wako wa Nyumbani Puyol B Mwasampeta

Jumanne, 9 Juni 2015

Mkurugenzi wa halmashauri ya kyela Cremes kasongo akitoa maelezo kwa watendaji wa kata,wavijiji,na wenyeviti wa vijiji wilayani Kyela kuhusu bei elekezi za kokoa nampunga ili kuwe na vituo vya kununuli na swala la ushuru wa kakao na mpuga
Watendaji wa kata,vijiji,na wenyeviti wa vijiji wa halmashauri ya kyela wakipata maelekezo ya bei elekezi zao la kokoa kwenye ukumbu wa halmashauri ya kyela
Halmashauri ya Wilaya Kyela jana imeendesha semia elekezi kwa watendaji wake wa Kata na vijiji kuhusu bei elekezi ya zao la kuu la biashara wilayani hapa ambapo ni shilingi elfu tatu(Tsh 3,000/=)
Akitoa maelekezo mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Kyela Bwana Clemence Kasongo amesema lengo kuu la kufanya hivyo ni kumfanya mkulima wa Wilayani kyela kunufaika na kilimo cha zao la kokoa na mazao mengine
Mkurugenzi huyo amesema kutakuwa na vituo vya kununulia mazao ili ushuru asilimia mbili(2%) zibaki kijijini hapo zifanye kazi kwenye kijiji.Maelekezo hayo yametolewa kwa zao la mpunga pale tu linapotumika kibiashara
Pia maelekezo yametolewa juu ya kudhibiti uuzaji na ununuaji wa kokoa mbichi kwa walanguzi ambao hufanya kilimo hicho kisiwe na tija kwa mkulima. Katika semina hiyo watendaji hawa wamekabidhiwa mamlaka ya kuwakamata wale wote ambao watakiuka maelekezo hayo.
KYELA Nyumbani inaipongeza Halmashauri kwa hatua hiyo na kuwataka watendaji kutekeleza maelekezo hayo kwa manufaa ya jamii wanayoitumikia .
Kibao cha shule ya Msingi kikionesha uelekeo wa shule ya msingi Mwakikome ilipo
Jengo mojawapo la shule ya Msingi Mwakikome
Katibu wa Chadema Kijiji cha Mpunguti bwana Elias Mwaijuni
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kijiji cha Mpunguti kata ya Katumbasongwe wilayani Kyela kimewataka wananchi wa kijiji hicho kuwa na subira juu ya kutimiza ahadi yao ya ujenzi wa kisima bora cha maji katika shule ya Msingi Mwakikome kijijini hapo.
Viongozi wa CHADEMA waliwahidi wananchi kuchimba kisima na kukijengea ukuta wa matofali na saruji katika shule ya msingi Mwakikome wakati wa kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika decemba 14 mwaka jana.
Chama hicho kilidai kuwa kitakamilisha ujenzi wa kisima hicho kabla ya kufungua shule mwezi januari mwaka huu lakini mpaka sasa kisima hicho hakijakamilika.
Akilitolea maelezo jambo hili mbele ya Mwandishi wa Mtandao wako wa nyumbani KYELA Nyumbani Katibu wa chama hicho tawi la mpunguti BwanaElias Mwaijuni amesema kuwa tayari wamenunua saruji na matofali kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kisima hicho na wao wanasubiri wakati wa kiangazi ili kisima hicho kiongezwe kuchimbwa ndipo wakijenge kwa ubora mkubwa.bwana Mwaijuni aliendelea kwa kuwahamasisha zaidi wananchi wa Mpunguti na Kyela kwa ujumla kushirikiana na viongozi wao ili kuyafikia maendeleo ya jamii yao kwa faida yao yote.Alimaliza kwa kusema CHADEMA wanaamini katika nguvu ya umma katika mabadiliko ya jamii.
Mtandao wako wa Nyumbani utaendelea kulifuatilia hili na litakapokamilika tutawaletea mrejesho watu wetu wa Nyumbani
Imeandaliwa na PUYOL B MWASAMPETA