Vurugu kubwa zimetokea hapa jijini Mbeya ambapo wafanyabiashara katika soko la Mwanjelwa wameigomea mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) mkoani hapa wakidai inawashinikiza wananchi hao kununua vifaa vya Electronic Fiscal Devices(EFD) maalum kwa kuhakikisha mamlaka hiyo inarahisisha ukusanyaji wa kodi kirahisi na kwa umakini zaidi.
Wafanyabiashara hao wameilalamikia mamlaka hiyo kuwa inawashinikiza kutumia kifaa hicho wakati uwezo wa mitaji yao ni mdogo sana.Waliedelea kulalamika kuwa mamlaka hiyo imekuwa ikiwashinikiza kuwa kila mfanyabiashara mwenye mtaji usiopungua shilin gi za kitanzania elfu arobaini na tano(Tshs 45000) analazimika kutumia kifaa hicho katika kutoa risiti kwa uuzaji wa bidhaa zake ambapo kifaa hicho kinapatikana kwa shilingi zisizopungua laki nane .
Hata hivyo Kyela Nyumbani inaendelea na jitihada za kuwatafuta wanaohusika kujibu malalamikao hayo ya wananchi yaliyopelekea kutokea kwa vurugu hizo kubwa jijini hapa na kuathiri uchumi wa nchi kwa ujumla.
Baadhi ya watu wakiwa wanakimbia Baada ya Mabomu ya machozi kuanza kurushwa kuepusha vurugu
Mawe yakiwa yamepangwa kuzuia magari yasiende kokote
Maduka yote yakiwa yamefungwa eneo la mwanjelwa kupinga ununuzi wa mashine hizo za TRA
Vijana hawa wakiwa wananawa uso baada ya Bomu la machozi kuwapitia
Jiwe kubwa likiwa limewekwa katika Barabara magari yasipite
Wafanya Biashara wakiwa wanajiandaa kusikiliza mkutano
Mpaka sasa hivi tunapo toa ripoti hizi za moja kwa moja kutoka Jijini Mbeya kutokana na vurugu kubwa iliyozuka kwa wafanya biashara kugomea mashine za TRA, Sasa wafanya biashara hao wamerejea makwao ingawa kulikuwa na vugu vugu la Vijana vibaka kuleta vurugu lakini Jeshi la polisi limeweza kuwadhibiti wote na hali sasa imekuwa tulivu... Ingawa kulikuwa na Minong'ono kutoka kwa watu mbalimbali wakiomba hali hii kesho iwe shwari na kusiwe na vurugu tena..
0 comments :
Chapisha Maoni