Jumanne, 22 Aprili 2014

Wakati maafa ya mafuriko yakiendelea wilayani humu japo kwa kasi ndogo kumetokea na hali ya kustaajabisha ambapo katika bwawa maarufu kama caterpillar(Katapila) lililopo katika eneo la Mpanda kata ya Kyela mkabala na shule ya msingi Mpanda.Hali hiyo imewastaajabisha wakazi wengi kanakwamba wengine wamehusisha tukio hilo na imani za kishirikina.
Mamba huyo inasemekana kuwa waalikuwa wawili ambao walikuwa wanawasumbua sana watu kwa muda mrefu sasa.Watu wakaripoti katika mamlaka husika na ndipo maafisa wa maliasili wa wilaya wakaanza zoezi la kuwasaka mamba hao na kufanikiwa kumuua mmoja tarehe 22.4.2014 saa 10 jioni mwingine akiendelea kusakwa.
Kwa sasa amehifadhiwa katika ofisi za UJENZI wilaya zilizopo karibu na Uwanja wa mpira wa Mwakangale.

IMANI ZA KISHIRIKINA HAZIJAKOSEKANA
Mwandishi wa mtandao huu wa KYELANyumbani akizungumza na shuhuda mmoja eneo la tukio amesema "huyu mamba(aliyeuawa) na anaesakwa walikuwa wa mtu (mmliki kishirikina) aliyekuwa amewahifadhi kwenye hilo bwawa na walikuwa wanasumbua watu alafu watu wakienda kuwashangaa ikiwa ni hali ya kustaajabu basi kila mtu atakaeenda kuwaona mamba hao anazalisha gunia moja la mpunga shambani kwa mwenye mamba hao".Kama watu waliowahi kuwashangaa mamba hao ni 200 basi huyo mwenye Mamba hao atavuna gunia 200 za mpunga.Hatari sana na mazao yameharibiwa na mafuriko tusubiri watakao tuhumiwa

Mamba huyo anatarajiwa kuwa kitoweo kwa watumiaji kuanzia kesho kwani inasemekana mkuu wa wilaya bi.Magreth Simalenga ameagiza asichinjwe na kuchunwa hadi atakapomuona hiyo kesho tarehe 23.04.2014.ambapo watu waliokuwa wakisubiri kitoweo wameghadhibika kwa kucheleweshewa kitoweo chao.
                  Tunaendelea kufuatilia zaidi

Jumatatu, 21 Aprili 2014

Mvua zinazoendelea kunyesha wilayani Kyela zinaendelea kuleta maafa mbalimbali ikiwemo watu kupteza maisha na wakazi kupoteza mali na makazi yao.
Mwandishi wa mtandao huu akiwa anatembelea maeneo mbalimbali yaliyoathirika sana ambayo ni BUJONDE,KATUMBASONGWE(NDWANGA) MWAYA (MMWAJA) KAJUNJUMELE(NKILWA) na mengine mengi hadi hivi sasa anasema inakisiwa watu wasiopungua wanne wamepoteza maisha.Mtu mmmoja aliyejulikana kwa jina la MALINDO MWAIPOPO amekufa maji baada ya kusombwa na maji eneo la LUGOMBO MWAYA akijaribu kuvuka kuelekea Mwaya.Pia maeneo ya KATUMBASONGWE(ndwanga) kumeripotiwa kuwa kunadhaniwa watu wapatao watatu wamekufa maji.
"Uswe tukumilwa umwe mkusalala uko"Hii ni kauli ya mama mmoja aliekuwa akiongea kwenye simu akiwajulisha ndugu hali tete ya mafuriko wanavyo athirika, eneo daraja la mto Kiwila lililopo Ipyana maji yakipita juu ya daraja
hili ni eneo la barabara ya kuelekea  bandarini huko Kajunjumele 
vijana mbalimbali wakujitolea kusafisha daraja la Ipyana.
Hapa ni mbuga ya Tenende watu wakijaribu kupita.Ni hatari sana
hapa ni Kyela jamani na mafuriko ndo hayo
hapa ni eneo la makaburi ya Kyela mjini yamemezwa na mafuriko
EWE MWENYEZI MUNGU TUNAIWEKA KYELA MIKONONI MWAKO.

Jumamosi, 19 Aprili 2014

TAREHE 19/4/2014 Historia inaenda kuandikwa wilayani Kyela  "KYELA MISS EASTER 2014", Walimbwende na warembo kutoka wilayani Kyela wanaenda kupambana usiku wa leo kumpata mshindi. Tukio litaanza saa moja kamili usiku wa leo katika ukumbi wa SATIVA MIDLAND HOTEL,Washiriki wanamalizia session ya saloon tayari  kwa kwenda kufanya mahojiano redioni"KYELA FM 96.0"
Kutoka hapo ndio mpambano utakapoanza rasmi. 
na hatimaye Fanesti Asheri ametwaa taji la "KYELA MISS EASTER 2014" katika kinyang'anyiro kikali ambapo mrembo huyo amejinyakulia pesa taslimu Tsh 300000/= na offer ya kusoma ICT katika chuo cha MOSEMI College kilichopo wilayani hapa.mshindi wa pili amejinyakulia kiasi cha Tsh 200000/= na mshindi wa tatu kazawadiwa Tsh 150000/=







Miss Fanesti Ashery akiwa tayari keshatangazwa mshindi na tayari kukabidhiwa zawadi
...