Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, 
Maliasili na Mazingira imepanga kukutana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda 
na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna 
Tibaijuka ili waweze kuzungumzia ongezeko la kodi ya asilimia 10 ya 
mapato ghafi ya mashirika ambayo imesababisha kupanda kwa gharama za 
nyumba za Serikali.
“Ongezeko hili limechangia wananchi wa 
hali ya chini kushindwa kumudu gharama za nyumba, jambo ambalo 
linakwenda kinyume na mkakati wa Serikali wa maisha ni nyumba,”alisema 
Lembeli.
Hata hivyo kamati hiyo inashtukia kodi 
hiyo sasa , wakati Bunge la Bajeti ya mwaka 2013/14 wakiwamo wajumbe wa 
kamati walipitisha kodi ya asilimia 10 ya mapato ghafi kwa mashirika 
yanayozalisha kwa faida ili kuichangia Serikali.
Akizungumza katika kikao 
kilichoshirikisha watendaji wa NHC, Mwenyekiti wa kamati hiyo, James 
Lembeli alisema kuwa ongezeko hilo ni kubwa, na kwamba limesababisha 
kuongezeka kwa gharama za nyumba ambazo wananchi wa kawaida wanashindwa 
kuzinunua.
Aliongeza, kutokana na hali hiyo, 
viongozi hao watakaa pamoja na kuangalia namna ambavyo wanaweza kufanya 
ili waweze kupunguza gharama hizo, jambo ambalo litakwenda sambamba na 
mkakati wa Serikali wa kujenga nyumba za gharama nafuu kwa ajili ya 
wananchi wasio na kipato kikubwa.
Akitolea mfano wa nyumba ambayo ilikuwa 
inauzwa kwa gharama ya Sh30 milioni, sasa hivi inauzwa kwa gharama ya 
Sh100 milioni, jambo ambalo linaonyesha wazi kuwa, wananchi wenye kipato
 kidogo hawawezi kununua nyumba hizo.
Alibainisha kuwa, kutokana na hali hiyo,
 Serikali inapaswa kukaa pamoja na watendaji wake ili kuhakikisha kuwa, 
kodi hiyo inaondolewa, jambo ambalo linaweza kuwasaidia wananchi hao.
Hata hivyo, kamati hiyo imeutaka uongozi
 wa NHC, kurudisha hati za nyumba ambazo zilichukuliwa na baadhi ya 
wafanyabiashara wakubwa na kujimilikisha kinyume na taratibu.
“Kuna wafanyabiashara wakubwa wamechukua
 nyumba wakati wa utaifishaji, lakini waliambiwa warudishe hizo nyumba 
wamekataa kutoa hati,jambo ambalo linakwenda kinyume,”aliongeza.
Alifafanua, kutokana na hali hiyo, 
kamati hiyo imewataka watendaji wa shirika hilo kuhakikisha kuwa, nyumba
 hizo zinarudi mikononi mwao ili ziweze kutumika kwa manufaa ya 
wananchi.
Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa 
NHC,Nehemiah Mchechu alisema kuwa, ikiwa Serikali itapunguza kodi, 
gharama ya nyumba inaweza kupungua, jambo ambalo linaweza kuwasaidia 
wananchi wa kawaida kuzinunua.
“Tunaiomba Serikali kuangalia upya kodi zilizoongezeka, kwa sababu zimechangia kupanda kwa gharama za nyumba,”alisema Mchechu.
Alisema,mkakati uliopo ni kuhakikisha kuwa, miradi iliyoanzishwa inakwisha katika kipindi kilichopangwa ili iweze kutumika kwa wananchi.
Chanzo cha habari: Mwananchi
Alisema,mkakati uliopo ni kuhakikisha kuwa, miradi iliyoanzishwa inakwisha katika kipindi kilichopangwa ili iweze kutumika kwa wananchi.
Chanzo cha habari: Mwananchi
Jumatatu, Agosti 26, 2013
Unknown
0 comments :
Chapisha Maoni