Alhamisi, 7 Novemba 2013

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjFuP-1F9vgG4m8Xa0cez6I9XAtJihP17V2_l8QbFK1sOTHGdrkEpDYI2DduqZqkCHlELWWQ0fD4Xh8EuOOrzMlOJaH364E1XF9Ut9itNgjLWKx8qzqiV3ZeSbyMqCpesq4Sl3p8xegZOeO/s640/d.jpg
              Kocha mkuu wa Azam mwingerezaStewart Hall
Dakika chache baada ya mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Azam FC na Mbeya City ambapo Azam imechomoa dakika za mwishoni na kuishia sare ya bao 3 kwa 3, Kocha Stewart Hall ametangaza kuachana na Azam FC.




Hall amesema anaachana na Azam FC baada ya kupata ofa kubwa iliyomshawishi kuichukua.

Hata hivyo, kabla KYELA Nyumbani ilipata taarifa za uongozi wa Azam FC kumuambia Hall kwamba hahitajiki.

Hii ni mara ya pili anaondoka, kabla aliachishwa kazi na kurejea kwao England, baadaye akarudi na kutoa Kenya ambako aliifundisha Sofapaka.



Azam FC iliyomchukua Boris Bunjac wa Serbia walishindwana naye na baadaye na kumuita tena ainoe.




 Wachezaji wa Mbeya City wakifanya mazoezi mepesi kabla ya kuanza kwa mchezo wao dhidi ya Azam FC. 


  Kutoka juu wachezaji Mbeya City wakifanya mazoezi mepesi kabla ya kuanza kwa mchezo wa dhidi ya Azam FC.
 Mashabiki wengi wao wa Mbeya City wakiwa katika misururu mirefu kuingia uwanjani kushuhudia pambano la Azam na Mbeya City kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam. 
 Golikipa wa Mbeya City akiokoa moja ya hatari zilizoelekezwa langoni mwake katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara dhidi ya Azam FC unaoendelea kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.
 Mashabiki wa Mbeya City wakishangilia kwa hamasa kubwa.

0 comments :

Chapisha Maoni