JESHI LA POLISI kyela limezindua mradi wa Ulinzi Shirikishi katika tarafa ya Unyakyusa na Ntebela Wilayani hapa.
Shughuli nzima ya uzinduzi imefanyika katika ukumbi wa ofisi ya tarafa
ya unyakyusa kyecu,ambapo mgeni rasmi OCD Ngassa amewataka watendaji
kata kushirikiana na polisi kata ili kuleta ufanisi katika utendaji kazi
hasa katika swala zima la ulinzi wa amani. Amesema kutakuwa na
kikosi cha TAX-FORCE cha tarafa kitakachokuwa na askari wasiopungua
ishirini ili kuleta nguvu ya pamoja kwa tarafa zote mbili kwa lengo la
kuimarisha amani na usalama wa raia na mali zake kwakuwa usalama
katika tarafa ni usalama wa wawilaya nzima. Kamanda Ngasa ameomba
kuwepo kwa ushirikianao kutoka kwa makundi mbalimbali ya kijamii kwa
maana ya vijana na wazee kupeana taarifa ili kufichua uovu unao weza
kufanywa na kundi au mtu flani kutaka kuleta madhara,ameogeza kuwa swala
la ulinzi si la polisi na serikali peke yake bali ni lakila raia wa
Tanzania. Aidha amezungumzia pia kuwepo na operesheni kubwa ya pombe
haramu ya viroba kwa wilaya ya Kyela na Rungwe ,amewataka watendaji
kata na vijiji kufanya operesheni ya waagizaji na wanywaji wa pombe
haramu kuhakikisha wanakamtwa na kiisha kuchukuliwa hatua za kisheria.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kikao hicho afisa tarafa ya unyakyusa
Kheri William ametoa shukrani zake uongozi wa jeshi la polisi kyela
kuzindua tax force ya tarafa kitu amabacho amesema kitaimaarisha zaidi
usalama wa tarafa na wilaya kwa ujumla.
0 comments :
Chapisha Maoni