Jumatatu, 19 Oktoba 2015

Timu ya MPUNGA CITY wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi Bwana Bedoni Gwatengile kabla ya fainali

Timu ya ISAMBULA FC wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi Bwana Bedoni Gwatengile kabla ya fainali

Bedoni Gwatengile akisoma risala kwa niaba ya Ezekiel Gwatengile wakati wa fainali za GWATENGILE CUP huko BUSOKELO
Bwana Bedoni Gwatengile akifuatilia kwa makini mchezo wa fainali ya GWATNGILE CUP

Mabingwa wa GWATENGILE CUP 2015 wakishangilia kikombe baada ya kukabidhiwa na Mgeni rasmi Bwana Bedoni Gwatengile jana huko BUSOKELO 
Bwana Bedoni  Gwatengile kwa niaba ya Ezekiel Gwatengile amekabidhi zawadi kwa mabingwa wa ligi ya GWATENGILE CUP  ambao ni timu ya Isambula Fc ambao ndio mabingwa wa ligi hiyo kwa kuwanyuka wapinzani wao mabingwa wa kihistoria Mpunga city goli moja lilofungwa na Lughano Mwantingo kwa njia ya penalti baada ya mabeki wa Mpunga city kuunawa mpira katika eneo la hatari wakati wa mechi ya fainali hiyo iliyokuwa na upinzani wa hali ya juu 
Zawadi kwa washindi wa ligi hiyo zilizokabidhiwa na Bwana Bedoni Gwatengile ambaye alikuwa mgeni rasmi ni kama ifuatavyo
1.Isambula kikombe cha dhahabu na seti moja ya jezi 
2.Mpunga City seti moja ya jezi 
3.mpira mmoja. 
Akikabidhi zawadi hizo Bedon Gwatengile kwa niaba ya Ezekiel Gwatengile amesema kuwa zawadi alizotoa haziwezi kulingana na thamani ya kazi walioifanya uwanjani ila zawadi hizo ni ishara tu ya kuwatambua washindi.
Amesema kuwa kama Mungu atampa uhai ataweka ligi ya jimbo mwakani itakayozishirikisha mshindi wa kwanza na wa pili wa kila kata ambapo jumla ya timu ishirini na nne(24), amewataka vijana kujituma ili waweze kupata ajira kupitia michezo na amesema ataviomba vyombo vya habari kuitangaza ligi hiyo ili wachezaji wapate soko.

Mwandishi ;Aidan Mwasampeta 0757337870
Mhariri; Martin Emanuel 0769858521
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la  MIICO Bwana ADAM SIWINGWA akiwaelekeza jambo baadhi ya wakulima waliohudhuria semina hiyo wilayanio Kyela juzi 
 Mkurugenzi wa Shirika la MIICO akiwapatia mafunzo wanakulima waliohudhuria semina hiyo 


Bi Catherine Mlaga akiwezesha semina kwa wanakijiji waliohudhuria semina iliyoandaliwa na shirika la MIICO
Majadiliano ya vikundi yakiendelea katika semina hiyo yakisimamiwa na Bi Catherine Mlaga
Mkuu wa wilaya ya Kyela Bi Thea Ntara akizungumza wakati wa uzinduzi wa semina hiyo ya uwezeshwaji kwa wakulima wa mpungawilayani Kyela




Mkuu wa wilaya akiwa na Kaimu afisa kilimo wa wilaya ya Kyela Bwana Paulo Sheyo wakati wa Semina hiyo


Mkuu wa wilaya Kyela akiwakabidhi baiskeli zilizotolewa na shirika la MIICO kwa wakulima waliohudhuria semina hiyo ya uwezeshaji wakulima wa kilimo cha mpunga wilayani Kyela
Shirika lisilo la kiserikali la MIICO kutoka jijini Mbeya juzi tarehe 16.10.2015 liliendesha semina ya kuwajengea uwezo baadhi ya wakulima wa kilimo cha mpunga wilayani Kyela
Semina hiypo iliyojumuisha washiriki ambao ni Wakulima kutoka vijiji kumi na sita ambavyo ni Katumba,Mpunguti, Isanga,Tenende, Bwato, Isuba,Makwale, Mahenge, Ngeleka, Katela, Kanga,Kafundo, Mubunga, Kingili,Ngana na Mpunguti ya Makwale. 
Mfanyakazi na mwezeshaji  wa shirika la Miico lenye makao makuu jijini Mbeya nane nane  Bi Catherine Mlaga amesema kuwa shirika hilo linafanya kazi na wakulima wa mikoa minne ambayo ni Morogoro,Iringa, Rukwa na Mbeya na wilaya sita zinanufaika na miradi yao. 
Pamoja na kuwapatia wakulima mafunzo jinsi ya uzalishaji wa mpunga pia shirika la MIICO limetoa baiskeli kumi na sita (16) kwa vijiji vinavyonufaika na mradi huo. 
Akikabidhi baiskeli hizo mkuu wa wilaya ya Kyela bi Thea Ntara amelishukuru shirika la MIICO kwa kuja wilayani Kyela na kuwafundisha wakulima wa zao la mpunga na kuwaomba MIICO kuendelea kufanya hivyo mara kwa mara wilayani Kyela. 
Ameliomba shirika hilo kuwapeleka baadhi ya wakulima nje ya nchi ili wakajifunze na kubadilishana mawazo na wakulima wa mpunga wa nje ya Tanzania. 
Mkuu wa wilaya pia  amewaomba wakulima hasa wanaume kutowanyanyasa wake zao hasa kipindi cha mavuno ambapo amesema kuwa wanaume wengi wakivuna mpunga wanakuwa wakali kitu ambacho kinasababisha mpunga kuisha bila mwanamke kujua na kuleta mfalakano ndani ya nyumba.
Mkuuwa wilaya hakusita kuwaomba wananchi wa wilayani Kyela na Nchini kwa ujumla kushiriki kwa amani katika zoezi lijalo la Uchaguzio mkuu Tanzania kwa kutimiza wajibu wao na kufuata na kutii sheria za uchaguzi...Amesisitiza sana wajibu wa wananchi katika kuilinda amani yao.... 

Mwandishi ;Aidan Mwasampeta 0757337870
Mhariri; Martin Emanuel 0769858521

Jumamosi, 17 Oktoba 2015

Mkuu wa wilaya ya Rungwe Bi Zainab Mbuussi akiwavalisha vijana fulana zenye nembo ya FEMA

 Mkuu wa wilaya akiwa na baadhi ya watoto katika picha ya pamoja 


Mkuu wa wilaya ya Rungwe  akiwa meza kuu akifuatilia kwa makini matukio mbalimbali siku ya Tamasha la kuombea Amani 

Wachezaji wa ngoma ya asili ya kinyakyusa maarufu LING'OMA wakitumbuiza siku ya Tamasha

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Tukuyu wakifikisha ujumbe kwa hadhira iliyohudhuria Tamasha hilo kwa njia ya sanaa ya Maigizo.

Vijana wakionyesha vipaji vyao kwa njia ya Sarakasi




Shirika la Karibu Tanzania likishirikiana na UNDP ana Fema waliandaa tamasha la kuombea amani kwa Taifa letu la Tanzania kuelekea Uchaguzi mkuu wa Rais ,Wabunge na Madiwani
Tamasha hilo lilifanyika tarehe 11.10.2015 siku ya jumapili katika chuo cha maendeleo ya wananchi Katumba kilichopo nje kidogo ya mji wa Rungwe ambapo mgeni rasmi wa tamasha hilio la kuhamasisha amani alikuwa mkuu wa wilaya ya Rungwe bi Zainabu Mbussi. Amewataka vijana kutotumika na wanasiasa kuvunja amani kwani bila amani hakuna maendeleo yatakayofanyika. 
Ameyasema hayo kwenye tamasha liloandaliwa na shirika hilo na kufadhiliwa na UNDP amesema kuwa lengo la tamasha hilo ni kuhamasisha amani ya Tanzania. 
Kwa upande wake mgeni rasmi huyo amewashukuru waandaaji wa tamasha hilo kwa kuichagua wilaya yake kufanyia tamasha hilo. 
Katika tamasha hilo kulikuwa na burudani mbali mbali kama vile maigizo, mziki na vingine vingi vya burudani katika vikundi hivyo vilionekana kumvutia mkuu wa wilaya na kumuagiza mkuu wa chuo hicho kumtafuta mwalimu wa sanaa ili kuzalisha wasanii na waigizaji watakaoitangaza wilaya ya Rungwe.


Mwandishi ;Aidan Mwasampeta 0757337870
Mhariri; Martin Emanuel 0769858521