Wengi tunafuga nyuki, tunakula asali lakini hatujui kama nyuki wana faida zaidi ya hizi hapa.
Wanasayansi kutoka chuo kikuu cha tiba Washington,
 Marekani  wamegundua katika utafiti wao kuwa sumu iliyopo katika mwili 
wa nyuki iitwayo toxin melittin inaweza kuvivunjavunja na kuviharibu 
virusi vya Ukimwi pasipo kuacha madhara katika chembehai za mwili.
Habari hii imeelezwa katika taarifa ya tiba za dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi iliyotolewa mapema mwaka huu.
Watafiti hawa wanaeleza kuwa matokeo ya utafiti 
huu kufika katika hatua kubwa inayoleta matumaini ya kupamba na VVU  kwa
 kuweza kupata dawa ya kupaka ya majimaji ndani ya uke itakayotumika 
kupambana na maambukizi ya VVU.
Dk Joshua Hood anasema: “Matumaini yetu ni kwa 
maeneo ambayo hali ya maambukizi yapo juu na vigumu kuzuilika, dawa ya 
majimaji mazito inaweza kutumika kupaka ndani ya uke katika kuzuia 
maambukizi ya mwanzoni kabisa.”
Sumu ya nyuki, melittin, imeonyesha uwezo wa 
kupambana na VVU kwa kuvunja ganda linalomzunguka kirusi na virusi 
wengine kwa kulitoboa na kuacha matundu.
Mwandishi mwandamizi wa makala za biokemia,  Dk 
Samuel Wicline, Profesa wa Biochemia wa Taasisi ya Russel Hornsby 
anafafanua kuwa kuwa vijipande vidogo vilivyoshindiliwa vya sumu ya 
nyuki vimeonyesha kuwa na tabia ya kuweza kuua chembe hai zenye 
saratani.
Anaeleza mtaalamu huyo kuwa hii si mara ya kwanza 
katika ugunduzi wa tiba ya namna hii, kwani mwaka 2004 wanasayansi wa 
Croatia walitoa taarifa yao katika jarida la sayansi ya chakula na 
kilimo kuwa mazao ya nyuki, ikiwamo asali na sumu ya nyuki  vina uwezo 
wa kutumika kutibu na kuzuia saratani.
Chembehai za mwilini zenye afya huendelea kubaki 
salama pasipo kupata madhara wakati wa tiba kwani sumu hiyo ya nyuki 
imetengenezewa na kitu kama ngao ambayo ikikutana na seli za mwili 
hudunda na kwenda mbali bila kujishikiza.
Hii ni kwa sababu ya seli za mwili ni kubwa 
kimaumbille kuliko sumu ya melittin, wakati kwa  virusi vya Ukimwi ni 
vidogo kuliko melittin, hivyo ikikutana navyo ngao hiyo haiwezi kuzuia 
kirusi kidunde kwani ni kidogo, hivyo  kirusi hudakwa na melittin na 
kushikamana, hivyo kirusi huweza kuharibiwa.
Dk Hood anaeleza kuwa vijipande vilivyoshibishwa 
na sumu ya melittin huweza kushikamana na kirusi na kutoboa tundu katika
 ganda la kirusi na kuchana ganda lote, hivyo kirusi huweza kuvunjwa.
Wakati tiba kwa kutumia dawa za kufubaza makali ya
 VVU, yaani ARVs zinafanya kazi kwa kuzuia uwezo wa virusi 
kujidurufisha, kwa tiba ya melittin hushambulia sehemu muhimu ya 
kimaumbile ya  virusi ambayo ndiyo nguzo imara kwa virusi
Jumamosi, Agosti 31, 2013
Unknown
0 comments :
Chapisha Maoni